Tuwatake radhi waarab!

Tuwatake radhi waarab!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,454
Wadau jana nimesikia katika habari za jioni za BBC kwamba nchi wanamotoka wale vijana wanne watuhumiwa wa mlipuko wa Bomu Arusha, wanaitaka Tanzania iwaombe radhi kwa kuwachafua na kuwasababishia usumbufu, Tanzania isipofanya hivyo watavunja uhusiano wa kibalozi na nchi yetu. Je;-

1. Ni utaratibu wa vyombo vya usalama kumtaka radhi mtu au nchi anayotoka kwa kumtuhumu?
2. Hizo nchi hazijawahi kuwatuhumu Watanzania kwa uharifu hata mara moja na kuwakuta hawana hatia?, kama imewahi kutokea walitutaka radhi?
3. Hizi tuhuma kwa hawa vijana zina uzito wa kuvunja uhusiano wa Kibalozi baina ya nchi na nchi iwapo hawatatakwa radhi?

Naishauri Serikali iwatake radhi haraka iwezekanavyo hizi nchi kama ina utaratibu wa kuwataka radhi suspects wote wa uharifu ambao baadaye wanagundulika hawakuhusika, isifanye hivyo kwasababu imetishiwa kuondolewa uhusiano wa kibalozi
 
Kutenda na kuenenda kwa hisia badala ya kutumia ujuzi na weledi ni kubaya sana...Vyombo vya dola vilikuwa na uwezo wa kuwahoji na kisha kuwaachia kimya kimya baada ya kujiridhisha TOFAUTI na walivyoitangazia dunia eti wamewakamata vijana wa kiarabu! Keyword hapa ilikuwa WAARABU! Lengo la Serikali ilikuwa ni nini hasa?...
LAZIMA waombe RADHI kwa kuitangazia dunia kwa walifanya makosa...
 
kazi ya usalama wa ccm kuwaondoa watu kwenye hoja ya ujangili wa kinana imezua mabalaa,sasa wawaombe radhi wamanga,wametuulia ndugu zetu bure sababu za siasa,ccm bure kabisa.
 
waarabu wametutawala kwa zaidi ya miaka 600.
Kimsingi wanatudharau sana.
KAMA INGEKUWA WALIKAMATWA USA,KWANZA WASINGEACHIWA KWA SIRI NA KWA HARAKA KIASI HIKI WAKATI UPELELEZI BADO UNAENDELEA.
haya ndio madhara kwa watu weupe kutuita sisi ni masikini alafu tukaitika na kulikubali jina fake la NCHI MASKINI.
NA MBAYA ZAIDI HATUISHI KWENDA KWAO KULIA NJAA NA KUTAKA MISAADA.
nchi ni pamoja na watu, pamoja na ardhi kama eneo lililo na raslimali chungu nzima.wanaita nchi yetu MASKINI nasi tunaitikia NDIOOO.......
kama mle bungeni SASA WATATUESHIMU SA NGAPI?
NINGEKUWA MIMI SIWATAKI RADHI NG'O.
na hata NYERERE ALIWAHI KUSEMA SISI NI MASKINI JEURI.
siku hizi imekuwa kinyume mana kila siku hatuishi kwenda kulia shida.
MI MALI YOTE TUNAIUZA KWA BEI YA SAWA NA BURE ALAFU TUNALIA?
najua watakuwa wameshaomba radhi tayari kwa siri kama walivyowaachia kwa siri na taarifa TUKAPATA toka AL-KHALEEJ huku kukiwa hakuna taarifa ya mapema toka awali ndani ya nchi yetu.
 
Wadau jana nimesikia katika habari za jioni za BBC kwamba nchi wanamotoka wale vijana wanne watuhumiwa wa mlipuko wa Bomu Arusha, wanaitaka Tanzania iwaombe radhi kwa kuwachafua na kuwasababishia usumbufu, Tanzania isipofanya hivyo watavunja uhusiano wa kibalozi na nchi yetu. Je;-

1. Ni utaratibu wa vyombo vya usalama kumtaka radhi mtu au nchi anayotoka kwa kumtuhumu?
2. Hizo nchi hazijawahi kuwatuhumu Watanzania kwa uharifu hata mara moja na kuwakuta hawana hatia?, kama imewahi kutokea walitutaka radhi?
3. Hizi tuhuma kwa hawa vijana zina uzito wa kuvunja uhusiano wa Kibalozi baina ya nchi na nchi iwapo hawatatakwa radhi?

Naishauri Serikali iwatake radhi haraka iwezekanavyo hizi nchi kama ina utaratibu wa kuwataka radhi suspects wote wa uharifu ambao baadaye wanagundulika hawakuhusika, isifanye hivyo kwasababu imetishiwa kuondolewa uhusiano wa kibalozi
Mkuu haya ni mazoea ya vyombo vya usalama ya kubambikizia watu kesi.Wamezoea kutubambikizia kesi na leo wanafanya hivyo hivyo kwa watu

Tuhuma za Ugaidi zinachafua image ya Nchi husika.Dunia ipo vitani dhidi ya ugaidi sasa unapombambikizia mtu tuhuma kama hizi na kuzitangaza kisha ikaonekana hawahusiki ni lazima uombe radhi kwa namna ile ile uliyotumia kutangaza
 
Safari hii 'political diversion' ya serikali imeenda mrama vibaya sana.

