TVE, mmekonga nyoyo za watazamaji

TVE, mmekonga nyoyo za watazamaji

Gini

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
399
Reaction score
386
TVE, mmekonga nyoyo za watazamaji!

Na Mwl Sylvester, George Wambura
Twitter @PGGeorgeJr Instagram @pg_georgejr
+255716109169
georgesylvester35@yahoo.com

Tukiwa bado katika sekeseke la ugonjwa wa homa kali ya mapafu yaani Covid-19 (Coronavirus) huku shughuli karibia nyingi zikisimama katika mataifa mengi duniani kama Michezo n.k, taasisi za burudani duniani zimekuwa zikiandaa program kadhaa katika kuwaburudisha watazamaji ambao nchi zao ziko katika lockdown ama zuio la kutotoka ndani ili kukabiliana na janga hili. Hapa Tanzania pia TVE wamekuja na kipindi kinachoitwa HOMA, kinachobeba maudhui ya burudani na kurushwa LIVE.

Pamoja na Tanzania kutofanya ile inaitwa lockdown lakini wazo la HOMA limejikita katika kuburudisha watazamaji siku ya Ijumaa saa 3-5 usiku baada ya siku nzima masikio yao yakijaa taarifa za Corona huku wengine wakiwa katika pirika pirika za kuziba midomo na pua kwa BARAKAO ili kuzuia na kujikinga. Sema zile barakoa za vitenge au vitambaa usipokuwa makini huvuti hewa, hewa inayopita kuingia ndani na kukusaidia kuendelea ku survive ni ndogo sana, inakubidi uibenjue hivi kidogo uvute hewa kisha uirudishie yaani hatari hatari, inshallah mwenyezi Mungu atuepushe na janga hili.

TVE ikiwa inafanya shughuli zake chini ya mwamvuli wa E-FM Company Limited inayomiliki pia Radio ya E-FM, inatajwa kumilikiwa na ndugu watatu wa familia moja ya Ciza ambao ni Francis Antony Ciza (Majizo) akimiliki hisa 40%, Jean Claude Ciza anayemiliki 40% ya hisa na Justine Antoine Ciza mwenye hisa 20%. Hii ni kwa mujibu wa MEDIA OWNERSHIP MONITOR TANZANIA TV E ambao taarifa hizi zimepatikana kutoka katika vyanzo kama, Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyanzo vingine huku Majizo akitajwa kuwa ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni (CEO).

Hayo sio muhimu sana, hapa nililenga kuongelea kipindi cha Homa ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa hasa kutokana na radha ya mziki mzuri unaopigwa na bendi, ni tofauti na mziki wakutumia playback, mziki wa LIVE unahitaji uwe na vocal, pumzi na wimbo uuimbe kulingana na vyombo. Hapa unapata radha yenyewe sio ile mikono juuuu, piga keleleeee, say oooohhhhhh.

Wadau wamekuwa wakitamani sana Ssebo kufanyiwa sub (substitution) na aingie mchezaji energetic maana Ssebo wa FNL ya EATV sio huyu wa TVE, umri umemtupa mkono na kasi ya vijana kama haimudu hivi. Ni kama game ya soka, ukiwa na straika mwenye miaka 35+ ni ngumu kuipita beki kisiki kama Vigil Van Dijk. Ssebo OUT Jonijoo IN. Yes, hapa tutaoa magoli mengi maana mchezaji aliyeingia ni bonge la mfungaji mwenye ma skills ya kufumania nyavu. Uzuri Ssebo hajamaindi kuwa substituted kama tulivyoona Ozil mzee wa kumaindi wakati timu inahitaji ushindi, mashabiki wa Arsenal wanaelewa hili vizuri tu.

Kwa upande wangu naona Management ya TVE imefanya jambo la busara mno na ieleweke kuwa, Ssebo ni mzuri ila watazamaji wanataka kupata radha tofauti ya uulizaji maswali pamoja na swagg. Ssebo tutakupa namba katika zile mechi za maveterani bob, we relax tu. Naamini kuanzia Ijumaa hii katika HOMA mitaa inasubiri, hapa Barbana Clasic pale Jonijoo. Hakuna asiyejua uwezo wa Barnaba Boy katika kuzitendea haki lines za ngoma zake, ukiongelea mwanamuziki unamuongelea Barnaba na wengine. Hope jukwaa litataradadi na burudani kabambe itawakosha mioyo watazamani. Wapwa, kiu yenu imekatwa, HOMA.
Tchao!, until next time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri waje vijana wa naniihii wakurukie kama mwewe
 
Back
Top Bottom