Tuwe wakweli, huyu anaweza kumshauri Rais?

Tuwe wakweli, huyu anaweza kumshauri Rais?

Huyo huyo wa Dodoma katika hiyo video alisifiwa kwa utendaji wake na Ngosha hadharani kwa kufanya kazi nzuri.

Kushauriwa anashauriwa na anashaurika.Suala kama kushughikia mishahara hewa sio uamuzi wake mwenyewe ni matokeo ya ushauri.

Yapo mengi tu anayoshauriwa na kina Mahiga na Kabudi na yanatekelezwa.
Haya bwana, hii ligi umeshinda!
 
Mmoja wa washauri wakuu wa Ngosha ni rafiki yangu wa karibu. Zipo njia za kisomi za kumshauri na akapokea ushauri.

Mwaka juzi alitaka kwenda kupumzika chato wakati uwanja bado haujakamilika. Jamaa yangu akamkatalia, waziri na naibu wakamtumia ujumbe jamaa lakini bado akakataa kwa kigezo kuwa ndege ya raia namba moja haiwezi kutua katika uwanja mbovu.

Bwana mkubwa akasafiri na gari mpaka huko kwake alikozaliwa. Baada ya siku chache Kiongozi mkuu akampigia simu jamaa na kumwambia ni kweli uwanja bado haujamalizika.

Ni baada ya uwanja kumalizika ndipo ndege imetua huko kwake.

Wasomi wengi wa kitanzania wanashindwa kujenga hoja za kina na zenye mantiki, ingawa mkuu kabisa analo tatizo la ubishi usio na sababu.
Huyo jamaa yako ndio alikuambia uje utusimulie hapa?. Bro, huna maadili.
 
Lakini uyo mzee hapo alikua anainuka sema hako kapicha kamemchoresha sana [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mmoja wa washauri wakuu wa Ngosha ni rafiki yangu wa karibu. Zipo njia za kisomi za kumshauri na akapokea ushauri.

Mwaka juzi alitaka kwenda kupumzika chato wakati uwanja bado haujakamilika. Jamaa yangu akamkatalia, waziri na naibu wakamtumia ujumbe jamaa lakini bado akakataa kwa kigezo kuwa ndege ya raia namba moja haiwezi kutua katika uwanja mbovu.

Bwana mkubwa akasafiri na gari mpaka huko kwake alikozaliwa. Baada ya siku chache Kiongozi mkuu akampigia simu jamaa na kumwambia ni kweli uwanja bado haujamalizika.

Ni baada ya uwanja kumalizika ndipo ndege imetua huko kwake.

Wasomi wengi wa kitanzania wanashindwa kujenga hoja za kina na zenye mantiki, ingawa mkuu kabisa analo tatizo la ubishi usio na sababu.
Ukiwa Ngosha Typical ama Mtu wa Mashinani kwenyewe kabisa pahala popote bongo hii (hapo huhitaji natural psychology kwani nacho ni kipaji) ni Rahisi sana kuishi kufanya kazi ama kumshauri namba moja....

Is an art...haihitaji cheo tofauti na hapo itakupasa tu sasa kuishi na kufanya kazi kwa kuvizia...mama wafanyavyo wateuliwa wake wengi. Rule # 01; Know someone's culture and style
 
Huyo jamaa yako ndio alikuambia uje utusimulie hapa?. Bro, huna maadili.
Inategemea na uelewa wako wa neno maadili.

Humu jukwaani kuna mengi mazito yanaandikwa kila siku na watu wazito. Lengo ni jema na nia ni kujenga hoja.
 
Huyo huyo wa Dodoma katika hiyo video alisifiwa kwa utendaji wake na Ngosha hadharani kwa kufanya kazi nzuri.

Kushauriwa anashauriwa na anashaurika.Suala kama kushughikia mishahara hewa sio uamuzi wake mwenyewe ni matokeo ya ushauri.

Yapo mengi tu anayoshauriwa na kina Mahiga na Kabudi na yanatekelezwa.
Timu ya mapambio na kusifia Jiwe katika ubora wake
 
Inategemea na uelewa wako wa neno maadili.

Humu jukwaani kuna mengi mazito yanaandikwa kila siku na watu wazito. Lengo ni jema na nia ni kujenga hoja.
Uelewa wangu uko vizuri tu. Mfano wako wa jamaa yako umefikisha point vizuri ikaeleweka. Ila upande wa pili wa shilingi kuna kitu kinaitwa “confidentiality”, hapo umefeli. Mshauri hakutakiwa akuambie kiurafiki ya huyo anayemshauri. Na wewe ukarikoroga zaidi kwa kumuaniaka jamaa yako hapa.
 
Jamaa yangu na mimi hakuna anayetujua ndio uzuri wa hili jukwaa.

Unakuta mtu humu jukwaani anaitwa njiwa au mwewe ila ukija kumuona kwa macho ni mheshimiwa fulani.

Lakini hoja yako imeeleweka 👍🙏.
 
Nimechek hiyo clip nimecheka kwa nguvu kidogo nijambe
Tunaamini watendaji wakuu wa serikali yaani Mawaziri, Makatibu wakuu, maRC, DC na wateuliwa wote wa kisiasa na kitendaji ndio chanzo cha mafanikio au maanguko ya Rais na serikali yake.

Mtu anateuliwa kushika nafasi ikiaminika ni mkweli, jasiri na hana woga wala unafiki na atamshauri vyema Rais kwa manufaa ya nchi.

Hii hali aliyo nayo RC wa Dodoma mbele ya Rais je anaweza kuwa reliable kumshauri Rais jambo zito?
Anaweza kumfahamisha jambo ambalo anajuwa lazima Rais atachukizwa nalo lakini ndio ukweli?
Sasa hali inaonyesha wateule wengi sana (eg Kabudi, Jafo, Makonda etc) ndivyo walivyo na mikwamo mingi inachangiwa kwa kiasi kikubwa na hulka hii
View attachment 1274048

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu wa kumsamehe ana waogopa wavamizi walio vamia maeneo yaliyo pangwa kisheria na hati kwa hoja nyepesi kuwa wataenda wapi kwani wametoka wapi
 
Ndio hulka zetu na haya mambo asili yake ni tangu enzi za uchifu kabla wakoloni hawajaja Afrika.

Kila mtu anaogopa kupoteza mkate wake kiasi cha kuwa tayari kunyenyekea hata kama kiuhalisia anajishusha sana.

Lakini ukijivua uoga na ukaongozwa na mantiki zenye kueleweka huyu huyu pichani ni muelewa sana. Unapokuwa nae kikazi usipaniki hata kidogo.

Hamna lolote, CAG alijiamini nini kilitokea? Kimsingi huyo jamaa hayo mamlaka ni makubwa kuliko busara zake zinapoishia.
 
27 November 2019
Bora huyu wa Igunga anamweleza hali halisi ya matatizo ya watu na watu wanashangilia sana Mh. Rais kuambiwa hakuna hela mifukoni na aachie hela, sasa sikiliza majibu ya Mh. Rais anasema fanyeni kazi ni kama vile watu hawafanyi kazi kumbe kuna matatizo ya masoko, malipo n.k kwa kazi walizofanya wananchi

Hayo majibu ya nyodo ni majibu ya watu wote wenye ajira na mishahara minono, huku wakipata huduma nyingine bure.
 
Back
Top Bottom