TV zetu Zitatusaidia katika Mchakato wa Kupata Katiba mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV zetu Zitatusaidia katika Mchakato wa Kupata Katiba mpya?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Gurudumu, Apr 7, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Leo tarehe 7 April, tukio muhimu lilikuwa ni wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada wa kutunga sheria ya kutunga katiba mpya Tanzania. Binafsi nilitarajia kuona live coverage ya angalau tv mojawapo zilizopo tz

  Asubuhi Star tv wakatangaza kwamba kuanzia saa tatu na nusu wataanza kurusha coverage live ya mjadala kutoka Dodoma ukumbi wa Msekwa. Muda ulipofika kwenye screen ikaandikwa kwamba ni live lakini kukawa kuna mjadala kati ya mtangazaji na mwanasheria fulani huko mwanza ambao uliboa sana. Muda fulani katika background wakaonesha watu kwenye ukumbi wa Msekwa wakiongea kuashiria kwamba mjadala umeshaanza lakini sauti hazisikiki. Kisha wakaaga wakaendelewa na vipindi vingine visivyo na tija.

  TV zingine zilikuwa zinaendelea na ama tamthilia, muziki, na mambo mengine ambayo sikuona kama yalikuwa ya muhimu kwa watanzania kuliko mjadala wa public hearing zilizofanyika leo Dodoma, Zanzibar na Dsm.

  Wakati huo huo, Citizen tv ya Kenya ilikuwa inafanya live coverage ya kesi ya wakenya iliyokuwa inasomwa kwa mara ya kwanza huko The Hegue. Wakati wa mchakato wa katiba mpya ya Kenya, nilifuatilia matukio mengi muhimu live kupitia tv za kenya, kwa kadri nilivyopata muda.

  Tukumbuke kwamba live coverage ndiyo inayoaminika zaidi kuliko news clips ambazo zinaweza kuwa zimetomaswa kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Taarifa za kilichokuwa kinajiri Dodoma zilisambaa haraka sana kupitia SMS na blogs. Kwa tv yeyote ambayo lengo lake ni kuhabarisha wananchi ingeunganisha mara moja live ili wananchi watazame na kusikia kinachotokea.

  Binafsi ningefurahi sana kupata maelezo nini kilitokea na nini kitatokea huko mbele tukizingatia safari hii ya katiba mpya tz ndiyo kwanza tunaianza.
   
 2. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,370
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kubwa sana kati ya wakenya na sisi na hasa linapokuja suala la utaifa, binafsi wakenya ni inquisitive kuliko sisi. Nakubali kusahihishwa, citizen tv japokuwa ni mali binafsi inatumikia umma wa wakenya, nami nilifuatilia mchakato wa kuandika katiba ya kenya, ilikuwa ni fursa ya kila mmoja kuona na kushiriki huku matukio yote yakioneshwa moja kwa moja.

  Hapa kwetu, TBC inachojua nu kucover mikutano ya ccm na miss ni nini sijui, chombo hiki cha umma kinalala kitanda kimoja na serikali badala ya kuwa pamoja na umma:disapointed:
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine wakishapokea amri kutoka serikali hata uwalipe bei gani hawatarusha live na inawezekana hata wasiweke kwenye habari. Hakuna tofauti ya tv za binafsi na ile ya umma
   
 4. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kaka....kaka....kakaaaa! Nakubaliana na wewe kwa asil.100 mkuu. Hata mimi leo wameniboa sana hawa wamiliki wa local tv zetu....lakini si bure labda wamepigwa bann kutokana na ile zomea zomea ya mkhuruma hall....si unajua mbinu za ccm? Lakini moto uliowashwa leo pale karimjee hall na Dodoma wenyewe wamejionea.....na kama wanaakili basi wajue kuwa watanzania wa sasa si wale tena wa mwaka 47.
  Pili sikunyingi sana sijakuona hapa jamvini kulikoni mkuu? usalama upo?
   
