Mdude Nyagali aweka picha ya Mtoto wa Benjamini Netanyahu ya 2017 na kusema anaagana na Baba yake kwenda vitani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,308
9,737
Ndugu zangu Watanzania,

Sasa ndio nieleweke vizuri napoandika mara nyingi humu jukwaani kuwa Mdude Nyagali hayupo sawa kichwani, ana matatizo kichwani yanayohitaji matibabu ya haraka na dharura. Sasa katika mtandao wake wa Twitter ambao kwa sasa unafahamika kama X Ameweka picha ya mtoto wa Benjamini Netanyau akiwa na Baba yake waliyopiga mwaka 2017 ,na kusema kuwa ni ya mwaka huu akiagana na baba yake kwenda vitani kupigana katika vita inayoendelea kwa sasa, jambo ambalo siyo la kweli na picha hiyo siyo ya mwaka huu.

Picha hiyo ambayo ameweka katika mtandao ilipigwa wakati huo kijana huyo wa Netanyau anatoka jeshini katika mafunzo ambayo wa Israel wote hupitia kwa lazima kama sehemu ya utamaduni wao wa utayari wa kuilinda na kuipigani nchi yao ikitokea vita kama ilivyo sasa. Kwa ufupi ni kama tulivyo na mafunzo ya mujibu wa sheria ambayo hutolewa na JKT kwa vijana mbalimbali kila mwaka kwa hapa kwetu na ambayo siyo sehemu ya ajira bali ni sehemu ya kuwajengea vijana ukakamavu,utayari wa kulipigania Taifa ,uzalendo na kujifunza stadi za maisha na kujitegemea pindi warudipo mitaani kwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

Sasa yeye Mdude akabandika picha hiyo ya muda mrefu na kuleta upotoshaji wake katika karne hii ambayo teknolojia imekua kubwa sana.

Sasa kwa akili yake mbovu na fyatu na iliyokosa muelekeo amejikuta anadanganya habari hiyo kwa kufikiri wote wana akili ndogo kama yake ya kukurupuka na kutofuatilia mambo yanavyokwenda ulimwenguni. Ameweka picha hiyo katika adhima ya kuchafua watoto wa viongozi wetu kwa kusema kuwa wakati mtoto wa Netanyau anaagana na baba yake kwenda vitani watoto wa viongozi hapa nchini wanafanya ufisadi na kugawana fedha za ufisadi.

Hapo ndio muielewe vyema akili ya Mdude kuwa haipo sawa na pia kichwa chake hakipo Timamu.Ni mtu wa mihemuko,kukurupuka, kuropoka na kuongea vitu pasipo kuwa na balansi ya akili na mdomo Wake. Niwaombeni watanzania wenzangu mumpuuze Mdude kwa kutambua kuwa hajitambui na wala hajielewi na ndio maana anafanya hayo afanyayo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sasa ndio nieleweke vizuri napoandika mara nyingi humu jukwaani kuwa Mdude Nyagali hayupo sawa kichwani,ana matatizo kichwani yanayohitaji matibabu ya haraka na dharura. Sasa katika mtandao wake wa Twitter ambao kwa sasa unafahamika..
Uteuzi utausikia kwenye redio ya mbao na midundo ya mende wakivinjari ....Kalime maboga huko Sekenke yanalipa
 
Mm sijaelewa. Unasema!!????
Mdude Nyagali kafanya umma kwa kupost picha Twitter ya Benjamini Netanyau na mtoto wake ya mwaka 2017 wakati mtoto wake anahitimu mafunzo ya jeshi ambayo kwa huku ni kama yale yatolewayo na JKT ambayo tunayaita kwa mujibu wa sheria.sasa katika picha hiyo akadanganya kwa kusema kuwa mtoto wa Netanyau anakwenda kupigana vita inayoendelea hivi sasa dhidi ya kundi la HAMAS.
 
Uteuzi utausikia kwenye redio ya mbao na midundo ya mende wakivinjari ....Kalime maboga huko Sekenke yanalipa
Hapana ndugu yangu mimi sipo hapa kwa ajili ya kutafuta uteuzi bali naandika ukweli ambao siyo wote wanaweza elewa .si unaona Mdude anaandika uongo na kupotosha akijuwa labda wote ni wajinga kama yeye?
 
Hapana ndugu yangu mimi sipo hapa kwa ajili ya kutafuta uteuzi bali naandika ukweli ambao siyo wote wanaweza elewa .si unaona Mdude anaandika uongo na kupotosha akijuwa labda wote ni wajinga kama yeye?
Namba ya simu unaweka kwa madhumuni gani?
 
Basi na wewe kichwani zimeruka, hupo sawa.

Kufustia fact check, picha ni ya mwaka 2014, siyo kama wewe ulivyopotosha hapa kuwa ni ya 2017.

Pili ufahamu kuwa hiyo picha imekuwa ikisambaa kwenye magroup mengi Dumiani, ikiwa imenzia huko Israel. Siyo Mdude aliyeitengeneza au aliyeanza kuisambaza.

Ni fact check ndiyo iliyogundua kuwa picha hiyo ni ya 2014.

Kama ungekuwa na akili timamu, usingemlaumu Mdude, bali walioanzisha. Ndiyo maana tunapoleta habari ambayo hukuishudia wewe mwenyewe, tunaweka source.
 
Back
Top Bottom