Bakhresa Company upande wa television mnatunyanyasa Watanzania kwa vifurushi vya kulipia

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,643
6,822
Naomba niwaulize hivi kifurushi cha 17,000/= ni channel zipi za maana mnazotuuzia? Azam 1, Azam 2, sinema zetu, UTV, MBC Plu Piwer na KIX? Ktk hizi chanel ni ipi mnaona kwamba ni chanel itakayobeba zingine kuendana na thamani ya pesa yetu?

Mmechukua league yetu ila mipira yote mmeweka kwenye kifurushi cha 25,000/= yani Watanzania tusiomudu hichi kifurushi aende mabanda ya kuonyesha mpira. Sio kila Mtanzania ana uwezo wa kulipia hichi kifurushi na mpira ndio burudani yetu tulio wengi.

ZBC 2 walikuwa wanaonyesha michuanobya club bingwa barani Africa ila kwa uchu na tamaa mmeanza kuzihamisha baadhi ya mechi kwenda Azam sport HD ili kutulazimisha tununue kifurushi kikubwa tusichomudu kwa elfu ishirini na tano.

Kwasababu kwa sasa nyinyi ndio kimbilio la wengi basi mnatumia fursa hii kutukandamiza bila kujali hali zetu za kiuchumi kwa Watanzania walio wengi.

Angalieni upya na kufikiria zaidi ni Watanzania wangapi wapenda soka wazalendo mnaowanyima haki ya kufurahia timu zao na familia na badala yake wanaenda vibanda umiza au bar kujichanganya na walevi na wahuni juangalia timu zao.
 
Naomba niwaulize hivi kifurushi cha 17,000/= ni channel zipi za maana mnazotuuzia? Azam 1, Azam 2, sinema zetu, UTV, MBC Plu Piwer na KIX? Ktk hizi chanel ni ipi mnaona kwamba ni chanel itakayobeba zingine kuendana na thamani ya pesa yetu?
nganya na walevi na wahuni juangalia timu zao.
Vizuri gharama mkuu. Hafanyi hisani yuko kutengeneza profit na kuna running costs. Unapewa unacholipia hapo. Kwanza AZAM ni cheap njoo DSTV uone, kifurushi cha 20000+ hakuna hata utakachotazama.
Huwezi lipia bei ya passo ukataka upewe V8 uanze lalamika mbona toyota kwenye passo hakujali sana comfortability.
 
Naomba niwaulize hivi kifurushi cha 17,000/= ni channel zipi za maana mnazotuuzia? Azam 1, Azam 2, sinema zetu, UTV, MBC Plu Piwer na KIX? Ktk hizi chanel ni ipi mnaona kwamba ni chanel itakayobeba zingine kuendana na thamani ya pesa yetu?
banda umiza au bar kujichanganya na walevi na wahuni juangalia timu zao.
Umeona mkuu, hizo coment zote zinaonyesha akili ya mtanzania ilivyo. Kila mtu usiye mjua humu yeye ana hela na atakwambia tafuta hela. Wewe umewasilisha jambo nyet sana kwa maslahi ya watanzania wote wenye uwezo wa chini.

Lakini "matajiri" wachache wanaibuka kubeza na kudhihaki maskini waache kulia lia et watafute hela, real!!. Na wakati mwingine wanaobeza hao utakuta wanaishi kwa mashemeji zao na hawajui hata bei ya kifurushi.

Inasikitisha sana
 
Hakuna mtu mwenye fitna kwenye biashara kama bakhresa halafu akianzisha kitu hataki mpinzani kuna mwekezaji alitaka kuonyesha NBC premier league akamfanyia figisu akaondoka mpira anaonyesha mwenyewe Tanzania nzima pale bandarini kuna kampuni inaitwa zanzibar fast ferries au zanzibar 1 alichowafanyia licha ya huduma zao nzuri kushinda bakhresa ila boti zimebaki mbili tu nyingine zote wameharibu engine ndio maana wameambia ni ngumu tajiri kwenda peponi kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
 
Naomba niwaulize hivi kifurushi cha 17,000/= ni channel zipi za maana mnazotuuzia? Azam 1, Azam 2, sinema zetu, UTV, MBC Plu Piwer na KIX? Ktk hizi chanel ni ipi mnaona kwamba ni chanel itakayobeba zingine kuendana na thamani ya pesa yetu?
angapi wapenda soka wazalendo mnaowanyima haki ya kufurahia timu zao na familia na badala yake wanaenda vibanda umiza au bar kujichanganya na walevi na wahuni juangalia timu zao.
Umeandika kwa uchungu na hisia kali sana!
 
Umeona mkuu, hizo coment zote zinaonyesha akili ya mtanzania ilivyo. Kila mtu usiye mjua humu yeye ana hela na atakwambia tafuta hela. Wewe umewasilisha jambo nyet sana kwa maslahi ya watanzania wote wenye uwezo wa chini.

Lakini "matajiri" wachache wanaibuka kubeza na kudhihaki maskini waache kulia lia et watafute hela, real!!. Na wakati mwingine wanaobeza hao utakuta wanaishi kwa mashemeji zao na hawajui hata bei ya kifurushi.

Inasikitisha sana
Sio suala la gharama, bali watanzania ujamaa umewaharibu. Kama suala la haki za msingi za kupata Habari, si kunachanel za bure amewaachia! Ikiwemo tbc itv na ya mziki eatv na ya wanyama safari tv mnataka nini zaidi? Sula la mpira siku hizi ni suala la ki biashara na meona anatia mabilioni ya pesa mnataka aonyeshe kwa bei rahisi?
 
Hakuna mtu mwenye fitna kwenye biashara kama bakhresa halafu akianzisha kitu hataki mpinzani kuna mwekezaji alitaka kuonyesha NBC premier league akamfanyia figisu akaondoka mpira anaonyesha mwenyewe Tanzania nzima pale bandarini kuna kampuni inaitwa zanzibar fast ferries au zanzibar 1 alichowafanyia licha ya huduma zao nzuri kushinda bakhresa ila boti zimebaki mbili tu nyingine zote wameharibu engine ndio maana wameambia ni ngumu tajiri kwenda peponi kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Mkuu ela sio rahisi km unavowaza....acha kutafuta ili uingie hyo pepo/mbingu.
 
Dstv kifurushi cha 10,000/= nafurahia maisha kuliko huko mnakopigwa kwa kufuata mkumbo,, yani Azam ukitoa ligi yetu ya NBC hakuna chochote mnachotuzidi,,
 
Hakuna mtu mwenye fitna kwenye biashara kama bakhresa halafu akianzisha kitu hataki mpinzani kuna mwekezaji alitaka kuonyesha NBC premier league akamfanyia figisu akaondoka mpira anaonyesha mwenyewe Tanzania nzima pale bandarini kuna kampuni inaitwa zanzibar fast ferries au zanzibar 1 alichowafanyia licha ya huduma zao nzuri kushinda bakhresa ila boti zimebaki mbili tu nyingine zote wameharibu engine ndio maana wameambia ni ngumu tajiri kwenda peponi kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Bro, nikwambie tuu kwenye biashara zote ni lazima fitna ziwepo. Tajiri hawezi kukuchekea na kukubembeleza ili faida upate wewe.

DSTV alitaka kurusha ligi lkn ujinga wake akasema atarusha mechi kubwa tuu simba/Yanga vs team ndogo, TFF wakamkataa mana Azam TV anaonyesha mechi zote hata kama ni JKT vs Mtibwa. Ndio pale Azam akanunua haki za matangazo kwa miaka 10. Kwa hapa bongo kwenye kuonyesha ligi hakuna kampuni itakayoweza kumtoa azam mana hata hivyo Afrika nzima nadhani n nchi nne au tano zinazoonyesha mechi zote za ligi.

Kuhusu meli napo kawaida tuu hizo figisu, ukizembea kidogo tuu lazima upigwe bao. Yn ukifika pale bandarini kwa muonekano tuu lazima ujipeleke mwnyw Azam marine 😂
 
Hakuna mtu mwenye fitna kwenye biashara kama bakhresa halafu akianzisha kitu hataki mpinzani kuna mwekezaji alitaka kuonyesha NBC premier league akamfanyia figisu akaondoka mpira anaonyesha mwenyewe Tanzania nzima pale bandarini kuna kampuni inaitwa zanzibar fast ferries au zanzibar 1 alichowafanyia licha ya huduma zao nzuri kushinda bakhresa ila boti zimebaki mbili tu nyingine zote wameharibu engine ndio maana wameambia ni ngumu tajiri kwenda peponi kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Acha majungu tafuta hela kama mwenzio majungu hayatakusaidia lolote.
 
Back
Top Bottom