Tuwe makini mwezi huu

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,905
Sio kwasababu tu ya yale yaliyokwisha tokea bali kwa yale yatakayotokea.

Kwa wale wanaofuatilia mtiririko wa mambo pamekuwa na ajali nyingi mwezi February mwaka huu na historia inaonesha pia February ya miaka fulani hali ilikuwa hivyo.

Hatuna tunachoweza kusema sana kwamba labda ni mvua au wasafiri wengi kama mwezi December lakini mtakubaliana nami kwamba ajali na vifo vinavyotokana na mauaji ni vingi zaidi mwezi huu.

Ulimwengu wetu una pande mbili; yale tuyaonayo na yale tusiyo yaona. Yote ni sehemu ya mfumo mmoja unaofanya kazi kwa lengo moja.

Si vizuri kuwa mshirikina ila pia ni vibaya kuukataa ukweli wa mambo. Tupo kwenye kile kilichsababisha mauaji yasiyo na maelezo ya maalbino. Haiingii kichwani lakini ni kweli watu waliwauwa ndugu zetu bila huruma, wakisukumwa na imani zao, na mwezi huu yanatokea yanayofanana na yale ya maalbino.

Kwanini mauaji haya yanaambatana na ajali nyingi? Ni swali linalofikirisha.Tuwe makini na tumwombe Mungu atuepushe na maovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…