Technology
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 769
- 284
The Brain behind the Team anasemaje???
Ukiona hivyo jua Chadema makao makuu huwa hawakurupuki.Mwanzoni nilikuwa na imani na CDM, lakini kwa mwenendo wao naona wananikatisha tamaa.
Hii habari ya muafaka tuliisikia kwenye vyombo vya habari kipindi, na hakuna kiongozi wa juu aliyekanusha. Baada ya muheshimiwa Lema kupinga hadharani ndio tunasikia kauli za viongozi wa juu.!:israel:
Wacheni kuzuga, mtimueni mwenyekiti wenu aliyekaa na Pinda wakakubaliana. Kumbuka, hao madiwani wamechaguliwa na wananchi na si Slaa. Mwenyekiti wenu alichaguliwa na nani kama si kurithishwa kiti na baba mkwe?Kisha kosea step akubali makosa na msiwatupie madiwani, madiwani labda muwape mshiko wa kutosha wakae kimya, mkiwabughudhi watasema ukweli. Msilalamike baada ya hapo. Sasa naamini yule aliesema cdm itakufa kabla 2015. Tunayaona.
Precedence ya maridhiano ipo sasa ilifuatwa? kwa sababu japo issues ni tofauti kwa kiasi nadhani ile ya Arusha ilihitaji zaidi uongozi na ushiriki wa Taifa kuliko ile ya Kigoma.
Pembetatu ya Ushindi isipojengwa jumba huporomoka. Labda tukumbushwe, wakati wa makubaliano ya kuendesha Halmashauri ya Kigoma mjini baada ya uchaguzi wa 2005 uongozi wa Taifa ulikuwa na nafasi gani hadi ikakubaliwa kukawa na zamu za kuongoza? Au ulikuwa ni uamuzi wa local party pale?
Precedence ya maridhiano ipo sasa ilifuatwa? kwa sababu japo issues ni tofauti kwa kiasi nadhani ile ya Arusha ilihitaji zaidi uongozi na ushiriki wa Taifa kuliko ile ya Kigoma.
Ungekuwa na mtazamo mpana labda ndugu yangu ungeona madhara yaliyopo ccm ni makubwa kiasi gani ili tuendelee kuyapiga vita. Hapa ndio tunaona PEOPLE'S POWER wanakuwa kisiasa kwa asilimia kubwa kuliko ccm. Ni mangapi hapa JF mnaomba majibu ccm lakini hamjibiwi mnaambiwa ni siri, uongozi wa chadema msisite kuchukua maamuzi itakapoonekana kuna mazingira ya ushawishi wa rushwa. Kwanza kumbuka siasa au uongozi wowote wa kubebana ni mbaya sana kwa sababu huwezi kumnyoshea mwenzio kidole hata kama atafanya madudu makubwa kiasi gani. Na ndio maana ccm imeshikwa na kigugumizi kupangua maovu yaliyopo kwa sababu kila mmoja anajua madhambi ya mwenzie. Ni afadhali muwe wachache ambao mnaweza kuwa na ushirikiano kuliko kuwa na lundo ambalo halina faida.Natabiri anguko la CHADEMA. Nilikuwepo Marando alipoikaanga NCCR Mageuzi hadi ikaisha, akawaachia kina Mbatia wakikusanya majivu. Nilidhani watu walijifunza, kumbe bado. Kwa heri CHADEMA. Kitakachotokea mkishawafukuza uanachama hao 3, watajiunga CCM na kugombea tena udiwani kwenye uchaguzi wa marudio na watashinda kwa kishindo, kisha Halmashauri inarudi CCM na watu walewale. Najua kuna moto mwingine miongoni mwa wabunge. You were warned.
Dhanna ni haraam.
Faiza naomba elimu yako,