Pole mama Tanzania tangu ujinasue toka utumwani mpaka sasa umepitia wakati mgumu sana

Observe

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
294
140
Jinsi ulivyomzuri MAMA angu TANZANIA!!! hakika Mungu alikuumba mrembo sana, Yaani TANZANIA wewe ni mrembo, umepambwa na mwili wako haujapungukiwa chochote isipokuwa sisi watoto wako ndiyo tumekuumiza sana kwa tamaa yetu, upungufu mkubwa wa upendo juu yako. Yaani sisi wanao tumekuumiza mno hatuna upendo wa kweli kwako bali. Yaani baadhi yetu mpaka tumefikia hatua ya kukuuza kwa wageni baadhi ya viungo vya mwili wako ili mradi tu tushibishe nafsi zetu bila kujali ni maumivu gani utayapata au kansa, kisukari, au moyo. tumekuumiza sana mama yetu.

Kimsingi mwili wako MAMA TANZANIA uliumbwa kutunyonyesha sisi wanao ili tukue na afya bora na wenye nguvu, maziwa yako Mungu aliyaweka kwa ajili yetu ili tuyatumie na kupata kinga toka maambukizi ya magonjwa nyemelezi. Lakini cha kusikitisha tumewaalika watu toka mbali, sisi wenyewe tumekuletea yale majambazi yaliyokuwepo hapo kale ambayo mababu zetu waliyafukuza kwa juhudi kubwa na nguvu nyingi. Kwakweli yaliondoka na wakabaki watoto wako tu ambao mwnyezi Mungu alikupa uwalishe na kuwalea vyema kulingana na wingi na utamu wa chakula alichokugawia Muumba.

Hebu tazama uzuri ulionao, mito mizuri, maziwa yenye yalijaa maji kiasi kwamba hata kama tungeanzisha kilimo cha umwagiliaji bado tusingeyamaliza kabisa kwakuwa aliyeyaweka alijua uhitaji watakaokuwa nao watoto wako. Hebu ona watu wa mashariki ya katiwanavyofaidi maji yako; Tangu Muumba akuumbe kamwe MAMA Tanzania haujaacha kutiririsha maji katika mto Nile, masaa ishirini na nne umemjaza Nile na maji yako kupitia beseni lako ziwa Victoria, hakuna anayekupa wa kukuongezea wewe sawasawa na kiasi unachotoa.

Milima mizuuuuriii, mabonde mazuuurii na yakupendeza yako juu ya mwili wako mama Tanzania. Ndani ya tumbo lako umebeba dhahabu lukuki, almasi, gase, mafuta, na kile ambacho hakuna mwamke mwingine anayeweza kuwa nacho-tanzanite, lakini bado sisi wanao tumewaita tena wale wasiokutakia mema na kuwakabidhi mali zooote hizi nasi tukageuka kuwa ombaomba kwao, kwahiyo sisi wanao hatuwezi kula tena kupata maziwa freshi yatokayo mwilini mwako bali tunakunywa kwa kutegemea ka mgao toka wageni. Kwakweli tumejikondea saaaaana, kibaya zaidi wale tuliowarejesha tena ndiyo wameanza kutupiga na kiamua leo ni kiasi gani cha chakula
tutakula, yaani tusamehe mama TANZANIA tumekosa sana; Ee BWANA MUMGU tusamehe sisi na baba zetu tumetenda yasiyo faa mbele zako, tumejiuza kwa wageni, tumeuza urithi uliotupa ili tumiliki, sisi kwa ujinga wetu tumewaita wageni na kuwamilikiwa nchi yetu ulitupa; tumekosa; tumekosa tumekosa sana sisi na viongozi wetu; Basi Mungu, Muumba wa mbingu na nchi tusamehe maana
kwako kunarehema nasamaha japo sisi tumetenda maouvu.

