SoC01 Tutokomeze ulawiti kwa watoto

Stories of Change - 2021 Competition

mussaamos

New Member
Jul 15, 2021
4
3
Suala kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile kwa watoto limekuwa likijitokeza Mara kwa Mara hapa nchini. Suala hili linatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kutafutiwa mwarobaini wake mapema.

Chanzo cha tatizo hili:-

(a) Malezi (maadili) mabovu kwa watoto. Nilikuwa nikifanya research kwenye shule moja huko dar es salaam, katika mahojiano na mkuu wa shule alitueleza kisa cha mwanafunzi aliyekuwa darasa la sita, mwanafunzi huyo alikuwa akiwadanganya na kuwachukua watoto wa chekechea, la kwanza, la pili na hata LA tatu na kuwapeleka sehemu ya mafichoni kisha anaanza kuwaingilia kinyume na maumbile kisha anawapa pipi na biscuits ili wasiseme, ilikuwa ni vigumu kumkamata kwani alikuwa anakomea njiani na kuwasubiria watoto hao ila baadae walimpata na kumchukulia hatua.

Binafsi ilinishangaza sana kwa mtoto wa darasa LA sita kufanya ukatili huu, ni dhahiri mtoto huyu hajalelewa vizuri nyumbani na wazazi wake hawafuatilii mienendo ya mtoto wao. Mtoto huyu hata akiwa mkubwa ni ngumu kuiacha tabia yake ya ulawiti.

(b) Utandawazi na kuangalia picha na video za utupu. Mtu atizamapo video na picha za utupu ni lazima hisia zimsisimuke, hivyo wanaolawiti watoto akikosa huduma kwa wakubwa wenzie anaamua kuangukia kwa watoto.

(c) Tamaa za kimwili.

(d) Marafiki na makundi mabaya

(e) Mavazi hasa kwa wanawake yamekuwa yakiwasisimua wanaume wengi na watoto ndio wanakuwa suluhisho LA msisimuo huo.

(f) Msongo wa mawazo ya kingono.

Madhara ya tatizo hili.
(i) Watoto wanaokumbwa na mikasa hii wanaharibiwa ndoto zao.

(ii) Kusababisha msongo wa mawazo kwa watoto na kuwafanya wasijiamini kwenye jamii.

(iii) Kuharibiwa kwa viungo vyao vya mwili (sehemu za siri n.k) mfano mtoto aliyebakwa mkoani Bukoba mkojo ulikuwa haukai kwenye kibofu hivyo ulikuwa unapitiliza kutoka. Alitakiwa kufanyiwa upasuaji kwa gharama nyingi ili angalau kuirudisha hali yake ya zamani.

*Wahusika wengi wa ukatili huu ni wanafamilia na watu wa karibu na familia zetu ambao wanafahamu muda tunaowaacha watoto na mda wa kurudi ndio maana wahusika wengi huwa hawakamatwi kwani mkasa humalizwa kifamilia.

Suluhisho la ukatili huu.

(a) Serikali kwa kushirikiana na asasi za kidini zijikite kuwafundisha watu maadili mema na namna ya kujikinga na tamaa za kimwili.

(b) Serikali itoe elimu kwenye jamii juu ya madhara ya ukatili huu ili watuhumiwa wasifichwe. Pia jamii itoe ushirikiano wa kutosha kwa serikali juu ya kuwaibua wanaofanya ulawiti kwa watoto.

(c) Serikali itunge sheria Kali dhidi ya wanaobainika na makosa haya na kwa wanaobainika kuwaficha watuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

(d) Wazazi wajitahidi kuwalea watoto katika maadili mema na kufuatilia mambo yote wanayofanya shuleni hata nyumbani kwani samaki mkunje aangali mbichi.

(e) Serikali itoe elimu juu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii na utandawazi kwa ujumla.

(f) Serikali itilie maanani katika kupambana na ulawiti kwa watoto na kuweka mikakati madhubuti ya kukomesha ukatili huu.

Tushirikiane kukomesha ulawiti kwa watoto.
#NchiYanguTanzania.AmaniYangu.
 
Back
Top Bottom