Tuwe wakweli, huyu anaweza kumshauri Rais?

Chakaza

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
41,026
Reaction score
74,704
Tunaamini watendaji wakuu wa serikali yaani Mawaziri, Makatibu wakuu, maRC, DC na wateuliwa wote wa kisiasa na kitendaji ndio chanzo cha mafanikio au maanguko ya Rais na serikali yake.

Mtu anateuliwa kushika nafasi ikiaminika ni mkweli, jasiri na hana woga wala unafiki na atamshauri vyema Rais kwa manufaa ya nchi.

Hii hali aliyo nayo RC wa Dodoma mbele ya Rais je anaweza kuwa reliable kumshauri Rais jambo zito?
Anaweza kumfahamisha jambo ambalo anajuwa lazima Rais atachukizwa nalo lakini ndio ukweli?

Sasa hali inaonyesha wateule wengi sana (eg Kabudi, Jafo, Makonda etc) ndivyo walivyo na mikwamo mingi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na hulka hii.

Ndio hulka zetu na haya mambo asili yake ni tangu enzi za uchifu kabla wakoloni hawajaja Afrika.

Kila mtu anaogopa kupoteza mkate wake kiasi cha kuwa tayari kunyenyekea hata kama kiuhalisia anajishusha sana.

Lakini ukijivua uoga na ukaongozwa na mantiki zenye kueleweka huyu huyu pichani ni muelewa sana. Unapokuwa nae kikazi usipaniki hata kidogo.
 
Phillipo, kila mmoja anamjua kiongozi wake yukoje kuliko hata sisi nje. Ukiona huyo yuko hivyo ni mawili.
Bosi wake huyo hana simile anaweza kukutapikisha kazi kufumba na kufumbua au yeye ana makosa mengi kiasi cha kumuogopa kuwa jee kamjua?
Eitha kwa yote mawili, jee anaweza kukaa meza moja naye na kumshauri mkuu wake anapoona mambo hayaendi vizuri?
Ndio msingi wa hoja hii mkuu!
 
Tupe mfano wa Kiongozi unaye dhani anaweza kuwa na ujasiri wa kimshauri Rais bila kupepesa macho.
 
Phillipo, kila mmoja anamjua kiongozi wake yukoje kuliko hata sisi nje. Ukiona huyo yuko hivyo ni mawili.
Bosi wake huyo hana simile anaweza kukutapikisha kazi kufumba na kufumbua au yeye ana makosa mengi kiasi cha kumuogopa kuwa jee kamjua?
Eitha kwa yote mawili, jee anaweza kukaa meza moja naye na kumshauri mkuu wake anapoona mambo hayaendi vizuri?
Ndio msingi wa hoja hii mkuu!
Mmoja wa washauri wakuu wa Ngosha ni rafiki yangu wa karibu. Zipo njia za kisomi za kumshauri na akapokea ushauri.

Mwaka juzi alitaka kwenda kupumzika chato wakati uwanja bado haujakamilika. Jamaa yangu akamkatalia, waziri na naibu wakamtumia ujumbe jamaa lakini bado akakataa kwa kigezo kuwa ndege ya raia namba moja haiwezi kutua katika uwanja mbovu.

Bwana mkubwa akasafiri na gari mpaka huko kwake alikozaliwa. Baada ya siku chache Kiongozi mkuu akampigia simu jamaa na kumwambia ni kweli uwanja bado haujamalizika.

Ni baada ya uwanja kumalizika ndipo ndege imetua huko kwake.

Wasomi wengi wa kitanzania wanashindwa kujenga hoja za kina na zenye mantiki, ingawa mkuu kabisa analo tatizo la ubishi usio na sababu.
 
Kutua ndege kwenye uwanja mbovu ni kuelekea kupata ajali na hatimaye kifo. Nani anaweza kushauriwa na akagoma? Au akashauriwa na akamfukuza kazi aliyemshauri?

Mkuu hapo bado hujanishawishi.

