Entrepreneur
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 1,087
- 622
Huyu nae aliweza kufanikiwa baada ya kusaidiwa na wamerekani. Unaweza ukampata kwenye CLIP HII lakini anza HIIMoving Windmills share William's inspiring story with his fellow Africans, sparking initiatives to improve their difficult circumstances. William inspired his village to change the way it sees itself, and now because of him, many Malawians are building windmills, digging wells and harnessing their imagination.
Mkuu NDETICHIA bora wewe umeliona hilo. Hakika Mdada huyu ameleta/analeta mabadiliko. Lakini hapo kwenye red, huyu Vida alishaula awali pale wazo tu lake lilipopata kutambuliwa, kuthaminiwa na kuendelezwa. Na ndio maana tunasema tunahitaji kuwatambua hawa watanzania wanaofanya innovation huko vijijini (locally) ili tuwathamini na kuwaendelezabasi huyu dada vida kajitahidi sana yaani ukiwa na mawasiliano mazuri na hawa FTV kwenye mambo ya ulimbwende umeula..
Wazo hili limekuwa linajia kichwani mara kwa mara hasa baada ya kukutana na Mtanzania mwenzetu, ndg,Zacharia Zamokewakati anaanza kufanya utafiti wake juu ya namna ya kutengeneza Incubator, nilivutiwa zaidi baada ya kukutana na Dada mmoja aitwaye Vida Mahimbo, na kujua historia ya namna alivyoanza kwenye designing and Fashion hususani khanga Jeans. Na sasa baada ya kusoma kitabu cha William naona ni wakati muafaka.
Labda kwanza tujiulize; Ni vijana wangapi wanaogundua vitu vyenye maana na kazi zao zinapotelea angani? Ni vijana wangapi wameshindwa kuziendeleza tafiti zao zenye manufaa kwa jamii kwa ukosefu wa elimu? Ni vijana wangapi tunawaona kama ni vichaa wanapoanza kutengeneza vitu vyenye manufaa, na badala ya kuwasaidia tunawakatisha tamaa? Je hatuna uwezo wa kuwaendeleza watu hawa, au hatutaki kuwaendeleza watu hawa? Na ni vijana wangapi, ambao kama wangesaidiwa, kazi zao zingeweza kuboresha hali ya maisha ya Jamii zetu? Ndugu mwanaJF wakati ukiwa unatafakari maswahi hayo, naomba unipe muda wako na tusafiri pamoja ili tukakutane na;
1. Zacharia Zamoke- Imberruz
Huyu kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa kibiashara, aliamua kuwekeza nguvu zake kwenye utengenezaji wa Incubators za kienyeji kwa kutumia rasilimali zilizomzunguka, lakin baada ya miezi tisa akafanikiwa kuja na Mashine yake. Baada ya kuonekana na kusaidiwa, now he is making a Brand na amebalisha namna Watanzania walivyokuwa wanauangalia utotoleshaji wa vifanga hasa maeneo yasiokuwa na umeme. Anapatikana HAPA kwa sasa
2. William Kamkwamba - Moving Windmill
Huyu ni school dropout, ambaye alikosa ada, lakini akiwa na umri wa miaka 14 aliweza kutengeneza mtambo wa kuzalisha umeme, kwa kutumia local resources na blueprint ya kwenye kitabu cha Fizikia. Kama bado hujapata kitabu chake THE BOY WHO HARNESSED THE WIND, nakushauri ukitafute kwani hutajutia fedha yako. It had a profound impact on me.
Huyu nae aliweza kufanikiwa baada ya kusaidiwa na wamerekani. Unaweza ukampata kwenye CLIP HII lakini anza HII
3 . Vida Mahimbo – Khanga Jeans
Tanzanian designer Vida Mahimbo has set her sight towards conquering the fashion world with her creative khanga jeans collections. She now conquer Europe,African and US market, with the same collection. Huyu ni mtengenezaji maarufu wa Jeans za akina Dada maarufu kama "khanga jeans", (hii ni Brand mpya kabisa katika ulimwengu wa fashion), lakin nae aliweza kufanikiwa baada ya kupata Msaada kutoka kwa Waitaliano. Unaweza ukampata HAPA
WanaJF,kwa kutambua uwepo wa wadau wetu katika sehemu kubwa ya nchi hii, na kwa kutambua uwepo wa watu (innovators) wanaojihusisha na uvumbuzi, huko vijijini na uvumbuzi wao unapotelea angani bila kuendelezwa au kuwa inspiration kwa watu wengine. Ninaomba yeyote mwenye taarifa za watu wa aina hii wawe wanatupia taarifa hizo kwenye thread hii ili tuweze kuwathamini na kuwaendeleza
Did I hear everyone say "Amen?"
Thank you.
Tunahitaji kuwatambua ili tuwathamini na kuwaendeleza
One individual can make a Difference.
