Mmoja wa washauri wakuu wa Ngosha ni rafiki yangu wa karibu. Zipo njia za kisomi za kumshauri na akapokea ushauri.
Mwaka juzi alitaka kwenda kupumzika chato wakati uwanja bado haujakamilika. Jamaa yangu akamkatalia, waziri na naibu wakamtumia ujumbe jamaa lakini bado akakataa kwa kigezo kuwa ndege ya raia namba moja haiwezi kutua katika uwanja mbovu.
Bwana mkubwa akasafiri na gari mpaka huko kwake alikozaliwa. Baada ya siku chache Kiongozi mkuu akampigia simu jamaa na kumwambia ni kweli uwanja bado haujamalizika.
Ni baada ya uwanja kumalizika ndipo ndege imetua huko kwake.
Wasomi wengi wa kitanzania wanashindwa kujenga hoja za kina na zenye mantiki, ingawa mkuu kabisa analo tatizo la ubishi usio na sababu.