Twaha Omari amefariki dunia

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Wana JF na wapenzi wote wa medani ya soka nawaletea taarifa ya kusikitisha kwamba Mchezaji wa zamani wa African Sports ya Tanga, Majimaji ya Songea, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mirambo ya Tabora na Reli Morogoro TWAHA OMARI (RIP) amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili mara tu baada ya kufikishwa kwa tatizo la shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa habari za ndugu wa karibu mwili wa marehemu utasafirishwa leo mchana na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao huko Korogwe Tanga.
 
https://www.jamiiforums.com/sports-and-entertainment-forum/28271-kunani-tanga-kwenye-soka.html


[h=2][/h][h=3]AFRICAN SPORTS VS. COASTAL UNION ENZI HIZO[/h]


napenda kuchukua fursa hii kuwauliza wakazi wa Tanga kulikoni soka mkoani hapo limepotea kabisa kulikuwa na timu za kutisha kama hizi

COASTAL UNION

1.HAMISI MAKENE 2.SAID KORONGO 3.DOGLAS MUHANI 4.JOSEPH LAZARO 5.YASINI NAPILI 6.KASSA MUSSA 7.MOHAMEDI KAMPIRA 8.ALLY MAUMBA 9.JUMA MGUNDA 10.HUSSEIN MAKURUZO 11.RAZACK YUSUPH

AFRICAN SPORTS

1.DANCUN MWAMBA/SALIMU WAZIRI 2.FRANCIS MANDOZA 3.BAKARI TUTU 4.HASSAN BANDA 5.MHANDO MDEVE (C) FATHER 6.RAPHAEL JOHN 7.ABBAS MCHEMBA 8.TWAHA OMARI 9.VICTOR MKANWA 10.MCHUNGA BAKARI 11.JUMA BURHANI(KAKOKO) RESERVE 1.ALLY MTUMWA 2.DONALD SEMKIWA 3.OMARI SELEMANI(MWARABU) 4.MARTIN MAHIMBO 5.DADI PHARESS 6.HAMZA MANENO 7.MWARAMI MGUMBA 8.ABDUL

KOCHA

1.SILSAID MZIRAY 2.ABDALLAH MABUDAH
 
Mungu amrehemu.
Wakuu inabidi tujifunze kupima afya zetu maana haya mashinikizo ya damu yamezidi kutuondoa mapema sasa
 
Dadi phares namuona mwanza town hapa ameajiriwa na kampuni fulani ya tours kama dereva wa kupeleka watalii mbuga za wanyama serengeti.
 
Mazishi ya Twaha Omari RIP ni leo huko Korogwe Tanga, nje kidogo ya mji wa Korogwe kijijini Rwengela, wakaribu huko tuwakilisheni wadau.
 
RIP Twaha Omar....Twaha Omar ninaye mfahamu mimi alikuwa mtu pole na mkarimu,akitokea kijiji cha kerenge nje kidogo ya mji wa Korogwe,ilimchukua muda mrefu kuonekana kipaja chake katika medani ya soka ukizingatia kabla hajajiunga na African Sport alihangaika sana kupata Timu ya uhakika,katikati ya miaka ya 80 alikuwa akichezea Timu moja ikiwa daraja la tatu Kilole United pale wilayani Korogwe alijaribu Biashara Shinyanga bila mafanikio.na baada African Sports kupanda daraja ndio na yeye alipopata nafasi kucheza ligi daraja la kwanza,na hawa African Sport walivutiwa na Twaha Omar walipomuona katika mchezo wa kirafiki kati ya Yanga v Nyota ya Korogwe..ingawa hakuwahi kuchezea nyota rasmi lakini mara nyingi hawa nyota katikati miaka ya 80 walikuwa na deturi ya kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa zinapokuja mkoani Tanga hivyo kutokana na kipaji chake mara nyingi walikuwa wanamuomba ktk mechi kubwa za kirafiki...
Alipojiunga na African Sport kipaji chake kilionekana zaidi wakati ule akishirikiana ktk nafasi ya kiungo na marehemu Abasi Mchemba,Rafael John.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amin!
 
Back
Top Bottom