Tulipopata uhuru miaka ya 1961 tulianza na kauli ya kutokomeza maadui wakubwa watatu -ujinga- maradhi na umasikini kwa kauli mbio kwamba "Let's run while others are walking" ngoja sisi tukimbie wakati wengine wanatembea-

Mwalimu Nyerere alijitahidi sana sana lwa mguvu zake zote usiku mchana mzee wa watu hakulala akiumiza kichwa ni kwa jinsi gani Tanzania itajitegea na kuacha kusubili mzungu atuletee hela. Kimsingi Mwalimu alijua madhara ya hela ya kupewa na athari zake kwa ukuaji wa taifa. Ukisikiliza baadhi ya hotuba zake alifikia hatua ya kuwaita hawa ndugu "wasenzi" hivyo Mwalimu alikemea sana rushwa na ufisadi kwakuwa alijua taifa la watu wala rushwa na wapenda ufisadi kamwe halitaweza kabisa kujaendelea hata kama ni kwa miujiza. Hivyo alijipambanua kuwa ni mtu asiyechanga siasa na biashara kwakuwa kiongozi maana alijua tabia za wafanyabiashara wa Tanzania ziko tofauti na za wamarekani. Mmarekani yuko tayari biashara yake idolole lakini America iendelee kuwa juu. Hapa kwetu mfanya biashara anatafuta nafasi ya iongozi ili awe na mamlaka ya kukwepa kodi wakati huohuo analiibia taifa hata kwa kile kidogo kinachokusanywa.

Mwalimu alituachia viwanda vingi na zinafanyakazi. Awamu ya pili iliingia madarakani, sina hakika ni kwa sehemu gani awamu ya pili ilijitahidi kuvilinda hivi viwanda. Ni katika awamu hii tulishuhudia noti za 10000, 5000, 2000, 1000 kama kiashilio cha kushuka thamani ya shilingi baada ya serikali kuwasikiliza wamafharibi Benki ya dunia na IMF kwa kudhani kuwa ni watarusaidia. Hata hivyo wa kujilaumu ni sisi wenyewe na siyo hao jamaa. Pamoja na hayo yote, awamu ya pili ilimaliza wakati wake hutu tukiwa na deni kubwa mno lakini ukiangalia ni kwa kiasi gani tulitumia hiyo mikopo kwenye uwekezaji, hapa hakuna mwenye jibu sahihi.

Tulikuwa tunakopa hela kwa ajili ya mishahara badala ya kuwekeza kwenye uzalishaji, huku ufisadi ukiota mizizi, wala hakutuonelea umuhimu wa kuwa na sheria kali zidi ya udisadi, au viongozi wetu ndo walikuwa wanafisadia taifa, na ndo maana hawangewezakushughulikia ufisadi kwa dhati.

Hotuba ya Mwalimu wakati wa kutafuta mgombea wa CCM 1995 huko Dodoma alibainisha wazi kuwa watanzania wanataka mabadiliko, wamechoka kabisa na viongozi wala rushwa na mafisadi.

Awamu ya tatu ilianza huku ikikabiliwa na deni kubwa ambalo fedha zake hazikuonekana ziliwekezwa kwa kiasi gani ili kuuUjenga uchumi. Lakini pamoja na hayo yote, awamu ya pili iliiacha ardhi ikiwa bikira kabisa, hakuna muzungu aliyekuwa ameuzwa ardhi kwa ajili ya migodi ispokuwa mwadui.

