TV Imaan Hewani, Hongera

Status
Not open for further replies.
Mi napata habari sahihi za kiislam toka kwa Boko haram na al shaabab. Hao wengine sijui tv imani ni waislam jina tu hao. Waislam wa kweli wa kuwasikiliza wapo Yemen, Pakistan na afghanistan
 
Hongera kwa lipi? Kitu gani cha maana walichofanya mpaka wapewe hongera au ndiyo yaleyale ya Radio Imaan tutaanza kuyashuhudia Live kwenye TV yao.

TCRA ifanye monitoring ya kutosha isije ikawa kama yaleyale ya Radio yao waliyoifungia kwa kueneza chuki.

Watanzania hatutaki kufika huko.

Watu wanaogopa kweli uislam, punguza woga kaka tenga muda juu ya uislamu utiona nuru iliyowazi
 
hongera kwa lipi? Kitu gani cha maana walichofanya mpaka wapewe hongera au ndiyo yaleyale ya radio imaan tutaanza kuyashuhudia live kwenye tv yao.

Tcra ifanye monitoring ya kutosha isije ikawa kama yaleyale ya radio yao waliyoifungia kwa kueneza chuki.

Watanzania hatutaki kufika huko.

ukiulizwa utaje chuki gani wali eneza huna...hizi ni porojo tu radio iman ni moja katika radio makini sana hapa tz. Na hakuna mfano wake kwa uchambuzi,
tatizo la wabongo hawapendi kukosolewa au kuona fikra mpya au kuona nyerere akikosolewa hili ndio tatizo.
Na bila ya kukusoa hatuwezi kujua wapi tumejikwaa.
Imaan tv nayo itakua moja ya tv bora afrika mashariki na naiweka katika meza moja na k24 , ntv au citizen..hizi ndio chanels za kuangalia na vipindi makini naamini iman tv itafika huko ingawa wafitini wapo lakini tusonge mbele
 
Nimeiangalia tv imaan jumapili nzima huyu ni mkombozi wetu.hima hima watu wema tizameni tv imaan mpate manufaa.nimependa vipindi vyake.najuwa itapigwa vita sana na makafiri.lakini naamin kwa kuwa mungu yupo upande wa watenda mema tutashinda.amiin
 
Nawaomba Waislam na wasio Waislam waingie na kujifunza mengi kuhusu maisha na fikra za Kiislam, wengi huwa wanapata habari za Waislam kutoka katika vyanzo ambavyo si vya Kiislam na huwa wanapotoshwa sana, sasa kitumieni chombo hicho kupata habari na kuujuwa Uislam kutoka kwa Waislam wenyewe.

Wa bi Llahi Tawfiq.
Sio kweli
Kuujua Uislam hatuna haja ya kutazama television station yoyote ile bali tunaisoma Quran pamoja na hadith na Sira baasi

Waislam wanaweza kuupotosha Uislam lakini hivyo nilivyovitaja hapo haviwezi kamwe kuupotosha

Labda kama unazungumzia kuwajua Waislam hapo ndipo tutalazimika kuwaangalia Waislam ambao ni pamoja na hicho kituo cha television!
 
Kwanini Emanuel TV iliondolewa kwa nguvu Startimes baada ya matangazo kibao TBC yaliyovutia wengi kununua king'amuzi hiki?
 
Sio kweli
Kuujua Uislam hatuna haja ya kutazama television station yoyote ile bali tunaisoma Quran pamoja na hadith na Sira baasi

Waislam wanaweza kuupotosha Uislam lakini hivyo nilivyovitaja hapo haviwezi kamwe kuupotosha

Labda kama unazungumzia kuwajua Waislam hapo ndipo tutalazimika kuwaangalia Waislam ambao ni pamoja na hicho kituo cha television!

Kama umeisoma Qur'an inakwambia:

Qur'an 21: 7. Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui

Qur'an 16: 43. Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui

Sasa kijana, unaweza kusoma na usielewe, ni wapi pa kuuliza?

Njia mojawapo rahisi ni hiyo ya kutazama Waislam na kuwaona na kuwasikia na kuwauliza. Ilmu ya Qur'an ni bahri kubwa sana isiyo na mwisho na wala hutamkuta Alim yeyote akakwambia kuwa mimi nimemaliza kila kilichomo kwenye Qur'an kuna specialty zake humo na kuna watu wanabobea kaka hayo.

Nakupa ushauri tu, ikiwa unataka kujuwa Uislam jifunze zaidi kutoka kwa Waislam.

Nakutakia utazamaji mwema.
 
Mi napata habari sahihi za kiislam toka kwa Boko haram na al shaabab. Hao wengine sijui tv imani ni waislam jina tu hao. Waislam wa kweli wa kuwasikiliza wapo Yemen, Pakistan na afghanistan

Teh teh teh teh teh! Kumbe wakti mwingine CHUKI/UKAFIRI humfanya mtu akawa mbumbumbu kiasi hiki eeh!!!!???
Pole yako.
 
"Hii ni taarifa ya habari toka Tivii iman, ...Naijeria;... imegundulika kuwa kikundi chote cha boko haramu ni wakatoliki, habari zinasema....":):smile-big:
 
...cc : ﺣﺮﻛﺔ ﺍﻟﺸﺒﺎﺏ ﺍﻟﻤﺠﺎﻫﺪﻳﻦ ; Ḥ

translated by google as

... cc: Young Mujahideen Movement
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom