TV Imaan Hewani, Hongera

Status
Not open for further replies.
Kama umeisoma Qur'an inakwambia:

Qur'an 21: 7. Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui

Qur'an 16: 43. Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui

Sasa kijana, unaweza kusoma na usielewe, ni wapi pa kuuliza?

Njia mojawapo rahisi ni hiyo ya kutazama Waislam na kuwaona na kuwasikia na kuwauliza. Ilmu ya Qur'an ni bahri kubwa sana isiyo na mwisho na wala hutamkuta Alim yeyote akakwambia kuwa mimi nimemaliza kila kilichomo kwenye Qur'an kuna specialty zake humo na kuna watu wanabobea kaka hayo.

Nakupa ushauri tu, ikiwa unataka kujuwa Uislam jifunze zaidi kutoka kwa Waislam.

Nakutakia utazamaji mwema.

Si ni Quran hii hii ambayo inadai kuwa rahisi kueleweka?

Sasa kama ni hivyo,yanini tena kutafuta watu wanieleweshe kitu ambacho ni rahisi kueleweka?
 
dvj alieko studio naomba unipigie kaswida ya 'utakwenda peke ako kaburini ukakae, uende ukalale chini adhabu ikufaaaeeee' tafadhari sana
 
Waislam kama wakristu wana haki sawa kufanya mambo Yao hasa yanayohusu imani Yao, so sio vizuri kuwabeza, ingawa Kuna hitilafu Kati ya hizi dini mbili, cha msingi kama alivyosema Faiza, chokochoko mara nyingi huanzishwa na watu wasiojua nini maana ya dini na amani, na Mimi naamini hivyo kwani nimeishi na waislam, na Nina marafiki waislam wengi Tu, na hizi chokochoko huwa naziona huku kwenye mitandao ya kijamii Tu, mtaani shwari kama kanisa la kkkt changanyikeni na msikiti WA changanyikeni vinavyoishi kwa amani.
...so hongereni Sana, na hubirini amani
 
Sio kweli
Kuujua Uislam hatuna haja ya kutazama television station yoyote ile bali tunaisoma Quran pamoja na hadith na Sira baasi

Waislam wanaweza kuupotosha Uislam lakini hivyo nilivyovitaja hapo haviwezi kamwe kuupotosha

Labda kama unazungumzia kuwajua Waislam hapo ndipo tutalazimika kuwaangalia Waislam ambao ni pamoja na hicho kituo cha television!

Takbiiiiiiiiiirrrrrrrr! Mshushie da'awa huyo mfataani FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Allahadulah!! Hawatafurahi Kwa Mafanikio Yenu Daima!! Kikubwa Ni Kupanga Na Kutekeleza Yetu Tu! Maneno Yenu Ya Shombo, Ndio Yaletayo Machafuko!! Chungeni Kauli Zenu!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom