Yaani wewe fikiria gharama za zabuni iligharamia serikali si uchuro huo, bilioni tatu watu Wamekula chai...Halafu unaniambia lipa Kodi lipa Kodi dadeki lazima tuuane.
Padre Dkt. Charles Kitima, Katibu wa TEC, ameibuka na ujumbe mkali mtandaoni kufuatia kutolewa kwa ripoti ya CAG, akigusia moja kwa moja kauli ya Rais kuhusu kuwataja wahusika ili “waone aibu.”
Katika andiko lake, Kitima alieleza kuwa aibu pekee haitoshi kama njia ya uwajibikaji, akisisitiza kuwa ripoti hiyo inaonyesha wazi uwepo wa hasara na mapungufu yanayohitaji hatua za kisheria na kinidhamu, si onyo la maneno tu.
Aliongeza kuwa uwajibikaji wa kweli unahitaji hatua madhubuti dhidi ya wahusika, jambo lililochochea mjadala mpana mtandaoni kuhusu namna bora ya kushughulikia hoja za ripoti ya CAG.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.