Ameachiwa Kwa mbinde usiku huu kwa Masharti ya kuwa na wadhamini wawili , hata hivyo anatakiwa kuripoti tena polisi tarehe 8/7/2022 .
Tulishasema tangu awali kwamba Polisi haina hata sababu moja ya ukweli ya kukamata vijana wa Chadema , oneni wenyewe , unamkamata kijana wa watu unamzungusha mavituo yoooote , tena kwa gharama ya serikali , halafu unamuachia bila hata kumpeleka mahakamani !
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliopiga kelele kila mahali hadi watesaji wakaona Aibu na kumwachia , LEO NI MWAIPAYA , JUZI NI MO , KESHO NI WEWE , ni lazima tushirikiane kupinga Uharamia .