Tuuache utamaduni wa kumfanya Marehemu kuwa wa maonesho

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,303
12,962
Mtu anapo kufa kuna taratibu za kuaga na kuzika kulingana na imani na tamaduni za jamii husika. Kwa waislamu maiti haioneshwi hadharani badala yake ndugu wa karibu tu ndio wanaweza kuiona. Lakini kwa baadhi ya imani na tamaduni ikiwa ni pamoja na serikali, mtu akifa anaagwa kwa kuoneshwa hadharani.

Mimi naona si jambo baya sana kama litafanyika siku anazikwa. Lakini utaratibu wa kumweka marehemu mahali kwa siku zaidi ya tatu au kwenye ukumbi watu wapite kumtazama kuwa ndio kumuaga na kutoa heshima mimi naona siyo mzuri ni wa kumdhalilisha marehemu na kuwatia uchungu zaidi wafiwa bila sababu. Yaani inakuwa kama marehemu amegeuzwa kuwa wa maonesho. Sasa kweli kuweka mwili mahali kwa siku tatu na kuwahimiza watu kwenda kumwangalia ni kwa faida na lengo lipi kama siyo kudhalilisha.

Kanuni za maudhui mitandaoni zinakataza kuonesha picha za marehemu lakini la ajabu serikali ndiyo inampeleka marehemu uwanjani kwa siku tatu aka angaliwe. Najaribu kujiuliza kama ni baba au mama yako amefariki anapelekwa mahali kwa siku kadhaa ili watu wamwangalie! Mimi naomba tuangalie upya utamaduni huu hauna haja wala lazima kufanya hivyo.

Sasa hivi baadhi ya sekta wafanya kazi wanaambiwa lazima wafike uwanja wa taifa kumuaga/kumuona marehemu? Why? Wakati huu wa korona tuna himiza watu kukusanyika kwa maelfu kuaga? Mimi nafikiri waislamu wapo sahihi. Tunajipanga kumwangalia marehemu ili iweje? Picha zake zipo zinatosha. Hata hivyo wengi tuna mfahamu.

Mtu akifa jamani maandalizi ya kumzika yafanyike lakini siyo wa kumfanya wa maonesho hii si haki. Ndugu na jamaa wa karibu tu ndio wahusike inatosha! Samahani kama nitakuwa nimewakwaza lakini sioni maana na umuhimu wa kumweka marehemu mahali kwa siku kadhaa ili watu wamwangalie halafu wakimpiga picha na kumweka mitandaoni mnaanza kuwakamata. It is not fair.

Nakumbuka hata Nyerere aliwekwa uwanja wa uhuru kwa siku kadhaa watu kuaga na wakampiga picha zikaanza kuuzwa mitaani ghafla serikali hiyo hiyo ya marehemu wa sasa ikaanza kupiga marufuku na kukamata wanaouza. Sasa why mlimdisplay publically? Mwekeni mortuary mpaka siku ya kuzikwa akazikwe siyo kumfanya wa maonesho!

RIP Benjamini William Mkapa!
 
Wazo zuri, ila hiyo ya kulazimisha watumishi wa umma kwenda kumuaga haijakaa poa. Lengo ni kuhadaa umma kuwa alikuwa anakubalika sana ama nini? Maana wakati wa Nyerere watu walienda kwa wingi kwa ridhaa yao. Sasa hiyo ya kushurutisha watumishi ina maana gani?
Hivi angekufa kipindi corona ni
Wangemweka hivo au siku ile ile kesho yake kifusi kingemuhusu
 
kama ulizungukwa na fahari zote,na last day uko alone tena lifeless ni kumbusho kwa wanaobaki kwamba ulikuja mtupu na utarudi mtupu

cheo,pesa na hata umaarufu ndivyo waliviheshimu

sote ni mavumbi na mavumbini utarudi
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom