Tutawatimua madiwani - Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutawatimua madiwani - Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngurati, Jun 30, 2011.

 1. n

  ngurati JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kipo tayari kuwapoteza madiwani wake watatu waliohusika kumaliza kinyemela mgogoro wa kumpata meya wa Manispaa ya Jiji la Arusha, kwa maridhiano ya kugawana madaraka.
  CHADEMA imeunda kamati ya watu watatu inayoongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na mwanasheria mkongwe, Mabere Marando, kufanya uchunguzi wa utaratibu uliotumika kufikia maridhiano hayo.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema maridhiano yaliyofanyika kumpata meya na naibu wake hawayatambui kutokana na upungufu uliojitokeza wakati wa mchakato wa kuwapata viongozi hao.
  Madiwani wa CHADEMA wanaodaiwa kukubali kufanya maridhiano ni pamoja n Diwani Estomih Mallah, ambaye atashika nafasi hiyo kuanzia sasa hadi mwaka 2014 atakapomwachia nafasi Diwani wa TLP, Michael Kivuyo, wengine ni John Bayo na Efatha Nanyaro.
  Akifafanua upungufu huo, Dk. Slaa alisema kwanza maridhiano hayo hayakufikiwa na idadi ya wajumbe (madiwani) ambao wanaweza kufanya maamuzi, kwamba maridhiano hayo yalifanywa na wajumbe tisa kati ya 21 ya madiwani wote wa halmashauri hiyo.
  Aliutaja upungufu mwingine kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo alikubali kufanya muafaka bila ya kupata barua ya CHADEMA ya kukubali maridhiano ambayo ina majina ya walioteuliwa na chama hicho kupewa madaraka.
  Aliongeza kuwa madiwani wa CHADEMA, watatu walioshiriki kwenye maamuzi husika walifanya hivyo bila kuwashirikisha viongozi wao wa wilaya, mkoa na makao makuu kwa ajili ya kupata baraka zao za kupendekeza majina ya watakaochaguliwa kuwa viongozi.
  Alisema upungufu mwingine ni kuwapo kwa mianya ya rushwa ya kuwashawishi madiwani husika kushiriki kwenye maridhiano hayo pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa.
  Dk. Slaa alisema kutokana na matatizo hayo, CHADEMA haiyatambui maridhiano hayo na kudai kuwa yamefanywa kwa kupindisha kanuni na taratibu za kuwapata viongozi hao.
  “CHADEMA tunasema kuwa hatuyatambui maridhiano yaliyofikiwa kumpata meya na naibu wake kwani hayakufuata kanuni na taratibu za kuwapata …uliofanyika pale ni uchakachuaji wa demokrasia,” alisema Dk. Slaa.
  Katibu Mkuu huyo alisema chama chake kipo kwa ajili ya kusimamia haki na kwamba kipo tayari kupoteza nafasi ya unaibu meya wa miaka minne aliopewa diwani wake na nafasi nyingine za mwenyekiti wa fedha na elimu.
  “Tunajua kuwa posho ni tamu sana na hili wamekuwa wakilisema madiwani wetu hawa mara kwa mara lakini chama chetu hakiangalii masilahi ya wachache, kipo kwa ajili ya kutetea haki na usawa wa Watanzania,” alisema.
  Dk. Slaa alisema kuwa msingi wa mgogoro huo ulianza tangu Desemba mwaka jana hadi chama chao kuomba maandamano ya amani ambayo yaliingiliwa na poslisi waliowajeruhi na kuwaua baadhi ya walioshiriki.
  Alisema kama madiwani hao waliamua kufanya maamuzi hayo kwa kuangalia posho bila kuangalia msingi wa mgogoro huo, chama chao kinawachukulia hatua baada ya kuthibitisha yaliyotokea katika maridhiano.
  Kiongozi huyo alisema kama chama hicho kila siku kinaikosoa serikali ya CCM na wanachama wake, kipo tayari kufanya maamuzi magumu ya kuwawavua madaraka madiwani wake na kurudia uchaguzi upya.
  Dk. Slaa alisema CHADEMA kama chama kingine, hakina watakatifu hivyo kipo tayari kurudiwa kwa uchaguzi wa baadhi ya kata, kama wananchi wa jiji hilo wanavyotaka, kutokana na mgogoro wa umeya ulivyo.
  Alisema kamati aliyoiunda ambayo ninaongozwa na Marando, itakayofanya kazi kwa siku sita na baadaye kupeleka ripoti yake kwa kamati kuu na vivyo hivyo, viongozi wa wilaya na Mkoa wa Arusha kupeleka ripoti hiyo kwa ajili ya kutoa hukumu ya haki.
  Kabla ya CHADEMA kutoa msimamo wake kama chama, Mwenyekiti wa chama hicho, ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha, Goodbless Lema, walinukuliwa na vyombo vya habari kuwa hawayatambui maridhiano hayo.


