Tuuache utamaduni wa kumfanya Marehemu kuwa wa maonesho

Mtu kesha kufa hajui lolote linaloendelea duniani anapataje na kuona heshima unayosema? Hizo ni mbwe mbwe tu za sisi tulio hai kutaka sifa ya msiba mkubwa lakini mwisho wa siku ni kumezwa na ardhi.
Anataka kujifa

Anataka kujifananisha na Mzee Mkapa anadhani ni mtu wa kawaida kama yeye...watu kama Mzee Mkapa hawazaliwi kila siku wala hovyohovyo anaweza kuzaliwa mmoja baada ya miaka kadhaa ....amuache apate heshima yake anayostahili
 
Na wewe ukifa unataka uwekwe uwanja kwa siku ngapi watu wapite kukuangalia, Kumbuka tunaweka kumbukumbu maana utakachosema ndio wosia wako
Ukifa / Ukifariki Wewe huu Ushauri wako tutauzingatia na kuufuata, ila kwa Heshima ya Rais Mzee Mkapa acha aonyeshwe tu.
 
Mnalalamika kila kitu hata kisichowahusu. Upuuzi mtupu. Ukiona kitu au jambo linakukera jua sio saizi yako . waache wanaoaga wafanye yao
 
Wazo zuri, ila hiyo ya kulazimisha watumishi wa umma kwenda kumuaga haijakaa poa. Lengo ni kuhadaa umma kuwa alikuwa anakubalika sana ama nini? Maana wakati wa Nyerere watu walienda kwa wingi kwa ridhaa yao. Sasa hiyo ya kushurutisha watumishi ina maana gani?
Yaaan daaah
 
Hii inatokea kwa wakristo tu,sidhani kwa waislamu kama itatokea.
 
Hizo ndo gharama za kuwa kiongozi wa kitaifa..!
Mda wote unakuwa mali ya Serikali.!
Sidhani kama familia ikikataa hawatasikilizwa. Sio sheria kwamba utafungwa, ni utaratibu tu, ambao walioubuni wanaona ni mzuri, au ndio heshima kwa marehemu.
 
Usisahau watanzania wana tamaduni na dini... kukubaliana kwenye hilo inaweza ikawa ishu
"... kukubaliana kwenye hilo linaweza ikawa ishu."

Tusiogope kuwa ishu, tukidhamiria tutakubaliana na kuwa na utaratibu wa kiTanzania. Sina shaka kabisa juu ya hili.

Tunachohitaji ni kuwepo kwa usimamiza ulio imara katika kulitekeleza jambo kama hili.
 
Mtu kesha kufa hajui lolote linaloendelea duniani anapataje na kuona heshima unayosema? Hizo ni mbwe mbwe tu za sisi tulio hai kutaka sifa ya msiba mkubwa lakini mwisho wa siku ni kumezwa na ardhi.
Anapewa heshima yake hata kama hayupo na huo ndio utofauti wako wewe na yeye
 
Hizo ndo gharama za kuwa kiongozi wa kitaifa..!
Mda wote unakuwa mali ya Serikali.!
Pia unaweza kataa kwa kuacha usia
Kama alivyofanya Rais wa Pili wa Zanzibar Mzee aboud Jumbe Mwinyi.

Aliandika usia wake mwaka 2000 huku aliusia

1.Akifa azikwe kama mtu wa Kawaida
2.Kusiwe na matabaka katika kubeba jeneza lake
3.Asipigiwe Mizinga
4.Jeneza lake lisifunikwe na Bendera ya Taifa
5.Usipigwe wimbo wa Taifa nk

Alifariki mwaka 2016 na serikali ilifuata usia wake
 
Uislam uliyoyaimiza ndiyo aliyoyaimiza Mwenyezi Mungu,Marehemu akifa haagwi,ni watu wachache watakaoenda kumsafisha kumuogesha na kumstiri.hazikwi na jeneza wala nguo,na kaburi lake halijengelewi yaani yafaa lipotee kabisa kusiwepo na kumbukumbu ili watu wasije kuingia kwenye zambi kuanza kumtembelea marehemu
 
Back
Top Bottom