Tuzungumze na bodi ya mikopo kuwanusuru Watanzania

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
HELLOW BODI YA MIKOPO, HAMUWEZI KWENDA NA HII?

Na Elius Ndabila
0768239284

Hivi karibuni kumekuwa na mjadala mzito juu ya hoja ya mnufaika wa Fedha ya bodi ya mkopo kutakiwa kuanza kuirejesha mara baada ya miezi 24 tangu kuhitimu.

Hoja hii imezua mjadala mzito kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wanatafsiri kama sheria hii inakuja kumkandamiza zaidi masikini aliyeshindwa kujisomesha na kuamua kukopa. Wanaokopa wengi bodi ya mikopo ni maskini au wanatoka kwenye familia maskini. Hawa wanategemea baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali wataajiriwa na kuanza kurejesha mkopo wao. Lakini wakiwa wanajaribu kupambana wanakitana na rungu la Bodi ya mikopo linalowataka kurejesha baada ya miezi 24 na kushindwa kufanya hivyo basi mnufaika huo atakutana na rungu la penalti.

Hii si hoja nyepesi, ni hoja nzito ambayo usuli wake ni zaidi ya ongezeko lile la 8% na kupelekea rejesho la 15% kwa watumishi.

Pamoja na kwamba sikubaliani na hoja kandamizi hizi kutoka bodi ya mikopo, lakini ninashauri Wabunge ambao ndio wawakilishi pekee wanaoweza kutunishiana misuli na Bodi ya mikopo ninatamani waje na mapendekezo haya ili kuokoa watanzania wengi maskini ambao hawataweza kulipa fedha hizi.

Kutokana na idadi kubwa ya vijana wanaoenda vyuo vikuu na ambao huwa wanakopa fedha toka bodi ya mikopo, na kwa kuwa vijana hawa wanakopa fedha wakiamini kuwa watakapo pata kazi ndipo wataanza kulipa, lakini kwa kuwa mahitaji ya ajira ni machache ukilinganisha na Idadi ya wanufaika ambao wanahaswa mitaani Basi Bunge litoe mapendekezo kuwa walau kila Mwanafunzi akihitimu chuo kikuu akopeshwe fedha 50% ya mkopo wake wa miaka aliyosoma shule ili akifika mtaani akafungue biashara itakayosaidia kupata fedha ya marejesho. Ukweli ni kuwa mtu akitoka chuo kikuu anapoteza miaka mitatu, hivyo anaporudi mtaani anakuwa hana cha kufanya na kushindwa kulipa hizo fedha. Lakini bodi ikiwakopesha wanapirudi mtaani na kupewa vitambulisho rasmi ninaamini watarejesha kwa uaminifu.

Hoja nyingine Wabunge washauri elimu yetu ibadilishwe. Elimu yetu toka shule ya msingi inamuandaa mtu kuajiliwa, haimuandai kujiajiri ndio maana tuna wimbi kubwa la Wahitimu wanatembea na bahasha kwa kuwa walichosoma hakipo mtaani. Mwanafunzi anasoma mambo ya akina Plato, Aristotle, Marekani n.k hasomi elimu inayomuandaa kupambana na mazingira halisi ya Tanzania na fursa zilizopo.

Mwisho, Mh Rais hivi karibuni alikaririwa akimuomba kiongozi wa China kuifuta Tanzania madeni, na sisi Wazalendo tunatamani China wasikie ombi la Mh Rais wetu. Lakini ktk hili nimuombe pia Mh Rais ikimpendeze awaagize bodi ya mikopo kuachana na utaratibu huu ambapo utaenda kuwaumiza Watanzania wanyonge.
 
Msitusumbue ! Sisi tuko vizuri wapinzani ndio walituchelewesha ,mitano zaidi akikataa tumlazimishe
 
Back
Top Bottom