TV Ya JF: Ushauri Kwa Mwanasiasa Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV Ya JF: Ushauri Kwa Mwanasiasa Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, May 22, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Dini plus Siasa = HAPANA
  Siasa plus Dini = NDIYO

  NILIKUWA nimekaa mbele ya Kompyuta yangu nikiharii safari ya Mheshimiwa hendisamu kule USA, nilipojiwa na jamaa yangu ambaye alikuja kunitaka ushauri, yeye ni mmoja wa vijana wa chama tawala... kwani safari hii naye anataka kuingia kwenye ulingo wa kugombea ubunge. Huyu bwana ikabidi achukue ule muda wangu wa kwenda kurekodi kwenye ile Television ya luninga JF. Kwa hiyo amewakosesha watizamaji wa Tivii ya luninga wiki hii, japokuwa mkanda upo tayari wa safari ya Vasco da Gama wetu. Ndugu msomaji wangu utanisamehe sana kwa kutokuwaletea Tivii ya luninga kwa wiki hii...

  Mazungumzo yetu yalikuwa marefu sana ila kwa ufupi nilimpa ushauri mmoja mzuri sana kama anataka kugombea ubunge... Unajua nilimshauri nini jamaa yangu yule? Nilimpa ushauri mmoja tu katika juhudi zake za kugombea chochote alichotaka kugombea. Maongezi yetu yalikwenda kama hivi:
  MIMI: Kutokana na uzoefu niliokuwa nao, na nionavyo wenzio waliofanikiwa walivyokuwa wakifanya, bwana mzee, shikilia suala moja tu, ambalo formula yake ni D + S = NO; but S + D = YES.

  YEYE:
  Bwana eh, mimi sijui hesabu, lakini hesabu zangu za shule ya msingi zinaonyesha hiyo haiwezekani.

  MIMI:
  Inawezekana. Wewe ni Mkristo. Kwani Askofu akikuambia 1 + 1 + 1 = 1, kwenye utatu mtakatifu, utambishia?

  YEYE:
  (Kicheko).

  MIMI:
  Kwani huu ni mwaka gani?

  YEYE:
  Elfumbili na kumi.

  MIMI:
  Mwaka wa elfu mbili na kumi tangu lini?

  YEYE:
  (Anafikiria kidogo) Tangu kuzaliwa Yesu Kristo.

  MIMI:
  Saddakta! Kwa hiyo siku aliyozaliwa Yesu Kristo ilikuwa tarehe moja, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza.

  YEYE:
  Eh, ndio... hapana.

  MIMI:
  Ala, kwani Yesu alizaliwa lini ati?

  YEYE:
  Tarehe 25, mwezi wa kumi na mbili.

  MIMI:
  Kwa hiyo hesabu zako za shule ya msingi, kama unavyoziita, zinakubali kwamba mwaka huanza tarehe 25 mwezi wa kumi na mbili, eti eh !!!?

  YEYE:
  Hapana.

  MIMI:
  Lakini unasherehekea Krismas au husherehekei?

  YEYE:
  Nasherehekea.

  MIMI:
  Kwa hiyo unakubali kwamba hesabu isiyowezekana saa nyingine inakubalika hivyo hivyo tu?

  YEYE:
  (Kicheko) Wewe bwana!!!
  MIMI: Tufanye umenielewa. Sasa na hii hesabu yangu imeshawezekana, kwa taarifa yako. Sasa, tufanye D = Dini na S = Siasa.. Kwa hiyo ushauri wangu mkubwa ninaokupa, ili ufanikiwe ni huu. USICHANGANYE DINI NA SIASA (D + S = NO). CHANGANYA SIASA NA DINI TU (S + D = YES).

  YEYE:
  Duh! Hii kali. Enhe, ndio inakuwa vipi.

  MIMI:
  Hewallaaa! Usije ukachanganya dini na siasa, hutafika mbali. Lakini changanya siasa na dini. Kwanza kabisa hakikisha kwenye kampeni zako unakuwa karibu na viongozi wa dini. Kwa mfano hapa Dar umpate Rwakatare mmoja au mchungaji yoyote wa Upako, maana hao wana lundo la watu. Sasa uzuri wa askofu au nabii wa upako, ana uwezo wa kuwaambia wafuasi wake wafanye lolote, na wakafanya, hata kama ni kwenda mbinguni kwa kuungua moto, kama alivyofanya yule wa kurudisha Amri Kumi za Mungu kule Uganda. Bwana Kibwetere. Kwa hiyo ukiwapata hawa mabwana, una kura jalo., Halafu uwakamate mashehe. Uzuri wa Mashehe, wanazo aya na hadithi za kila jambo katika ulimwengu huu. Na ukitaka kumpata Mwislamu Wewe mgonge aya tu, au hadithi. Sasa mashehe ni mafundi sana wa aya na hadithi. Pata mtu kama Yahaya wako mmoja, mambo saafi.

  YEYE:
  Aisee. Kote nilikopita, sijapata ushauri bomba kama huu. Hebu endelea. Kata nyanga, kata nyanga!

  MIMI:
  Sasa, sio kukata nyanga tu, kuna tatizo, patna! Jinsi ya kuwapata. Rwakatare ndio vigumu zaidi kumpata, kwa sababu ana mapesa. Huwezi kumnunua mtu kama huyo. Lakini ukitumia saikolojia unaweza kumpata. Ni kuingia tu kwenye madhehebu yake halafu umuombe akubariki, na akuombee kuwa mbunge. Kwa hiyo pale Kanisani, kama kuna watu wa jimbo lako, watakuona ukiombewa, kwa hiyo siku ya kura watajua huyu ndiye yule jamaa aliyeshikwa kichwa akaombewa awe mbunge. Hapo hujakwaa kura?

  YEYE:
  Aaaah, umezikwaa, mwanangu! (Anagongesha).

  MIMI:
  Ama kuhusu mashehe, wako wa aina mbili. Kuna wale wa

  YEYE:
  Siasa Kali?

  MIMI:
  Enhe, ndio wanavyoitwa. Hao bwana hawasikii la mchota maji wala mnadi swala. Usijihangaishe. Watakutoa mkuku uache viatu. Katika njia ya hao usiende, bali shika njia kuwaendea kondoo waliopote... waliopoteaaah, samahani, kuwaendea wengine.

  YEYE:
  Sasa mshirika Si noma hiyo?

  MIMI:
  Hapana, usikonde. Wapo wengine wa siasa poa wakina mufti. Hao hawana noma, ni rahisi sana kuwapata. Andaa futari tu halafu uwaalike.

  YEYE:
  Ah, kwani uchaguzi utakuwa mwezi wa Ramadhani? Halafu, uji rahisi, sasa mihogo na viazi noma, huu sio msimu wake. Pilau kwani vipi?

  MIMI:
  Kwani ukiwaambia kuna futari watauliza huu ni mwezi gani? Watakusahihisha tu, kwamba hatusemi futari yakhe, twasema swadaqa.

  YEYE:
  Yap! Kwa hiyo hapo atapata aya ya kunipigia debe.

  MIMI:
  Hakosi, hata kama haimo kwenye Korani, si atakung'uta Kiarabu tu. Gongo pia anaweza kulipatia aya, akasema: "Lau kaana haraam laakin da'wa".

  YEYE:
  (kicheko).

  MIMI:
  Huo ni wakati wa kutafuta kura. Ukishapata, utaapa kwa Biblia au QurÂ’an, kule bungeni. Unaona hapo D + S inapokuwa YES. Ukihudhuria Bungeni, Spika anafungua kwa maombi, anaombwa Mungu. Halafu wakati unashughulikia siasa, Ukiboronga, acha watu wengine waseme. Akiropoka shehe au askofu, mwambie: "Wewe unachanganya hiyo. Mungu hapendi namna hiyo." Wewe utakuwa unakataza wao wasimchanganye Mungu kwenye siasa lakini wewe umemchanganya wakati wa kukataza. Kama alivyofanya Mzee wangu Makamba. Anafundisha dini kwenye viriba vya siasa. Utamsikia: "Mtume hakufundisha kuchanganya dini na siasa msikitini", ila yeye ukimuuliza, kafundisha kuchanganya jukwaani? Sijui atasemaje. Kamtaja Mtume kwenye jukwaa la siasa. Kwao kutaja Mungu, Mtume, Yesu, n.k., kwenye jukwaa, ruksa. Using'ae macho, mimi nakupa ushauri, we vipi... Takrima unayo lakini?

  YEYE:
  Nakupata, mgosi. Nakupata. Takrima hipo usijali... Kwa hiyo mgosi Makamba kache....

  MIMI:
  Mmm usiseme hilo unalotaka kusema. Nakufundisha miundo mbinu. Si unataka kuwa mgombea? Kwa hiyo usitoke nje ya maongezi yetu, wala usitamke sentensi ambazo sijazitoa. Au umeanza kufeli hapa hapa, unachanganya kabla hujaanza?

  YEYE:
  Haya endelea.

  MIMI:
  Hayo ndio maneno! Hali ya kisiasa ikiwa mbaya, au hali ya uendeshaji nchi ikiwa mbaya, usiruhusu maaskofu na mashehe kusema, watachanganya. Ila hali ya hewa ikiwa mbaya, na njaa ikizidi, na uchumi ukiwa mgumu, unaenda kwa mashehe na maaskofu, unawaambia, jamani ombeni sana, salini jama tuondoke kwenye janga hili. Salini mvua inyeshe. Ombeni amani na utulivu. Hapo unachanganya siasa na dini. Na ndivyo tunavyokwenda.

  YEYE:
  Nimekupata, ni kweli D+S = No; S + D = Yes, naenda zangu.
   
 2. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ....Aaah mkuu mbona easy tu hapo, ni kuwapa tu ahadi tamu na kufanya nao MoU ya kuujenga na kuuimalisha uislamu na waislamu na sharia ya dini yao, ukipata madaraka imekula kwao..
   
 3. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  inavutia sana japo ni ndefu, na ina logic nimeipenda mkuu "senks tena"
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  I like this. Very Creative and the message is very clear. Thank you.
   
 5. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  You're so creative with divergent thinking,big up the message has well sent and clearly delivered
   
Loading...