MKUU KWA HUYO NO MOJA
1. Nijuavyo mimi wavumbuzi wano tengeneza vitamishi vya mayai ya kuku wako wengi sana sasa swali linakuja je waendelezwewote au huyo mmoja tu?
Mimi nilitembeleaa monyesho ya kilimo ya nane nane, nilikutana na wavumbuzi tofauti 10 wa viatamishi sasa mimi nzani ni bora kuwaendeleza wote
2. Mkuu kingine hata hawa wavumbuzi wana makosa mengi sana na wanatakiwa kujifunza kwanza na uvumbuzi huchua miaka mingi sana hata wakina HENRY FORD iliwachua miaka mingi sana mpka kuja na real Car
- Cheki kwenye post yangu hapa wambuzi wa ndege iliwachua miaka
- Sasa Watanzania tunagundua kitu leo kesho mtua anaanza kukiuza tena kwa bei ya juu sana yaani yeye anatageti faida, mimi nilimhoji mmoja wa watengeneza viatamishi nikamuuliza Una muda gani tangu kugundua hii kitu?
ALINIJUBU NI MIEZI 9 NA HAPO ALIPOMKUWA ANAIUZA HIYO ALIYO GUNDUA YA KWANZA, NDO MAKOSA TUNAYO FANYA, NI LAZIMA KWANZA WALENGE MIAKA HATA 20 IJAYO NA SI KUGUNDUA LEO NA KESHO WANATENGENEZA TENA WANAANZA NA UCHAKACHUAJI KABISA,
- Kuna jamaa mmoja aligundua jiko zuri sana na yeye alikuwa na muda mfupi sana, cha kusikitisha alianza kutengeneza order za watu kwa kuchakachua vitu sana hebu fikilia mtu kama huyu ana tageti nini?
Mkuu hatuhitaji kumuendeleza huyo namba moja pekee kwani yeye ameshapata watu wa kumuendeleza na sasa ana brand yake ya Imberruz. Nadhani hao wengine kumi (uliowasema) ndio wanaohitaji huu msaada wa kuendelezwa zaidi kuliko huyo Bw. Zakaria niliyemtaja. Sasa tungepata kujua their side of story ingekuwa ni muafaka sana.
Halafu watanzania wengi, wanaojihusisha na uvumbuzi, wanakosa msaada mhimu katika kujiendeleza ndio maana product zao zinakuwa za mashaka. Hata maswala ya Intellectual Property protection hawayajui ndio maana uvumbuzi wao unaishia kuchakachuliwa baada ya muda mfupi. Lakin pamoja na haya yote bado tunahitaji kuwajua watu hawa ili tuwathamini na kuwaendeleza
Hapo kwenye RED ndio matatizo ya kutokuwa na R&D Institution kwani utafiti unagharama kubwa sana. Sasa kwa kuwa wavumbuzi wengi wanakosa finacing katika tafiti zao na piloting, matokeo yake ni kulipua kazi ili kufidia gharama. Wengi wao wanatumia kile kidogo walichonacho na wakifanikiwa tu kuzalisha wanachokihitaji, basi wanafikiria kwanza kurudisha gharama zao, kabla watoto wa mjini hawajaanza kuchakachua utaalamu wake. Hili ni tatizo kubwa, lakin pamoja na hayo bado tunahitaji kusikia historia zao
1. Ni kweli wanakosa msaada ila tatizo kubwa kwao ni kwamba wanawaza pesa mara tu baada ya kuvumbua, hawawai kuja kuwa watu muhimu katika Dunia hii wao wanawaza pesa,
2. Kuna yale mashirika ya Serikali nazani ndo wanahusika kuwa endeleza ingawa hawa watu wa serikali wako kiulaji sana,
3. Na kingine ili wafanikiwe ni lazima na sisi tupende vitu vya Tanzania hata kama havina Ubora, Watanzania wanachikia sana vitu vya ndani ya nchi na hata wewe jiulize ndani mwako sufuria unazo pikia zimetengenezwa wapi? je Meza ya komputa?
China kwa mara ya kwanza walivyo tengeneza JEIFONG YAO/ TIPER YAO walichekwa sana na nchi za ulaya kwamba ina sura ya ajabu lakini kiongozo wao wa mapinduzi alisha sema hawatakaa waagize kitu kutoka nje labda malighafi tu na wachina waliunga mkono kwa kununua vitu vya kwao hata kama vilikuwa havina ubora
Wazo zuri sana kuwatangaza na kuwaendeleza wavumbuzi na wafabiashara wetu wa ndani. Shida kubwa ni pale SERIKALI YETU inapataka watu waagize mpaka vibiriti, sukari, maboga, machungwa, maembe, nk wakati vinaweza kuzalishwa hapa hapa nchini kwetu.
Once mtu anapogundua kitu na kuweza kutumika, the next big thing is market. Kama huna soko, huo ndio mwisho wako. Kwa hiyo inabidi tuanze kuibana serikali yetu iache hii tabia ya kutoa vibali vya kuagiza kila kitu.
Source; The guardian of 19th October 2009. Ex-army officer-cum-inventor struggles for recognition. By Lucas LukumboCaptain Athumani Msekeni's zeal for invention was manifested when he was in the army. In 1977 he sought audience with Mwalimu Julius Nyerere, Chief of Armed Forces to sell his idea of making strong chassis and boards for some military vehicles. This was after finding out that certain military vehicle chassis were not durable especially when subjected to rigorous military exercises.
"I went to Mwalimu's place with two models I made. One was my own model and the other was the one from outside the country. I asked him if he could sponsor me to rectify the anomaly by making our own type of chassis," he narrated.
Unayoyasema ni ya ukweli Kamuzu, ndio maana ninapendekeza sisi kwa sisi tuwatambue, tuwathamini na kuwaendeleza bila kuwawetegemea hao viongozi wetu. Kwani kwa miaka hamsini hapa ndipo walipoweza kutufikisha. Yaan hata tooth pick na cotton buds tunaagiza kutoka china!Akili ya viongozi wetu ipo kwenye KUOMBA so hawaoniumuhimu wa kuwaendeleza watu wenye mawazo ya ubunifu kama hawa, labda wangekuwawatoto wao, hapo, lalalalala..... tungesikia filimbi zinavyopigwa.
Lakini wapi, mtoto wa kigogo au fisadi hawezi kuwa mbunifu ki hivyo kwaniubunifu aghalabu huambatana na shida aliyonayo mtu jambo ambalo kwa wenyeukwasi halipo.
Wakuu, mimi kama mjasilimali swala la Kuleta Venture Capitalist (Business incubator) bado ninaliwaza kila siku. Nadhani Tanzania kuna idea nyingi na innovators wengi lakini hakuna capital allocation system nzuri. Mitaji ipo sababu surplus zipo lakini allocation of capital to entrepreneurs ndio hakuna na hapo ndipo ninapowaza kuwekeza.
Hawa innovator wanatakiwa kupewa mtu ambae atawapa capital na atawapa business strategy "know how". Nikimaanisha, kuumpa mtaji, kumuongoza kwenye hatua ya Research & Development, kisha kwenye hatua ya kutafuta patent na mwisho kwenye hatua ya kuzalisha na kuleta product sokoni. Venture Capitalist ndio walio sababisha dot com business inyanyuke kwa haraka ndani ya muda mfupi.
Sikubaliani na wale wanaotaka serikali iwape mitaji hawa wajasilimali, bali nakubaliana na wale wanaosema serikali itakiwa iondoe ukiritimba kwenye sehemu zote muhimu kuanzia kusajili biashara yako mpaka kuondolewa tax kwa muda fulani. Watanzania wanaweza wakiwezeshwa.
Kuna watu walidhani business incubators ni lazima zianzishwe na serikali au kwa msaada wa NGO kubwa za kimataifa. Lakini nimeshuhudia private enterprise zikifanya hii kitu South Africa, tena kwa faida na mafanikio makubwa sana. Sasa Mkuu Mtanganyika, kikwazo kwako ni nini? Mbona huanzi?
Kwa sasa nimeona watu wa COSTECH wanafanya hii kitu hasa kwenye maswala ya ICT. Lakini bado kuna watu wengi sana out there ambao ubunifu wao unapotea kwa kutokuendelezwa
Entrepreneur kuna mambo mawili matatu yamesimama njiani lakini mpango huo upo. Nadhani hatuitaji serikali kwenye swala hili.
...Anyway, kwa sababu huyu jamaa kasema inaitwa gesi550 - basi habari zake ni kama hizi
The Gesi 550 is the first and smallest Biogas system in the range of Urban digesters that will be available from Januari 2012. The system is designed for the amount of organic waste of an average (peri) urban family.
Specifications:
Requirements:
- Capacity: 550 litre
- Diameter: ca. 1 meter
- Height: ca. 1.3 meter
- Maximum daily input: 3 kg organic household waste
- Output: ready-to-use gas and organic fertilizer
- The system includes complete installation, a stove, all necessary user training and service.
Price and savings:
- Outside space of 1,5 m2
- Input: organic waste 1-3 kg/day and water 5-15 L/day
During 2012, two larger systems within the Urban range will be launched. These systems have a larger capacity, and are designed for more commercial application. SimGas is also developing a range of biogas systems for rural use, suitable for manure, kitchen and agricultural waste. Check this website to stay informed !
- Introduction price: TSh 550,000/= including VAT.
- The price includes complete installation and a stove, all necessary user training and service.
- Average savings are TSh 1500/= per day, previously spend on charcoal.
- A biogas system has an average payback time of one year.
- Information about loan schemes is available on request.
Demonstration of Gesi550 and stove Gesi550 system installed Satisfied Biogas user