Twenzetu Uganda: Jinsi ya kununua hisa za MTN Uganda

KingOligarchy

Member
Sep 28, 2013
85
150
Uwekezaji nikiimanisha (investment ) ni jambo la busara kwa kila mtu sababu linatengeneza Passive income. Tukija kwenye masuala ya Hisa ama Stocks wale wanaoinvest kwa mfumo wa kupata Dividend na sio speculation mara nyingi wanatoboa sana,sababu eventually price ya hisa mara nyingi itakuja kuwa stable. wacha nije kwenye Topic

MTN Uganda ndo tunamwita tycoon wa Mitandao ya simu yote uganda , ambapo ana share ya market kwa asilimia 53% , yani kama vodacom alivyo Tanzania.

Kimsingi , MTN uganda kwa miaka mingi huwa natengeneza faida

RankName of OperatorMarket Share (%)
1MTN Uganda53.0
2Airtel Uganda35.3
3Africell Uganda4.2

sasa kutokana na sera za huko UG , MTN uganda inabidi afloat 20% ya hisa zake kwa wananchi kupitia Uganda stock exchange yenye watu 40,000 tu, ukisikia USE (Ugandan stock exchange) wanakwambia kwamba wanategemea kupitia IPO hii users watafika 200,000 (BIG DOUBT - STORY HIZI) anyway tuachane na hayo. so MTN Uganda kama anafloat hizo hisa maana yake kipindi cha kizuri cha kununua hisa ni sasa kutokana na hivyo kuna maswali ya watu wengi nilikuwa napata

1. JE NAWEZAJE KUNUNUA HISA ZA MTN UGANDA
Africa mashariki tunaruhusiwa kushiriki kwenye mchakato wa kununua hisa , ambapo ili tuweze kununua hisa lazima kwanza tutafute dalali anaetambulika na Uganda Stock exchange, ambao ni kama Baroda capital markets (uganda), Equity stock brokers, crested capital old mutual and sbg securities. kama unavyowaona hapo chini


1634027324743.png


Ili ufungua akaunti vitu vifuatavyo vinahitajika kwa watu wa Afrika mashariki:

1.2. Individuals (East African)

a) 3 coloured passport Photos

b) Identification Documents(National IDs, Passport only)

c) Fully Filled and Executed Form 1A

d) A summary of the nature of business activities that the person is engaged in or details of source of income

e) A disclosure of the risk appetite of the client

SWALI LA PILI: JE GHARAMA YA HISA MOJA NI TSH NGAP

MTN inauza kila hisa yake kwa gharama ya UGX 200 (hisa 4,477,808,848) kwa gharama ya kitanzania TSH 128

1634027553199.png


SWALI LA TATU: HIKI SIO KITU KIPYA KWANGU, NIMEWAHI NUNUA HISA ZA VODACOM TANZANIA LAKINI SIOJAONA MABADILIKO YOYOTE YA BEI.
Ni kweli yawezekana kwamba sio kitu kipya kwako, lakini mara nyingi kwenye masoko ya hisa kuna aina mbili pia la watu wanainvest, naweza nikaita SPECULATORS - watu wanaoinvest ili bei ibadilike wauze (asilimia kubwa kunsi hili ni kundi la kifo ) na Wale waonaoinvest kwa ajili ya DIVIDEND (tunaita Gawio ) (hili ndo kundi tamu kuliko yote).

wacha nielezee kidogo, unapofanya investment kwenye hisa unategemea vitu viwili moja. Capital/price appreciation na kupata Gawio (dividend). hivi vyote unaweza ukavipata ongezeko lake kwa mwaka kupita mahesabu. mara nyingi wengi amabao wanaingia kwenye hisa wanapenda kuspeculate hela ipande then wauze na endapo inapotokea price imeshuka wanaumia ,hili ndo kundi kubwa . lakini kundi dogo kama la wakina warren buffet kazi yao ni kuinvest kwenye makampuni kwa malengo ya Dividend ambapo ikiaminika kwamba huko mbele price itastabalize, sababu mpango ni kununua hisa na kuzihold kwa minimum 10-15 years.

sasa mtu wa divided huwa anaangalia bei ya hisa na dividend itakayotoka halafu anapiga mahesabu asilimia atakayopata. mfano mwaka 2019 Bei ya hisa ya crdb ilishuka mpaka tsh 90. lakini gawio la crdb lilikuwa kama TSH 22, maana yake kwa hisa uliyonunua ulipata return ya 22/90*100 24% per annum. nb( gawio huabadilika mwaka kwa mwaka) , lakini mpaka kipindi hiki leo 2021 crdb ipo bei ya 250. so kwa yule alienunua kwa kufocus na divid end tu ni ndani ya miaka 4 hela yake imerudi baada ya hapo ataendelea kula hela safi kabisa bila shida kwa maisha yake ceteris paribus. lakini pia mtaji wake umekuwa maradufu ndani ya miaka hii miwili.