Walitaka kutumia tukio la bomu kanisani ili kusahaulisha watanzania kuhusu kashfa za ujangili wa katibu mkuu wa ccm taifa..
Wametekeleza tukio hilo, lakini halikuweza kusahaulisha watu kuhusu ujangili wa Kinana.

Mwaka 2011, walimtumia babu wa Loliondo ili kuwasahaulisha watu kuhusu uchaguzi uliochakachuliwa wa 2010.
Pia babu huyo alifanikiwa kuwasahaulisha watu kuhusu kashfa za Dowans, n.k.

This time imekataa...!!!

OOOpppppsss...!!!!
This time the 'political diversion' has gone horribly wrong... !!!!
 
Kutenda na kuenenda kwa hisia badala ya kutumia ujuzi na weledi ni kubaya sana...Vyombo vya dola vilikuwa na uwezo wa kuwahoji na kisha kuwaachia kimya kimya baada ya kujiridhisha TOFAUTI na walivyoitangazia dunia eti wamewakamata vijana wa kiarabu! Keyword hapa ilikuwa WAARABU! Lengo la Serikali ilikuwa ni nini hasa?...
LAZIMA waombe RADHI kwa kuitangazia dunia kwa walifanya makosa...
Hakuna kitu kibaya kama vyombo vya habari kufanya mambo kwa maagizo ya wanasiasa, ninaamini kabisa kulikuwa hakuna haja kabisa kutanga majina ya watuhumiwa ilihali uchunguzi haujakamilika, majina ilitakiwa yatajwe wakati wa kuwapeleka mahakamani
 
Wadau jana nimesikia katika habari za jioni za BBC kwamba nchi wanamotoka wale vijana wanne watuhumiwa wa mlipuko wa Bomu Arusha, wanaitaka Tanzania iwaombe radhi kwa kuwachafua na kuwasababishia usumbufu, Tanzania isipofanya hivyo watavunja uhusiano wa kibalozi na nchi yetu. Je;-

1. Ni utaratibu wa vyombo vya usalama kumtaka radhi mtu au nchi anayotoka kwa kumtuhumu?
2. Hizo nchi hazijawahi kuwatuhumu Watanzania kwa uharifu hata mara moja na kuwakuta hawana hatia?, kama imewahi kutokea walitutaka radhi?
3. Hizi tuhuma kwa hawa vijana zina uzito wa kuvunja uhusiano wa Kibalozi baina ya nchi na nchi iwapo hawatatakwa radhi?

Naishauri Serikali iwatake radhi haraka iwezekanavyo hizi nchi kama ina utaratibu wa kuwataka radhi suspects wote wa uharifu ambao baadaye wanagundulika hawakuhusika, isifanye hivyo kwasababu imetishiwa kuondolewa uhusiano wa kibalozi
Over my dead body.
Watanzania wanaohlsiwa huko Uarabuni umeombwa radhi mara ngapi?
Ukijidharauu utadharauliwa.
 
Mie naomba wale wenyeji wao<watanzania> waliokamatwa nao waachiwe huru kasoro driver wa boda boda tu japo nae ushahidi ukikamilika aachiwe huru kwani sio sahihi kumfungulia mashitaka ya ugaidi halafu hapo hapo bado tunamtafuta mtu aliehusika kulipua bomo kwa donge nono la M50? sasa huyu aliepelekwa mahakamani ni shahidi wa kwanza ama mhusika msaidizi ama mhusika mkuu?

Na kwa nini upelelezi wa raia wa kigeni ukamilike haraka hivyo kuliko upande wa raia wetu ambao tunaweza fatilia mpk kwa babu zao i mean chimbuko lao na ushahidi ukakamilia within a month or weeks? Raia hana thamani hapa nchini ila mgeni anathaminiwa kisa anatuletea dolali?
 
Safari hii 'political diversion' ya serikali imeenda mrama vibaya sana.

Walitaka kutumia tukio la bomu kanisani ili kusahaulisha watanzania kuhusu kashfa za ujangili wa katibu mkuu wa ccm taifa..
Wametekeleza tukio hilo, lakini halikuweza kusahaulisha watu kuhusu ujangili wa Kinana.

Mwaka 2011, walimtumia babu wa Loliondo ili kuwasahaulisha watu kuhusu uchaguzi uliochakachuliwa wa 2010.
Pia babu huyo alifanikiwa kuwasahaulisha watu kuhusu kashfa za Dowans, n.k.

This time imekataa...!!!

OOOpppppsss...!!!!
This time the 'political diversion' has gone horribly wrong... !!!!