  MY TAKE!

  Wale CCM waliokuwa wanatumia nafasi hii kumshataki LEMA kwa wananchi sasa wameumbuka. Lema hakushiriki kuuuafiki muafaka wa arusha na alikuwa bungeni dodoma jamaa wakachukua advantage. However Diwanoi Nanyaro Efatha alishakuja hapa akasema yeye alishiriki kwenye hatua za mwanzo kama mwenyekiti wa BAVICHA mkoa hila hakutilia saini maridhiano ya mwisho na aliyapinga vikali with open eyes. LETS WAIT AND SEE KAMATIO YA MARANDO.*
  Though imani yetu kwa CHADEMA arusha sasa imerudi.
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MI naona CDM wachukue maamuzi magumu tu hamna kingine zaidi ya hapo ni kuwafuta uanachama iwe fuzno kwa wengine na si vinginevyo sioni kama kuna sababu ya kulea upuuzi hapo.
   
 3. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  CCM ni wezi mafisadi na walaghai. Magamba at work. Wamewanunua madiwani wa CDM kwa kuwapa pipi wakizani wamezima moto. Mchezo mbaya sana Nape Nnauye siku tisini zimemshinda wanasaka pakutokea.

  Ikidhibitika hao madiwani wamekula mlungula wanaondoka, tutachagua wengine, waende ccm kwa amani huko rushwa ni sifa na ufisadi ni uraisi.
   
 4. M

  Minze Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hata kama wangelikuwa ni wabunge, so long as wameenda against na msimamo wa chama, lazima wawajibishwe. My advice, kama itakuwa proved madiwani hao walitanguliza maslahi vyeo/fedha mbele, lazima watimuliwe.
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado na Shibuda pia ana lake jambo.
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Lazima kujenga misingi imara inayoheshimu sheria, taratibu na haki, kwa ajili ya ustawi wa chama, utawala, taifa, na wananchi kwa kizazi hiki na kizazi kijacho. Nawapongeza viongozi wa CDM kwa kuliona hili mapema. Mfumo dhabiti huzaa viongozi imara watakaosimamia katiba ya nchi na ya chama bila kuogopa faida za matumbo yao.
   
 7. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anzeni kwa shibuda aliyevunja katiba si tu kuwaonea madiwani ambao wanaonesha kuwa na uchungu wa maendeleo.
   
 8. G

  Galula Jr Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tuanze na Shibuda kabla ya hawa dagaa
   
 9. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Napata shida kushawishika kiasi hicho juu ya undani wa Muafaka huu.Siwezi kuamini kuwa ulifanywa na madiwani watatu tu wa CDM.Hii si kweli,matokeo ya uchaguzi yaliletwa hapa na MwanaJF tena Kada wa CDM mkongwe Crashwise ikionyesha ushiriki wa madiwani wote kwa maana ya kura zilizopigwa.

  Jamani,mgogoro wa Umeya Arusha ulisababishwa na madiwani wote kwa maana ya pande mbili,hatupaswi kuwabana sana Madiwani hawa kwani kimsingi walipaswa wao kuutatua huo mgogoro ama Wananchi waliowachagua.Wengi tunafatilia vyombo vya habari mbona hatujasikia ama kuona maandamano yakifanywa na Wananchi wa Manispaa ya Arusha kupinga muafaka huu.Pia sishawishiki kuwa viongozi wa CDM Taifa na Mkoa walikuwa hawajui suala hili na mwenendo wake.

  Hapa kunatofauti za kimaslahi mbali na Lema kuna baadhi ya Madiwani kama Nanyaro kujifanya hawajui tamati ya suala hili hasa baada ya kukosa walichokuwa wanakitamani kupata (yaani uongozi katika hizo nafasi walizopata akina Mallah na wenzie).

