Tuwapongeze Wabunge hawa wa CCM wampa makavu Waziri wa Fedha. Ndassa asema Waziri huwa ana kiburi na si msikivu

Bunge likiwa namna hiyo litatenda haki kwa nchi hii. Sio kila kitu kukosoa tu au kuunga mkono tu. Wabunge (ccm na wapinzani) waweke maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya vyama vyao. Nje ya hapo ni kujidanganya tu na hatutafika popote kimaendeleo.

Nafikiri Spika ameanza kuchukua ushauri/kufanyia kazi concerns alizo raise ZZK kuhusu bunge kutokuwa huru. Jambo jema.
 
100% hafai na hana nia njema na nchi yetu.
Unajiuliza nguvu kubwa hii inayotumika kutaka kuwaaminisha watu kuwa yuko sawa!!! Huku mawazo mbadala kwao ni haramu
Afadhali wameanza kufunguka maana hili jinamizi la uchumi na wapika data ni tishio na adui wa Taifa
Wakifunguka wao CCM ni sawa!!. Lakini wakifunguka kina Zitto, Lissu, Mdee nk mahabusu na Nissan inawahusu?! Tanzania ni nchi ya ajabu na ubaguzi.
 
Deni la Taifa limefikia wapi?
DSE hali ikoje?
Kwenye mabenki hali ikoje?
Mmejenga viwanda vingapi? Nipe physical address ya vitano tu plz.
Dear Mgibeon nchi yetu iliendeshwa na uchumi hewa. Acha sasa uchumi wa sekta binafsi ujiendeshe wenyewe, ukue wenyewe.
 
Dear Mgibeon nchi yetu iliendeshwa na uchumi hewa. Acha sasa uchumi wa sekta binafsi ujiendeshe wenyewe, ukue wenyewe.
Shida ni kwamba hakuna strategies za kuruhusu huo uchumi, huwezi kumruhusu tu kijana wako aliyemaliza darasa la saba aingie mtaani bila kumuandalia mazingira flani ya kumsaidia IKIWA KWELI unania njema nae!

Kuzipuuza sector binafsi ni kuupuuza kundi kubwa linaloishi kwa kutegemea PP.
 
usiku wkt nasikiliza marudio ya BUNGE TBC TAIFA, nilistuka nilivyosikia mijadala ikiendelea nikahofu labda Mtangazaji alikua aja edit hizo hotuba? Mungu amzidishie nguvu spika mana mjadala wa jana ni sehem ya ahadi yake alivyo sema anatamani avae viatu vya marehem Mzee sita. Hali ya uchumi ni mbaya kiukweli, wabunge mtusaidie kupaza sauti na ALLAH awaongezee ujasir ktk hili.
 
Shida ni kwamba hakuna strategies za kuruhusu huo uchumi, huwezi kumruhusu tu kijana wako aliyemaliza darasa la saba aingie mtaani bila kumuandalia mazingira flani ya kumsaidia IKIWA KWELI unania njema nae!

Kuzipuuza sector binafsi ni kuupuuza kundi kubwa linaloishi kwa kutegemea PP.
Sekta binafsi haijapuunzwa. Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi. Ktk awamu za serikali zilizopita serikali iliibeba sekta binafsi. Wewe hukumbuki kwa mfano hela za serikali banki binafsi ilikuwa asilimia ngapi? Na mabenki hawakuwa wabunifu. Nenda hata DSE, unakuta watu waliiba hela na kwenda kuzificha huko, yaani kwa ufupi tulikuwa na economic uchumi wa puto. Sisi kama watalaamu tunataka kila sekta ijiendeshe yenyewe na siyo kutegemea hela za dili toka serikalini ili ujiendeshe. Na ndiyo maana hao waliohongwa hela kuwasemea hao wapiga dili wajue wanajisumbua kwa sababu serikali inajua kila kitu na ndiyo maana haitateteleka
 
Nimesoma vizuri hakika nimeelewa kwa undani zaidi Mungu wape uwezo wabunge wote wa CCM akili zao zifunguke kama hao ndugu Zetu watatu walivyochangia.
 
Waziri anadhani Mashine za EFD Ndizo zinalipa lodi 'We Need Welfare Economy' Uchumi ambao anomuongezea Mwananchi kipato pia Serikali inatakiwa ilipe madeni ya ndani isiwe km kumkamua Ng'ombe bila malisho
 
Tatizo ni kubwa kuliko Rais na serikali yake wanavyofikiri; jana nimeenda kula chakula mgahawa fulani, jamaa mwenye ule magahawa akawa analalamika anasema alikuwa anauza nyama ya mbuzi wanne kwa siku na kuku zaidi ya 40 lakini hivi sasa hata mbuzi mmoja tu haishi na kuku hawafiki sita kwa siku. Tumekuwa tukisema hapa uchumi wa nchi hujengwa kwa kutumia akili na maarifa makubwa sana.
 
Back
Top Bottom