Tuwafanyeje STARTIMES waache wizi wa local channels

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Huu wizi wa startimes kwa watanzania utaisha lini?

Siku za karibuni walikuja na option ya kubadili kifurushi kwa simu na pia wakaweka vifurushi ya siku week na mwezi

Sasa mimi juzi niliunga cha siku then jana nikabadili nikanunua cha siku kwa kubadili tena

Leo rasmi nimeamua kununua cha mwezi baada ya kuona vya siku na week vinacost sana sasa nikashangaa hawajafungua channels toka asubuh nikaamua kuwapigia walichonijibu ni kuwa

"Mteja haturuhusu mtu kubadili kifurushi zaidi ya mara tatu kwa mwezi hatutaweza kukufungulia channel kwasababu umebadili kifurushi chako mara tatu hivyo inabidi usubiri mpaka mwezi uishe ulipe tena ndo tutakufungulia channel s"

Halafu kuhusu local nikitaka ziwe bure eti nilipe elfu 45 nyingine then watanifungulia hapa sio kweli ndugu zangu wanazifungua baada ya miez 3 zinakata wanakwambia kalipie tena elfu 45

Hivi tcra hawa "wezi" wamewapa nini???

Hivi JMT nzima inawaogopa hawa wachina???

Hawa wachina wana nini mpaka waogopwe??

Nini kipo nyuma ya ajenda?????

Hivi serikali ya hapa kazi tu na tambo zote mmeshindwa kuwashughulikia hawa "wanyonyaji" "mabeberu"??

Nashangaa sana hivi mtu wa huko kijjini mtanzania anayeishi chini ya 1500 kwa siku ataweza kumudu kulipia local channels kwa elfu kumi kwa mwezi???

Wanatumia mitambo yetu kusambaza huduma nchi nzima,

Walipokea ruzuku ya serikali zaidi ya bilioni 3 kufunga minara na kusaidia kueneza digital hapa tz

Halafu nasikia toka 2013 mpaka 2016 hawakuwahi kulipa kodi hata thumni

Juzi juzi ndo wameanza kulipa...

Hivi watz hawa wachina tunawafanyaje???Ni njia gani sahihi ya kuwabana hawa watu waache kwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi yetu?hebu tupeane mawazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vigezo na masharti kuzingatiwa. Inawezekana hayo ndio masharti yao sana sana labda kosa lao ni kutoweka hayo bayana. Na tulio wengi huwa hatuko makini na details. Remember always that... Devil hides in details
 
Mimi na mwaka wa tatu sasa naangalia local channels bure nili zihack

Napata ITV,TBC,EATV,ETV,,STAR TV,CAPITAL,ALJAZEERA,KTN,EMMANUEL TV, NA RADIO KAMA 5 HIVI

TOKA NIMEKINUNUA SIKUWAHI KULIPIA

Sent using Jamii Forums mobile app
hongera sana mkuu, nakupongeza kwa dhati.... nimekuwa nikijaribu kwa muda mrefu ila nashindwa ila soon nitaweza tu
 
hongera sana mkuu, nakupongeza kwa dhati.... nimekuwa nikijaribu kwa muda mrefu ila nashindwa ila soon nitaweza tu
Inaewezekana, fanya hiv search automatic, note zile Code ambazo zinakuwa na signal kubwa na kuleta channels, zinote ,njoo zijaribu kwa manual

Pia uwe unahamisha antena, kama upo dar uwe unaweka 490,ukiipata zitakuja ,baada ya list ya channel zilizopo kwenye kisimbus, ndio utaziona hizo ulizopata kwa kusearch

ubarikiwe mkuu, nitafanya na nikishindwa popote pale nitarudi hapa.... lazima tuwe wazalendo kuhakikisha hatuibiwi na wachina.
 
Inaewezekana, fanya hiv search automatic, note zile Code ambazo zinakuwa na signal kubwa na kuleta channels, zinote ,njoo zijaribu kwa manual

Pia uwe unahamisha antena, kama upo dar uwe unaweka 490,ukiipata zitakuja ,baada ya list ya channel zilizopo kwenye kisimbus, ndio utaziona hizo ulizopata kwa kusearch

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhamisha antenna kivipi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom