Tuzungumze familia: Kwanini unatamani/ulitamani kuwa na mtoto?

Bdo cjaona sababu ya msingi kwann nahtaj mtot kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu ngoja nikuambie ukweli.

Kimsingi, hakuna mtu mwenye sababu ya maana ya kuwa na mtoto. Kwetu sisi waafrika, kuwa na mtoto ni kitu "automatik" ambacho mtu akishafikisha miaka fulani anaona anatakiwa kuwa nacho. Yaani sisi hatuna tofauti sana na wanyama wa porini ambao akishafikisha umri wa kuzaa basi wanaanza kuzaana.
Baadhi ya sababu zinazotolewa na wadau hazina tija yoyote, mfano:
1. Kuijaza dunia: Hapa tulipo sasa hivi dunia ina watu karibu 9 bilioni. Nafikiri tumeshavuka kiwango cha idadi ya watu ambao dunia inaweza kubeba, ila bado watu watakuambia imani inasema tuzaane tujaze dunia. Dunia imeshajaa!!
2. Kupata mrithi: Kwanza jiulize ni mali zipi hizo ulizo nazo kiasi kwamba unadhani unahitaji mtu wa kuzirithi? Na hata kama unazo, je ni lazima umrithishe mtoto wako? Hakuna mtu mwingine anaeweza kuzirithi? Una uhakika gani kwamba mtoto wako atakuja kuwa na akili ya kuziendesha? Kwani hizo mali ukiwaachia ndugu/jamaa/marafiki au watoto yatima utapata hasara gani wakati wewe umekufa?
3. Kuendeleza jina: Wewe ukifa, weather jina lako litaendelea ama la, haikusaidii chochote. Wewe utakumbukwa kwa mambo uliyoyafanya, sio kwa watoto ulioacha! Nelson Mandela wote tunamkumbuka, ila hakuna anaejua watoto wake wanaitwaje wala wako wapi.
4: Kuacha "copy" yako: Ili iweje? Wewe una nini cha ajabu ambacho unafikiri unahitaji kukiacha hapa duniani? Una uzuri, akili, au nini ambacho unadhani kikikosekana dunia itapata hasara?
5. Kusaidiwa uzeeni: Huu nao ni ufinyu wa fikra na mawazo ya kizamani. Wewe tengeneza mazingira ambayo yatakufanya uishi vizuri uzeeni usije ukafikiri watoto ni uwekezaji kwa manufaa ya baadae. Unaweza kuwa nao na wasikusaidie kitu badala yake ukajikuta wewe ndio unawasaidia maisha yako yote.
 
Natamani kuwa na watoto sababu napenda sana,what a feeling ile kuona ni kiumbe cha Mungu kupitia wewe/mimi aisee, viniite Mama rahaa,afu I wish kuwa na watoto 5 , 3 baby boys and 2 beautiful girls.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na mtoto ni raha sana,hasa ukiwa na mazingira mazuri ya kiuchumi utafurahia sana,wana vituko balaa mana wanakuwaga wageni kwa kila jambo la hapa duniani kwa hiyo mda wote wewe ni kufundisha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wa nini? Sipendi watoto kwasababu sipendi kusikia wakilia huwa nawahurumia sana.

Labda baadae huko nita adopt akiwa mkubwa mkubwa may be three years old hivi.
 
Good/bad for you

Mostly ikiwa watoto wanashinda nyumbani who teach them au mashuleni which behavior are they gaining? Do you know the back ground of those people? Do you have proper time to spend with your children?
If not who is spending time with them?
Why are we arguing that our children behavior isn’t good!.
 
Mostly ikiwa watoto wanashinda nyumbani who teach them au mashuleni which behavior are they gaining? Do you know the back ground of those people? Do you have proper time to spend with your children?
If not who is spending time with them?
Why are we arguing that our children behavior isn’t good!.

Sina mtoto mkuu

Halafu who's arguing?ama unaongea na simu?
 
Back
Top Bottom