Mi nadhani wawatake Radi tu yaishe kwani itatughalimu nini? kwasababu uhusiano wa kibalozi ukifungwa na hizi nchi itakuwa na impact kubwa sana kwa Watanzania hebu jaribu kufikiria ikitokea Saudia Arabia inaondoa Ubalozi Tanzania, watu wanaokwenda kuhiji itabidi wafuate Visa nchi jirani, itawaumiza sana Watanzania
 
Mkuu haya ni mazoea ya vyombo vya usalama ya kubambikizia watu kesi.Wamezoea kutubambikizia kesi na leo wanafanya hivyo hivyo kwa watu

Tuhuma za Ugaidi zinachafua image ya Nchi husika.Dunia ipo vitani dhidi ya ugaidi sasa unapombambikizia mtu tuhuma kama hizi na kuzitangaza kisha ikaonekana hawahusiki ni lazima uombe radhi kwa namna ile ile uliyotumia kutangaza
Tatizo kubwa ni kwamba vyombo vyetu vya usalama vimejiingiza katika Siasa, Professionally huwezi ukataja jina au nchi ya mtuhumiwa wakati bado unaendelea na upelelezi, kwanza unaichafua nchi husika pili unamchufua muhusika na Tatu unaweza kuvuruga upelelezi, hebu fikiria kitendo cha kumtaja Victor Amrose ilihali unaendelea na upelelezi hawaoni kwamba kwa namna moja au nyingine inawafanya aliokuwa nao ikiwezekana wajifiche zaidi? Ninaamini vyombo vyetu vya uasama vina watu wenye weledi wa kutosha ila wameamua kutokuutumia ili kutuharibia nchi yetu kwa makusudi
 
Serikali inaweweseka na haijui ifanye nini? Polisi wa leo hawana utaalamu wowote, kwani asilimia kubwa wamefoji vyeti. Kilicho bakia ni kubambikizia watu kesi.
 
Mkuu haya ni mazoea ya vyombo vya usalama ya kubambikizia watu kesi.Wamezoea kutubambikizia kesi na leo wanafanya hivyo hivyo kwa watu

Tuhuma za Ugaidi zinachafua image ya Nchi husika.Dunia ipo vitani dhidi ya ugaidi sasa unapombambikizia mtu tuhuma kama hizi na kuzitangaza kisha ikaonekana hawahusiki ni lazima uombe radhi kwa namna ile ile uliyotumia kutangaza
Mkuu sisi kama chadema pamoja na Rwakatale tunapaswa kuombwa msamaha na hii jamuhuri kwa kutuzushia kuwa chadema na kiongozi wetu ni magaidi???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu haya ni mazoea ya vyombo vya usalama ya kubambikizia watu kesi.Wamezoea kutubambikizia kesi na leo wanafanya hivyo hivyo kwa watu

Tuhuma za Ugaidi zinachafua image ya Nchi husika.Dunia ipo vitani dhidi ya ugaidi sasa unapombambikizia mtu tuhuma kama hizi na kuzitangaza kisha ikaonekana hawahusiki ni lazima uombe radhi kwa namna ile ile uliyotumia kutangaza

Wamekurupuka sana, wamezoea kuwabambikiza kesi Watanzania na kuwachafua kwa tuhuma kadri wawezavyo na mambo yanapita jujuu juu sasa wamejisahau wakaenda mbali kufanya maamuzi ya kukurupuka bila kujua madhara, wawatake radhi basi, wao wanadhani ukimsingizia Ugaidi lwakatare akikaa kimya basi unaweza ukamfanyia mtu yeyote. CHADEMA tuandamane nchi nzima kumtaka DPP amtake Radhi Lwakatare kwa kumchafua kwamba ni gaidi
 
masikini hao Waarabu nchi zao zinawathamini na zimeinuka kuwatetea lakini angalia mtoto aliye katika nchi asiyeweza kutetewa anaelekea sasa kufanyiwa kama ya ndugu yake Rwakatale!!!
 
Over my dead body.
Watanzania wanaohlsiwa huko Uarabuni umeombwa radhi mara ngapi?
Ukijidharauu utadharauliwa.

are you speaking for mr. jakaya kikwete or what?he doesn't think that way,atawaomba radhi kupitia kwa membe,kwa nini asifanye hivyo wakati yeye kila siku kiguu na njia nchi za wenzake,for him to satisfy his traveling thirst,he will put your so called pride at humiliation..we know him better.
 
Kutenda na kuenenda kwa hisia badala ya kutumia ujuzi na weledi ni kubaya sana...Vyombo vya dola vilikuwa na uwezo wa kuwahoji na kisha kuwaachia kimya kimya baada ya kujiridhisha TOFAUTI na walivyoitangazia dunia eti wamewakamata vijana wa kiarabu! Keyword hapa ilikuwa WAARABU! Lengo la Serikali ilikuwa ni nini hasa?...
LAZIMA waombe RADHI kwa kuitangazia dunia kwa walifanya makosa...

Imetulia hii! Mijipolisi ya kibongo ni mizuzu!! ha ha ha Inakenua tu! Hii yote sababu ya lisirikali legelege! yani limefanya kila kitu kimekuwa legelege.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom