Nadhani imefika wakati tuchore mstari wa kuanza kujenga taifa jipya lisilokuwa na visasi wala malipiziano ya makosa yaliyofanywa na mtu siku za nyuma.Tuwafungulie wafungwa wote na tusamehe kesi zote zinazoendeshwa ili taifa libaki jeupe na lenye mshikamano.Tuweke sheria kali kwa wataofanya makosa mapya kuanzia kipindi hiki. lakini kama mtu aliiba fedha nyingi za serikali na kuzificha nje ya nchi basi tumwamulu azileta na kuwekeza nchini kwetu kwa manufaa ya uchumi wetu. Nadhani kwa mwendo huu baada ya miaka 5 taifa litakuwa mbali kwani kuna takribani trion zaidi ya 9 zilizofichwa na mafisadi nje ya nchi ambazo zikiingizwa kwenye uchumi Tanzania itakuwa kwa kasi na wananchi wengi watanufaika.