Tuwe wakweli; hivi CCM itakubali kuachia Igunga?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
523
Wadau, natamani sana CCM ishindwe uchaguzi Igunga, lkn akili yangu haikubali kabisa kuwa CCM, hata ikishindwa; itakuwa radhi kuachia Jimbo la Igunga kwa sababu zifuatazo;
1. Kushimdwa na kuachia Igunga ni ishara mbaya kwa CCM 2015!
2. Igunga lilikuwa ni mali ya CCM, na hawakutarajia kama RA angeachia ubunge
3. Uwezo wa wana Igunga kujitoa muhanga kama Arusha na Mwanza kulazimisha kura zitangazwe ni mdogo, hawana nguvu ya kulazimisha matakwa ya umma.
4.CCM hawako tayari kuaibishwa kwa shujaa wao Mkapa
 

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,752
Inawezekana hizo zikawa fact Ibrah....
Na kuna "ukweli" zaidi kuwa si matamanio ya CCM kuachia hata kipande cha tarafa moja...
Lakini kwenye swali la nini watu wanataka na nyakati husika kwa kushabihiana na mazingira...
CCM mara zote italazimishwa kukubali wasiyoyatarajia rejea uchaguzi uliopita wa 2010.. (Mbeya, Dar na Mwanza)
Kwenye orodha hapo mbele utakuta Igunga.....
Wananchi si mali ya mtu...pole zake "shujaa" wao Ben Mkapa (taswira ya ufisadi nchini)
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
12,627
11,311
CCM kumrudisha Rostam kufanya kampeni Igunga ni kuwatukana wananchi wa Huko na wao wanaelewa kuwa Rostam kafanya kampeni hizo kwa kulazimishwa na hivyo wataiangusha CCM! Ngoja mtaona wanaIgunga watakavyowashikisha adabu hawa jamaa.
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
5,375
Halafu hichi kitendo cha CCM kugawa unga wa mahindi ni ishara tosha kuwa hawajiamini kwa umaarufu wao miongoni mwa raia wa Igunga. Chama kingine chochote kingefanya hivyo wangesema kinahonga. Lakini in the final analysis tutegemee kuwa kura itakuwa huru na ya haki na kwamba watu watakuwa makini wakati kura zinahesabiwa. Ni kweli CCM haitapenda kupoteza jimbo hili kwa sababu wanaamini kwenye domino effect theory---kwamba kama wamepoteza hata katika eneo ambako walikuwa na uhakika nalo itakuweje katika maeneo mengineyo miaka ijayo?
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
523
CCM tunayoijua, itakuwa tayari kuiachia Igunga itue mikononi mwa wapinzani kweli? Igunga wana ubavu wa kusimamia kura zao kama MZ, AR na Mbeya? Kwa Jiograpfia ya Igunga tusishangae matokeo kuytangazwa baada ya wiki moja!
 

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,620
1,777
Vyama vya upinzani vina safari ndefu sana, kama havita acha ubinafsii na kujiona kuwa ni vyenyewe tu, bila ya kushirikiana kuwa vitaleta mabadiriko, basi wajuwe kabisa wanajidanganya sana.
 

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Kwa kweli siasa zenu bado sana ni siasa za matukio kama tunavyosikia na kuona huku Igunga.
Nikiangalia mchakato mzima wa uchaguzi Igunga na vyama vya siasa vilivyojigawa naona kabisa uchaguzi wa Igunga utazigawa kura za wapinzani na kuwapa nafasi CCM. sio kama watu wa Igunga wanawapenda sana CCM, wapinzani wenyewe ndio wanasababisha yote haya kutokea tutaona baada ya uchaguzi kura za wapinzani zitakuwa nyingi kuzidi kura za CCM
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom