Tuwacheni masikhara, ukulima tulio nao bado ni cha mtoto

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
leo nimeguguli na kuangalia huko ulimwenguni kilimo kinavyofanyika, kwa kweli ni hatari, kuna ukilimo wa hali ya kiwango cha juu sana na tutahitaji karne ili kuwafikia na kuufikia ulimaji wa kisasa.

hapa ni kudanganyana tu ,mara madawa,mara mbegu bora, kusema kweli hatuna lolote la maana ni kama tunapigishwa maktaimu na viongozi wa ukulima hapa Tanzania.

1697021764394.png
 
Na kubwa kuliko yote, ikiwa utabahatika kuvuna kwa wingi .kila kitu kitakuozea nyumbani wanunuzi hakuna isipokuwa walaji wapo wengi ,watu walee kodi,mazao yote umeyapata wapi? Na hakuna uwezo wa kuyasafirisha kwenda nchi za ghuba ya uajemi.

Machungwa yanatuozea ,maembe yanachezwa mpira mananasi ya mpingo yanaoza na Serikali inaona lakini haina msaada wowote wa kuwawezesha wananchi kusafirisha nje na kujipatia hela za kigeni.

Na kama atajitokeza mtu kusafirisha vizingiti vinavyowekwa vinamvunja sio moyo hadi miguu. Na niliwahi kusikia usafirishaji wa mazao kutoka nchi kwenda nchi za nje ni lazima kuwepo na makubaliano ya kiserikali sina uhakika kwa hilo.

Niliokuwa na uhakika nalo ukipita na pakacha ya maembe pale uwanja wa ndege basi utazuiwa na kuambiwa unasafirisha hazina ya Taifa, una kibali? Pakacha tu au mahindi. Zenji ukipita na shokishoki 50 tu basi unazuiwa lazima uonyeshe kibali.
 
Nikitaka kujifunza kilimo cha nyanya nipate mavuno kama hayo material yapo huko youtube mtoa mada?
 
Na kubwa kuliko yote ,ikiwa utabahatika kuvuna kwa wingi .kila kitu kitakuozea nyumbani wanunuzi hakuna isipokuwa walaji wapo wengi ,watu walee kodi,mazao yote umeyapata wapi ? Na hakuna uwezo wa kuyasafirisha kwenda nchi za ghuba ya uajemi.

machungwa yanatuozea ,maembe yanachezwa mpira mananasi ya mpingo yanaoza na Serikali inaona lakini haina msaada wowote wa kuwawezesha wananchi kusafirisha nje na kujipatia hela za kigeni.
Na kama atajitokeza mtu kusafirisha vizingiti vinavyowekwa vinamvunja sio moyo hadi miguu.
Na niliwahi kusikia usafirishaji wa mazao kutoka nchi kwenda nchi za nje ni lazima kuwepo na makubaliano ya kiserikali sina uhakika kwa hilo.

Niliokuwa na uhakika nalo ukipita na pakacha ya maembe pale uwanja wa ndege basi utazuiwa na kuambiwa unasafirisha hazina ya Taifa, una kibali ? Pakacha tu au mahindi ,Zenji ukipita na shokishoki 50 tu basi unazuiwa lazima uonyeshe kibali.
Tanga kuna vikundi vya wakulima wa machungwa. Naona vinafanya kazi kwa wakulima kuyakusanya hayo machungwa kwa kikundi chao kisha kikundi klinashughulikia kutafuta soko na vitu kama hivyo.

Nafikiri mfumo wa vikundi unaweza apply kwenye mazao mengi. Kwa uelewa wangu bidhaa zetu hupanda bei ikatokea kuexport kumerahisishwa na kwa kuzingatia bei ilivyopanda nafikiri exportation ina ruhusa sasa hivi.

Shida yetu Tanzania ni bureaucracy, rushwa na incompetent leaders.
 
.

Niliokuwa na uhakika nalo ukipita na pakacha ya maembe pale uwanja wa ndege basi utazuiwa na kuambiwa unasafirisha hazina ya Taifa, una kibali ? Pakacha tu au mahindi ,Zenji ukipita na shokishoki 50 tu basi unazuiwa lazima uonyeshe kibali.

Haaaa! Pakacha la mahindi tu? Lakini kupita uwanja wa ndege na kobe au twiga ruksa...
 
Back
Top Bottom