Tuwapongeze Wabunge hawa wa CCM wampa makavu Waziri wa Fedha. Ndassa asema Waziri huwa ana kiburi na si msikivu

..mbona wakati wakipitisha BAJETI wabunge wa CCM walikuwa wakimsifia Dr.Mpango?

..sasa tangu bajeti imepitishwa na sasa hivi Dr.Mpango amekuwa mtu mbaya, mwenye kiburi na asisikiliza ushauri wa wabunge?

..kwanini imekuwa ghafla namna hii?

..nina hakika mkienda youtube mtakuta video za Mh.Hussein Bashe akimwagia sifa kemkem Waziri wa Fedha Prof.Mpango.

..Pia wakati wa ziara ya Raisi mkoani Kigoma Mh.Serukamba alipewa nafasi ya kuzungumza na alisifia sana utendaji wa serekali ya awamu ya 5. Sasa inashangaza kwamba miezi michache baadaye anaanza kuilaumu serekali ileile aliyokuwa akiisifia.

Cc Pohamba, tindo, Magonjwa Mtambuka
 
We must give out projections asking on the true performances of the past years. If the reports given by the Minister of finance before the parliament is intending to make some people happy, one day it will make himself sad and crying.
 
Wabunge wengi wa CCM wakianza kutumia akili zao na kwenda kama wawakilishi wa wananchi BUNGENI na sio kama sasa hivi wana akili za kuwakilisha chama wakaanza na kuisimamia pamoja na kuikosoa Serikali kama Hivi tutafika mbali sana nasio kila kitu ku support tu Wakiamini kila kitu kitapitishwa kwa kutumia uwingi wao.
 
Tunamuonea bure. Kiburi anacho mwenye mbwa..si mbwa

Kumsema mwenye mbwa ni makosa, sasa hapa manake ajiongeze dongo hili ni la kwake mwenye mbwa watu wanatumia tafsida wakifunguka zaidi wengine hawataweza kupeleka watu Nairobi. Tahadhari tu kaka ukiwaangali usoni woote hao yupo waliemwambia sio Mpango.
 
Hata mimi lakini kwanini Ndugai anawapatia muda watu kama kina kibajaji Sugu na msukuma na Lijuakali kuchangia uchumi mambo ambayo yapo nje ya uwezo wao wa kufikiri?

Masuala kama haya yanatakiwa watu kama hawa waliozungumza maana wamesema ukweli. Nadhani hawa ni ma back benches ulaya wanaitwa watu ambao japo wapo upande wa chama kinachotawala lakini lazima wajiaminishe ndiyo waunge mkono. Tukifika na kuendelea kama mjadala huu basi kuna mwanga mbele.

Nimependa uchangiaji wa Mbowe pia si vijembe ni facts. Taratibu tutafika tu.
Yeah, si unajua tena haki ya mtu..haijalishi unaweza ua, ni kwamba ukiomba na ni haki yako ni sharti upewe.

Ndugai naona amerudi kwenye his senses, aliwaambia wafunguke...ila asije akanuniwe, oooh...
 
Hao wabunge wametumwa, hawana cha maana zaidi ya unafiki, eti wanajidai kusema eti rais kakosa wasaidizi, unajua huo unafiki wa hao wabunge serikali inaujua na ndiyo maana haiwezi kuteteleka, itatekeleza sera zenye tija kwa maendeleo ya watanzania na siyo kupenyeza ajenda za kufaidisha mafisadi na wezi.

Sekta binafisi kwa sehemu kubwa ilitawaliwa na uchumi hewa, kilikuwa kichaka cha kuibia serikali
Jibu hoja za wabunge Serukamba na Bashe na kitu gani kifanyike kuukwamua uchumi wa nchi yetu, usikalie uzwazwa wa kutumwa!
 
Hahaha, wabunge wa ccm wanampingaMagu kwa mgongo wa mawaziri. Kila wanachofanya mawaziri wanaagizwa na Magu. Kwa sababu si heshima kumshambulia mfalme waziwazi, basi unawatwanga subordinates wake!
 
Hahaha, wabunge wa ccm wanampingaMagu kwa mgongo wa mawaziri. Kila wanachofanya mawaziri wanaagizwa na Magu. Kwa sababu si heshima kumshambulia mfalme waziwazi, basi unawatwanga subordinates wake!
 
..mbona wakati wakipitisha BAJETI wabunge wa CCM walikuwa wakimsifia Dr.Mpango?

..sasa tangu bajeti imepitishwa na sasa hivi Dr.Mpango amekuwa mtu mbaya, mwenye kiburi na asisikiliza ushauri wa wabunge?

..kwanini imekuwa ghafla namna hii?

..nina hakika mkienda youtube mtakuta video za Mh.Hussein Bashe akimwagia sifa kemkem Waziri wa Fedha Prof.Mpango.

..Pia wakati wa ziara ya Raisi mkoani Kigoma Mh.Serukamba alipewa nafasi ya kuzungumza na alisifia sana utendaji wa serekali ya awamu ya 5. Sasa inashangaza kwamba miezi michache baadaye anaanza kuilaumu serekali ileile aliyokuwa akiisifia.

Cc Pohamba, tindo, Magonjwa Mtambuka

Ndio Siasa!

Ulipaswa kushangaa Kama wangekuwa wamekariri kusifia au kukosoa tu Muda wote! Mtu anasifiwa na kukosolewa kwa Tukio sio appearance
Hata baadhi yetu humu Mf.mimi nikiona Jambo zuri Rais kafanya namsifia na Kama Baya namkosoa

The same kwa Dkt Mpango japo simkubali kabisa Hussein Bashe lakin alikuwa sahihi kumsifia Mh.Waziri wa Fedha wakati wa kutayarisha Mipango ( Budget) aliandaa vyema kwa kugusa sector Muhimu lakin kwny Implimentation ( utekelezaji) Kama hayaendi Kama yalivyopangwa ni haki na sahihi kukosoa!

Ukijiona umekeriri kusifia tu Mara zote au kukosoa tu Mara zote tambua una tatizo
 
Hao wabunge wametumwa, hawana cha maana zaidi ya unafiki, eti wanajidai kusema eti rais kakosa wasaidizi, unajua huo unafiki wa hao wabunge serikali inaujua na ndiyo maana haiwezi kuteteleka, itatekeleza sera zenye tija kwa maendeleo ya watanzania na siyo kupenyeza ajenda za kufaidisha mafisadi na wezi.

Sekta binafisi kwa sehemu kubwa ilitawaliwa na uchumi hewa, kilikuwa kichaka cha kuibia serikali
Don't be so rhetoric. Talk sense and we'll respect you.
 
Back
Top Bottom