 5. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilitazama taarifa ya habari usiku huu Channel ten walionesha both Dar na Dodoma. Sikupata habati ya kuona chochote tv zingine, kuna aliyeona kama wameonesha?
   
 6. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka hapo kuna tatizo ubwa ingawa watu hawaonekani kujali sana kama itaendelea hivi tutarajie mamo yaleyale ya kulindana na si vinginevyo
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nipo mkuu, majukumu, nikaamua kujipa ban kidogo. Nashukuru kunikumbuka
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama TV zilirusha jinsi kura original za urais 2010 zilivyokuwa zinahesabiwa na kujumlisha kabla ya kuleta ile chakachua yao basi tarajia the same trend kwenye mchakato wa katiba kwani ni sawa kujumlisha kula halali za urais CCM wasizojua ni ngapi zao na ngapi za wapinzani mbale ya watu wote. Ni hatari sana kwa masilahi yao na genge lao lote la wapora nchi. Transparent Mchakato wa katiba ni msumari wa moto kwenye heart of CCM, kama ilivyo kuruhusu watu kujumlisha matokeo ya kura za urais na kutangaza, unakumbuka DTV na uchaguzi wa 1995 Zanzibar walipotangaza Seif kashinda kwa kujumlisha kura wao wenyewe walifanywa nini?, walipigwa fine ya milioni tano na kutungwa sheria ya kukataza mtu yeyote asiye tume kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi, hao ndiyo CCM wanapendwa kwelikweli na wananchi na watatawala mpaka 2099
   
 9. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimeona kama star tv watarusha mjadala wa Dom kuanzia saa 4.30 usiku! Kuna mtu anasema ni baada ya Bunge kuzuia kwenda live! Labda halikutaka fujo ziende live
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Edited tape, only positives views on the eyes of CCM will get chance, with few negatives close to their side to give the programme little credibility. Don't waste your time to watch it.
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jamani hizo fujo ni zipi? Kwa nini wananchi wakihamasika serikali inasema ni fujo?
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Zingatia kwamba kesho ni siku ya kazi kwa hivyo muda huo wa saa 4:30 ni kupunguza kwa kiwango kikubwa sana watazamaji. Am sure maeneo mengi umeme utakatwa pia!
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Taarifa ya habari ya itv saa mbili usiku nao walionyesha pia!
   
 14. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumaini la watanzania katika habari zinazohusu taifa limebaki kwa IPP media peke yake kwani hao wameonyesha kila kitu ikiwemo ile ya tambe kuzomewa kwa kuzungumza pumba!! lakin9i hilo ni tv lenu mnaloliita la taifa hamna kitu kabisa halijui hata maana ya utaifa ila tutadili nao kwani sio chombo cha CCM ni cha dwananchi!!
   
 15. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka mimi nakupongeza sana kwa kuanzisha mada hii kwani vyombo vya habari ni mhimu sana katika mchakato wa kupata katiba mpya tukilifumbia macho tutajikuta tunarudi kulekule!! Naomba wadau tusipuuze hili kwani ni jambo mhimu sana tujadili na tupate suluhisho kwa ajili ya jambo hili kwamba tuhakikishe CCM hawahodhi vyombo vya umma hasa katika kipindi hichi cha mchakato
   
 16. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumaini la watanzania katika habari zinazohusu taifa limebaki kwa IPP media peke yake kwani hao wameonyesha kila kitu ikiwemo ile ya tambe kuzomewa kwa kuzungumza pumba!! lakin9i hilo ni tv lenu mnaloliita la taifa hamna kitu kabisa halijui hata maana ya utaifa ila tutadili nao kwani sio chombo cha CCM ni cha dwananchi!!
   
 17. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuwatie moyo ITV kwani wanaonyesha ndio pekee wanaotoa taarifa bila uoga wala kigugumizi
   
 18. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ingawa itv nao siyo wasafi sana, nadhani uwezo wao wa kufanya live coverage ni mdogo sana, hasa nje ya mkoa wa dsm
   
Loading...