Nataka anayeweza kumwambia huu mradi wa kujenga hospitali hapa hauna tija ni bora tuanze na mradi wa maji kwani vifo vingi eneo hili vinasababishwa na magonjwa ya matumbo na maji machafu.

Jee aina hiyo ya RC wa Dodoma anaweza kuisimamia hoja yake na kusisitiza ushauri wake?
 
kakatwa jicho hadi akili ikapotea. Yanaweza kuwa madhara ya viboko shuleni, vinakufanya uogope wenye mamlaka.
 
Kutua ndege kwenye uwanja mbovu ni kuelekea kupata ajali na hatimaye kifo. Nani anaweza kushauriwa na akagoma? Au akashauriwa na akamfukuza kazi aliyemshauri?
Mkuu hapo bado hujanishawishi.
Nataka anayeweza kumwambia huu mradi wa kujenga hospitali hapa hauna tija ni bora tuanze na mradi wa maji kwani vifo vingi eneo hili vinasababishwa na magonjwa ya matumbo na maji machafu.
Jee aina hiyo ya RC wa Dodoma anaweza kuisimamia hoja yake na kusisitiza ushauri wake?
Huyo huyo wa Dodoma katika hiyo video alisifiwa kwa utendaji wake na Ngosha hadharani kwa kufanya kazi nzuri.

Kushauriwa anashauriwa na anashaurika.Suala kama kushughikia mishahara hewa sio uamuzi wake mwenyewe ni matokeo ya ushauri.

Yapo mengi tu anayoshauriwa na kina Mahiga na Kabudi na yanatekelezwa.
 
Alishauriwa kuna wahuni wengi hawana vyeti akawabutua ndio ndio kutwa mnabwabwaja humu

Ni ushauri gani hataki?
 
Kutua ndege kwenye uwanja mbovu ni kuelekea kupata ajali na hatimaye kifo. Nani anaweza kushauriwa na akagoma? Au akashauriwa na akamfukuza kazi aliyemshauri?
Mkuu hapo bado hujanishawishi.
Nataka anayeweza kumwambia huu mradi wa kujenga hospitali hapa hauna tija ni bora tuanze na mradi wa maji kwani vifo vingi eneo hili vinasababishwa na magonjwa ya matumbo na maji machafu.
Jee aina hiyo ya RC wa Dodoma anaweza kuisimamia hoja yake na kusisitiza ushauri wake?
Ni kweli aisee.
Hiyo ya kutua kwenye uwanja fulani sijui mbovu hiyo ni kitu minor Sana ambacho mtu yeyote anaweza kumueleza,hakina uzito kwenye maendeleo ya nchi.
 
27 November 2019
Bora huyu wa Igunga anamweleza hali halisi ya matatizo ya watu na watu wanashangilia sana Mh. Rais kuambiwa hakuna hela mifukoni na aachie hela, sasa sikiliza majibu ya Mh. Rais anasema fanyeni kazi ni kama vile watu hawafanyi kazi kumbe kuna matatizo ya masoko, malipo n.k kwa kazi walizofanya wananchi
 
Tunaamini watendaji wakuu wa serikali yaani Mawaziri, Makatibu wakuu, maRC, DC na wateuliwa wote wa kisiasa na kitendaji ndio chanzo cha mafanikio au maanguko ya Rais na serikali yake.

Mtu anateuliwa kushika nafasi ikiaminika ni mkweli, jasiri na hana woga wala unafiki na atamshauri vyema Rais kwa manufaa ya nchi.

Hii hali aliyo nayo RC wa Dodoma mbele ya Rais je anaweza kuwa reliable kumshauri Rais jambo zito?
Anaweza kumfahamisha jambo ambalo anajuwa lazima Rais atachukizwa nalo lakini ndio ukweli?
Sasa hali inaonyesha wateule wengi sana (eg Kabudi, Jafo, Makonda etc) ndivyo walivyo na mikwamo mingi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na hulka hii
View attachment 1274048

Imenikumbusha nyimbo moja ya dini nadhani iliimbwana na Mwanza Town Choir miaka hiyo nyimbo inasema "Heka heka hekaheka za wokovu..."
 
Back
Top Bottom