Nadhani kosa kubwa linalotutesa na litakalotutesa lilianza kuonekana awamu ya tatu, pale serikali ilipokiri kushindwa kusimamia mashirika ya umma na kujikita kuyauza kwa wawekezaji huku sheria zetu zikiwa bado butu kuwachukulia hatua pindi washindwapo kuyaendeleza. Awamu hii ilijipambanua ya ubinafishaji na uwekezaji. Kwahiyo tulishuhudia viongozi wetu wakisaini mikataba ya mpaka miaka mia moja huku tukikubaliana na 3% na kumwachia mzungu abebe 97% huku tukijitapa kuwa rulichokifanya ni sahihi. Kimantiki haingii akilini kiongozi anayependa taifa lake aweke mikataba kama hii. Kwahiyo tulijiuza sisi wenyewe kwa makaburu, tulishuhudia mikataba ya akina Neti solution group ya makaburu eti ndo wangetusadia kuboresha TANESCO?? badala yake wakala hela na kuiacha TENESCO ikichechemea. Huku tukiendelea kukopa kila mwaka bila hata mkakati madhbuti wa ni lini tutajitegemea, kibaya zaidi serikali kwa nguvu zote serikali ikijitahidi kuficha uwazi wa mikataba hiyo kwa kile kilichoitwa siri za serikali bila kujua kuwa hiyo siri ni kamba ya kujinyongea wenyewe. Eti tunafanya siri na mzungu na kuwaficha watanzania wenzetu, sasa yako wapi?

Kwa miaka yote TANESCO imekuwa shimo la viongozi kuifilisi na kuingiza hasara nchi. Eti shirika kubwa kama hili halina pesa za kununua mitambo ya kuzalisha umeme, huku kajikampuni ka mtu binafsi ndo kanaweza, huku viongo wetu wakishangilia ma baadhi yetu tukiwaunga mkono ili mradi tu ni wachama chetu, wakati wamarekani wako tayari chama kianguke lakini America isonge mbele, sisi huku tuko tayari kuona nchi inaanguka na kupata hasara ili tu chama kiendelee na hii ndo tofauti tuliyonayo kati ya wazungu na sisi.

Tunasheria inayowabembeleza wazungu, eti tuko tayari kusamehe kampuni la madini lifanye kazi zake kwa miaka zaidi miwili bila kulipia ushuru na kodi tukidhani wazungu ni baba zetu wataruhurumia, baadhi ya viongozi wetu wakituaminisha kuwa hakuna tatizo huku watanzania wenzetu wakiathirika na mifugo yao kwa madawa mfano kule Nyamhongo. Viongozi tuliowachagua walipuuza kilio cha watu wetu hivyo kuathirika vibaya mno na hakuna wakuwalipa. Mzungu aliendelea na kazi za kutuibia na kibaya zaidi akishirikiana na baadhi yetu kulibia taifa, mzungu alipotimiza lengo lake akaibuka na kusema eti amepata hasara sana nasisi tutakubaliana. Hayo mashimo yaliyoachwa ni nani atayafukia? kwa gharama za nani? faida gani timepata? kwahiyo sera ya uwekeza na ubinafishaji iliyopigiwa upatu na serikali ya tatu imelitia hasara kubwa mno taifa kwa mikataba mibovu ya unyonyaji miaka mingi. Siamini kama viongozi walisaini tu bila wao kunufaika ma %fulan kwakua haingii akili mtu msomi kama huyo eti asini tu 3% bila yeye binafsi kunufaika.

Awamu ya nne iliingia na sera ya maisha bora kwakila mtz. Hata hivyo ikawa yaleyale, katika awamu hii yulishuhudia mikataba ya madini ikisainiwa nyumbani kwa wazungu bila hata kuzifanyia marekebisho sheria zeru-(siri ya serikali), na matokeo yake hakuna kiongozi yeyote mwenye ujasiri wa kuwaeleza watanzania ni kiasi gani taifa linapata kutokana na madini. juzi pia tumeshuhudiaikataba ya gase nayo ikisainiwa kwa staili ileile na hata pale tulipata watu wa kutuamsha tuliwazomea na kuwanga mkono wanaohujumu taifa ili mladi tu ni wachama chetu na hili ndo kosa kubwa sana. Wachina na wazungu waendelee lunufaika na watanzania wabaki yatima na kusubiri misaada inayotokana na faida wanayopata kutokana na dhahabu na gase yetu.

Katika awamu hii tumeshuhudia ufisadi ambayo haujawahi ripotiwa ktk historia yetu, yaani viongozi waliamua kuchukua mafurushi ya noti mchanamchana wala hakuna mamlaka iliyosubutu hata kukohoa, Raisi alihusika? hakujua juu ya hili?. kibaya zaidi viongozi wetu wanachukua hela hizi na kuziweka kwenye mabenki ya wazungu na ni hela hizi hizi wazungu wanazichukua na kutukopesha. Yale matrioni ya uswisi?

Taifa limekuwa halina dila kabisa wala mpango
wa kujinasua kutoka kadhia hii, ufisadi na rushwa ni fahari kubwa kwetu na siyo utaifa na tumekuwa tukiwashangilia viongozi wa aina hii-chama chetu bahna.

Siungi mkono ya Zanzibar, ila ninachotaka kisema hapa ni kwamba imeonyesha wazi kwmba sisi bila wazingu hatuwezi kabisa wakati huohuo serikali zetu kwa mda mrefu zimeshirikiana na wazungu hawa hawa kuiba rasili mali zetu ambazo kimsingi ndo urithi tuliopewa na MUNGU kama taifa kamili.

Tumeshindwa kabisa hata kuyaunganisha mashirika makubwa kama NSSF, PPF, GPF ili kupitia mitaji waliyomayo waitumie kuunda kampuni kubwa litakalojihusisha na utafiti wa
madini na gase ili kama taifa tuanze kuuza wenyewe madini na gase yetu nchi za nje na badala yake sisi wenyewe tumekuwa tukijiibia hata viakiba vilivyopo kwenye mashirika haya ma baadaye kujaribu kutunga sheria ten ya kutuumiza sisi kwa sisi eti mtu hataruhusiwa kuchukua mafao yake aachapo kazi mpaka atakapofikisha miaka 60? kisa tu kiongozi mmoja amekwapua pesa yote na kuifanyia mambo yasiyokuwa na faida kwa nchi.

Jana wazungu tulioshirikiana nao kwa mda mrefu kuiibia nchi yetu wamezuia ka trion kamoja tu, na taifa limeyumba wakati hiyo trion tunaweza kuipata toka kw mafisadi walituibia kwa mda mrefu endapo tutaamua kuwasaka usiku na mchana. Tunauwezo mkubwa wa kupata matrion toka kwenye mbuga zetu za wanyama lakni cha ajabu nahuko tunashirikiana na wazungu kutorosha wanyama wetu kinyela, lakini pia visheria vyetu vizaifu hata pale mtu anapokamatwa kwa kosa kama hili.

Mishahara hewa ndo yamekuwa maisha mema kwa mda mrefu bila kijua kuwa tuanjiua sisi wenyewe. Ni aibu kwa nchi yenye miaka 50 ya uhuru kubaki tegemezi 60% kwenye bajeti ua mwaka, inamaana inaonyesha ni kwa jinsi tusivyojua nini maana ya uhuru. Je endapo wazungu wakaamua kutotoa kabisa vihela vyao ambazo ksingi siyo zao bali ni faida ya matrioni yanayopata makampuni yao yaliyoko hapa TZ na yale matrion viongozi wetu wameibia nchi nw luyaficha huko tutafanyaje kama nchi?

Basi tuongee nao kwa upole ili watupe hizo hela ili kusudi sasa tuanze kutumia hizo hela tuanze kujipanga namna ya kujikwamua toka utegemezi, tuwekeze kwenye nishati na utafiti ili tuwe nashirika ya umma yakayojikita kwenye
kwenye uzalishaji zaidi. Mashirika yaliyopo iwe miarufuku kupeleka ruzuku huko bali yajiendeshe kwa faida tu yenyewe ndo yalete ruzuku hazinani. Pia tubadolishe sheria zetu za madini na gase kwmba lazima serikali ipate % zikazoleta faida kwa serikli na kwawekezaji mambo ya siri ifike mahali yapitwe na wakati hapo ndo tutaweza kusimama kwa 78% bila mzungu.Nabii alishaonya kuwa "Alaaniwe mtu yuleamtegemeaye mwanadamu moyoni mwake amemwacha BWANA"

Wafanyabiashara wa Tanzania wanazidi kupanua shell kumbe lengo lao ni kuagiza mafuta na kukwepa flow metres ili wasilipie ushuru stahiki. Wengine kupitia vijikampuni uchwara wanatafuta kuingia vimikataba vya ajabu na serikali ilimradi wanyonye huku wakoshikiana na baadhi ya watumishi wa umma. Hii ni laana kabisa itakayoleta umaskini kwa MAMA Tanzania.

