Tuweni makini na picha za wanawake kuna ujio wa app ya Photo Lab

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,850
Ndugu watoto wakiume, wavulana, vijana na wanaume wote bila kusahau wazee wetu wanaume

Nawasalimu nyote kwa Jina la Jamuhuri ya wana JF.

Na wote tuseme JF idumu milele.

Ndugu zangu ujio wa app ya photo lab upo mjini na wale wazee wa kuview mapicha picha pamoja na kutumiwa picha tuweni makini sana tujitahidi kuonaa na watoto wa kike, mabinti pamoja na wanawake ana kwa ana (uso kwa uso) na siyo kutegemea kutumiwa picha ndugu zangu.

Teknolojia imekua na kila siku kuna ujio wa vitu vizuri vizuri ili kurahisisha maisha na kupendezesha dunia.

Ujio wa app ya photo lab umefanya picha za wanawake ziwe nzuri zaidi hivyo tujitahidi pia kukutana nao uso kwa uso kabla ya kuanza kuwekeza akili huko.

Naomba kuwasilisha.
 
... jamani anzisheni mada za kuchochea mawazo ya kulipelekea taifa mbele - changamoto za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kimaadili, ajira, n.k. Hizi akili za kila mara kuwaza katikati ya magoti na kitovu cha mwanamke, "Tigers of the East" tutaendelea kuimba kama kasuku tu.
 
Hata ukianzisha wasomaji,wachangiaji hadi impression haipandi sababu hawazitaki mkuu!.
 
... jamani anzisheni mada za kuchochea mawazo ya kulipelekea taifa mbele - changamoto za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kimaadili, ajira, n.k. Hizi akili za kila mara kuwaza katikati ya magoti na kitovu cha mwanamke, "Tigers of the East" tutaendelea kuimba kama kasuku tu.
Hata hili linasaidia kupeleka taifa mbele na kuepusha migogoro ya kiuchumi na kijamii isiyo ya lazima baina ya wanaume na wanawake hasa hasa pale ambapo utategemea ukutane na mwanamke au mwanaume fulani ukakuta vitu ni tofauti na umeshapoteza gharama nyingi .

Hivyo kwa mantiki hii Taifa letu litaendelea kuwa na amani na kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji ili kukuza uchumi wa Taifa na wa mtu binafsi mmoja mmoja kwa kila nafasi yake
 
Ndugu watoto wakiume, wavulana, vijana na wanaume wote bila kusahau wazee wetu wanaume

Nawasalimu nyote kwa Jina la Jamuhuri ya wana JF...
Du ndiyo unajua leo? Hivi wewe bado huwa unaamini mwanamke fulani uliyemuona kwenye picha ni mrembo bila kumwona ana kwa ana?

Hiyo app itafanya nini cha zaidi ambacho wanawake walikuwa hawakijui kwenye kupiga na ku edit picha?
 
Back
Top Bottom