  Nasikitika na huu unafiki katika siasa.

  Wito;Ndugu wana JF tusikubali kushawishika kirahisi katika hili,labda Marando afiche mambo kwa heshima ya Chama lakini ukweli utakuja kujulikana tu.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wacheni kuzuga, mtimueni mwenyekiti wenu aliyekaa na Pinda wakakubaliana. Kumbuka, hao madiwani wamechaguliwa na wananchi na si Slaa. Mwenyekiti wenu alichaguliwa na nani kama si kurithishwa kiti na baba mkwe?Kisha kosea step akubali makosa na msiwatupie madiwani, madiwani labda muwape mshiko wa kutosha wakae kimya, mkiwabughudhi watasema ukweli. Msilalamike baada ya hapo. Sasa naamini yule aliesema cdm itakufa kabla 2015. Tunayaona.
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Chadema mnatia aibu sasa!

  Huyu bwana Slaa siku zote hakujua kuwa kuna mwafaka kule Arusha? Nilitegemea siku ile ile ambayo magazeti yaliandika angejitokeza kukanusha habari.

  Kwanza jambo kubwa kama hilo linatokea Suongozi wa Chadema haujui?? au ni magirini tu waliwatoa wenzao kafara wao waonekane ndio wema??

  Acheni aliflela ulela viongozi wa chadema , mkumbuke ya kuwa huko Arusha watu wamepoteza maisha yao kuwaunga mkono hao madiwani mnaotaka kuwatimua na si kumuunga mkono Slaa wala Mbowe!!!
   
 12. k

  kayumba JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yangu macho!
   
 13. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Natabiri anguko la CHADEMA. Nilikuwepo Marando alipoikaanga NCCR Mageuzi hadi ikaisha, akawaachia kina Mbatia wakikusanya majivu. Nilidhani watu walijifunza, kumbe bado. Kwa heri CHADEMA. Kitakachotokea mkishawafukuza uanachama hao 3, watajiunga CCM na kugombea tena udiwani kwenye uchaguzi wa marudio na watashinda kwa kishindo, kisha Halmashauri inarudi CCM na watu walewale. Najua kuna moto mwingine miongoni mwa wabunge. You were warned.
   
 14. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  da siasa za maji taka bwana hapa ndio nakosa kabsaaa kuwaamini wanasiasa, sirini na mioyoni wananena vingine hadharani wanasema vingine.
  bora lema na zito wako wazi,
  inaboa mpaka basi
   
 15. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  ni somo tumejifunza. habari hii ililetwa hapa na vijana wa nape kuwa mwafaka umefikiwa na eti wakaimba SOLIDARITY FOREVER....kumbe chama hakijahusika na mwafaka.....

  tujifunze sasa kuwa makini na info sensitive zinazokuja hapa....

  ni angalizo pia kuwa kila info inayokuja ifanyiwe kazi kabla ya kupelekwa mbele ya kanuni.....

  faizafoxy wewe mzuri lakini!!! halafu ni black beauty!
   
 16. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  oya kapige mswaki, domo ako linanuka
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Ingekuwa hawajakutana Mbowe na Pinda cdm wangepinga na ccm wangepinga kukanusha hizo habari. Hakuna binaadam alie mbaya. Wadhungu hunena "beauty is in the eyes of the beholder".
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ngurati,


  Ungeweza tu kuleta hiyo taarifa ya Katibu mkuu.Hayo mengine sijui my take ungeacha Ripoti ya Marando ikaja kutoka Arusha.

  Mashabiki wa CCM na wengineo nanyi kuweni na subira,kwanza CCM ndiyo chanzo cha hayo yote
   
 19. n

  ngurati JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Saanane Ben,

  Nadhanoi hujaisoma vizuri opinion yangu , tena nikaibold with capital letters, this is what i said as a conclussion to my take...."LETS WAIT AND SEE KAMATI YA MARANDO ITAKUJA NA NINI"
   
 20. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nilimaanisha hiii hapo kwenye Blue.was that really necessary? Au sio wewe umesema mkuu?Anyways,tuendelee na mjadala.........


   
Loading...