kuna mifano hai mingi tu lakini the point is INVEST KWA KUFOCUS ON DIVIDEND ZINAZOTOKA KILA MWAKA NA SIO PRICE,

sasa basi kutokana na hilo najibu kwa mfumo wa yule alieuliza ishu ya vodacom, kama ulikuwa umeinvest kwa sababu ya capital/price appreciation pole sana, sababu hii ilikuwa speculation lakini kwa yule alieinvest kwa dividend maisha nin mduno since day 1 ukiachia vichangamoto vidogovidogo vya juzi,najua naongea technical kidogo but hopeful it makes sense


sasa comin to MTN, tukiwa tuna focus kwenye dividend hebu tuangalie faida mabazo zimetangazwa huko nyuma na MTN , nikimaanisha magawio waliyotoa kwa wamiliki wake kabla

1634028771807.png


Kwa miaka minne , MTN imekuwa ikigawa gawio tamu sana kwa kila hisa moja , ambapo faida imekuwa ikipanda kutoka bilioni 102 mpaka bilioni 154, ambapo 2020 faida ilipungua kidogo kwa bilioni 1 . lakini yet mapato kwa kila hisa moja yalipanda kutoka tsh 27 mpaka tsh 41. SAFI SANA HII

Hii inamaanisha nini? kwa lugha nyepesi ni kwamba kama hisa moja itauzwa ugxx200 na mwakani wakatoa gawio la tsh 40 kwa kila hisa maana yake return yako ni 40/200*100 = 20%. kwahyo kuna hat hati ya kila mwaka kuingiza 20%-25% kamouni ikifanya vizuri, 15%-20% kampuni ikifanya vibaya, 10%-15% ikifanya vibaya sana.Bado hapa ni pazuri kwasabau 25Yrs bond tu ya tanzania return yake ni 15.95% so ni kubwa kuliko ,YANI EMERGING MARKET FUNDS wakipiga hesabu zao na kuona hili kazi yao itakuwa ni kumwaga mzigo tu, haklafu wakimaliza mambo yao wataexist market kwa Block trades(anyway tuachane na hili) . so all in all kwa dividend investing its a go ahead.

tuangalie kidogo prospectus inasemaje:

PFA,


JE LISTING ZA MTN NI TAREHE NGAPI

1634029225651.png

mZIGO Mzima unapatikana USE (uganda stock exchange) kama tarehe zilivyoonesha hapo juu

JE KUNA RISK GANI MIMI KUINVEST NJE YA NCHI YANGU:

Risk kubwa ni Capital Flight sababu tunapeleka mtaji nchi nyingine, lakini hii naiassociate na Exchange rate risk . amabapo pale unapopata faida yako lazima ubadilishe from ugx kuja Tsh, ambapo kuna uwezejkano wa upotezaji wa fedha kwenye shughuli hii. risk nyingine zipo ndogo ndoogo tu ndo maana sijaziongelea, sio relevant sana

tuishie kidogo hapo, lakini mambo mengine ntaendeleea andika.

KAZI IENDELEEE
 

Attachments

  • MTNU-IPO-Full-Prospectus-11.10.21.pdf
    18.7 MB · Views: 10

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,244
2,000
Nimetumiwa message wana hisa wa voda tunakikao keshokutwa

Haya mambo siyajui vizuri lakini matamu
 

ngawia

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
523
500
Uzi umekosa wachangiaji wabobez wa finance wako wapi ingekuwa koneksheni ingepata wachangiaji wengi Sana...
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,228
2,000
MTN si kwa uganda nazani ndo kampuni kubwa kabisa ya mawasilioan Africa, jamaa wapo jadi huko kwa Wataleban, kama unafuatilia ile kashifa kwba walikuwa wanawahonga pesa Watalibani ili wasilipue minara yao
 

Kiduila

Senior Member
Jun 22, 2017
173
250
DSE wanayo App, mie nimejiunga kwa kutumia njia hiyo. USE hawana App? Naona kwa njia ya App ni rahisi kujiunga hasa kwa sisi tuliokuwa mbali.
 

Ntakasime

Senior Member
May 30, 2014
119
225
We jamaa una akili sana. Kiukweli wabongo kenye elimu ya masoko ya fedha tulilala kupiliza. Lakini angalau saizi tumeanza kuamka. Ndo maana ukiangalia hata huko kwenye Tbond mambo ni fire. Ushindani kama wote yani. Mm niwasihi Watanzania wenzangu tuamke! tuamke! Ni kweli tuliowengi vipato vyetu ni kiduchu. Lakini si mbaya kwa kiasi hicho hichho kidogo tukugawe katika mipango ya muda mfupi(kuwekeza kwenye biashara za kawaida kwenye maeneo yetu)na mipango ya muda mrefu( kuwekeza kwenye masoko ya fedha) hii itatufanya siku moja tuje kuwa na uhuru wa kifedha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom