Tuwe wavumilivu kwa masuala tunayoyapenda na hata kwa tusiyoyapenda pia

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,586
17,699
Katika ulimwengu huu na miaka hii ambapo patience intertwines with the passions, muda mwingi tunatamani kusikia yale tu tunayoyapenda kutoka kwa watu, na hata kuna yale tusiyoyatamami mtu ayasikie tunapoona yanasikika tunakosa uvumilivu, muda mwingi tunatamani kuyaondoa mawazo hayo lakini bad enough hatuna uwezo huo!

kibaya ni kwamba tunapokuwa na Uwezo wa kufanya hivyo tunajitahidi sana mambo hayo yasifike kwa jamii na tunatumia njia zote kudhibiti sio tu yasifike bali yatakayofika ni yale tu tunayotamani yawe huru kusikika na watu ili kuzidi kuwapumbuza.

Buddha kuna muda aliwahi kusema "Patience is key. Remember: An angry person is always ugly, whether on the inside or the outside."

Sio tu Buddha hata kwa Wakristo, Yesu pia aliwahi kutuonyesha Subira ndio kila kitu, Luka 21:19 "Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu".

Na hata katika Quran (2:153) M/Mungu anasema, "Innallah Maswabirina," hii inamaanisha kwamba hakuna sehemu ambapo hatufundishi Subira, Uvumilivu hata kwa vile tusivyovipenda. Sasa tatizo uanza wapi?

Tatizo huanza pale tunapojiona tuna haki kuliko, wengine, tunauchungu kuliko wengine na hata tumeshika ukweli kuliko wengine huku hatutaki kusikia upande wenye ukweli kwa sababu unatutia machungu.

Ukiona huna uvumilivu kuusikia ukweli au ukiona huna uvumilivu kusikia upande ambao upo kinyume na wewe, elewa kwamba hauna tofauti na Gaidi. Sema tu umekosa vifaa vya kutimiza ahadi yako!

Tafuteni iliyo kweli nayo itawaweka huru!

Asante, huu ndio ujumbe wangu kwa siku ya leo.
 
Katika ulimwengu huu na Miaka hii ambapo patience intertwines with the passions, Muda Mwingi tunatamani kusikia Yale tu tunayoyapenda kutoka kwa watu, na hata kuna yale tusiyoyatamami mtu ayasikie tunapoona yanasikika tunakosa uvumilivu na Muda mwingi tunatamani kuyaondoa Mawazo hayo lakini Bad enough hatuna uwezo huo....

kibaya ni kwamba tunapokuwa na Uwezo wa kufanya hivyo..

Tunajitahidi sana Mambo hayo yasifike kwa Jamii na tunatumia Njia zote kudhibiti sio tu yasifike bali yatakayofika ni yale tu tunayotamani yawe huru kusikika na watu ili kuzidi kuwapumbuza...

Buddha kuna muda aliwahi kusema "Patience is key. Remember: An angry person is always ugly, whether on the inside or the outside."

Sio tu Budha hata kwa wakristo Yesu pia aliwahi kutuonyesha Subira Ndo kila kitu Luka 21:19 "Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu"

na hata katika Quran (2:153) M/Mungu anasema...."Innallah Maswabirina"...
hii inamaanisha kwamba hakuna Sehemu ambapo hatufundishi Subira,Uvumilivu hata kwa vile tusivyovipenda..

Sasa Tatizo uanza wapi..

Tatizo huanza pale tunapojiona Tuna Haki kuliko Wengine..Tunauchungu kuliko wengine..
Na hata Tumeshika Ukweli kuliko wengine huku hatutaku kusikia Upande wenye Ukweli kwa sababu unatutia Machungu..

Ukiona Huna Uvumilivu Kuusikia Ukweli ,Au ukiona Huna uvumilivu Kusikia Upande ambao upo Kinyume na Wewe Elewa kwamba hauna Utofauti na Gaidi..Sema tu umekosa Vifaa vya kutimiza Hadi yako...

Tafuteni Iliyo kweli nayo itawaweka Huru...
Asante huu ndo ujumbe wangu kwa siku ya Leo
Ameeni!
 
Back
Top Bottom