Raisi Magufuli ametokea kuwa mmoja ya maraisi adimu sana kutokea Africa. Kusema ukweli huyu kiongozi ameonyesha kweli kweli kwaba hakuomba uraisi ili kuotafuna nchi kama wenzake waliomtangulia ukiondoa Mwalimu na pengine mzee Mwanyi, awamu ya tatu na nne yalikuwa ni majanga kwa nchi, na Tanzania imepata hasara kubwa mno kwenye hizo awamu. Wazungu ndo walionekana wa maana sana kumbe wanatumaliza kabisa wakishirikiana na maraisi wetu. Leo hii wanasema hawako tayari kutoa hela zao kwa Tanzania. Je hawa ndo bado tunawaona ndo watu wakutusaidia kwa ili nasisi tuimalishe uchumi wetu? sidhani!

Raisi Magufuli ameweka wazi kwamba wafanyabiasha wazawa wajitokeze kuwekeza kwenye nishati, uchimbaji na utafiti wa gase, crude oil, madini ili wazungu waje kama joint venture. Pia aliwashauri wajenge viwada vya kuchakata ngozi na kuzalisha aina ya bidhaa zote zitokanazo na ngozi na hivyo kuziba mianya ya wachina kutuuzia bidhaa za ngozi kwakuwa tunamifugo ya kutosha kabisa; sasa sijui bado wanajiandaa kwa hili au ni kweli mitaji yao ni ya juice" (Muhongo).

Kwanini hawayaki kuwekeza kwenye bonde la Ziwa Voctoria na kilimo cha kumwagili halafu tuone kweli kama wamisri watakuja kutuvamia?

Kwanini wafanyabiasha wa kitanzania wanataka kifanya biashara na serikali tu? je hawana hata mitaji ya kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa za nishati-vifaa vyote vya
umeme maji- taps na pipe, basi wajenge viwanda vya kutengeneza vyombo vyote vya ndani na fanicha maana tunamisitu ya kutosha kabisa.

Ni wakati sasa serikali kuptia TANESCO izalishe umeme wa kutosha kwa matumizi ya viwanda ili kuwavitia wawekezaji wa viwanda. Zile longolongo za vikampuni binasfi kuiuzia TANESCO umeme iwe mwiko kama Raisi alivyoagiza bali TANESCO yenyewe ijenge hiyo mitambo maana Mungu bado anatupenda tu ndo maana ametusaidia kupata gase tena bado tunaendelea kugundua nyingine hivyo basi tuichangamkie kuichomba kwa kasi ili tuzalishe na kuiuza nchi za nje kama vile wenzetu Uganda wanajiandaa kuuza mafuta yao.

Ni makala ndefuu: Pole wakuu kwa usumbufu utakaojitokeza wakati wa kusoma na kuchangia; kurekebisha kwenye makosa; kusahihisha, kwenye mapungu kuongezea.
 
tatizo mtoto anayenyonya sasa ni mkorofi..ameshang'ata chuchu moja ya titi la kushoto na sasa amehamia titi la kulia ambalo tayari chuchu yake nayo imeanza kung'atwa....toto korofi sana hili haliambiliki wala hatulii ili mama ampakate vizuri wakati wa kunyonya,walau angekuwa na miezi sita mama angeanza kumpa uji lakini mpaka sasa ana miezi mitatu kwenda wa nne ...toto hili linapayuka na linataka kila mtu alisikie likiwa linalia...cha ajabu hata anacholilia hakijulikani...mamake ameana kuchoka na hiyo chuchuya kulia ikiondoka ndo bas tena mama hataweza kunyonyesha tena...
 
Back
Top Bottom