Tutawaachia nini wanaotufuata? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutawaachia nini wanaotufuata?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fundi Mchundo, Oct 18, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tutabaki na nini? Hivi hao watalii tunaotegemea kukaa kwenye hiyo Hoteli Sunrise watatoka wapi baada ya sisi kubomoa majengo yote ya kale?

  Mji wa Dar es Salaam unasikitisha kwa kasi ya kubomea majengo ya zamani na kujenga maghorofa bila kuangalia infrastructure iliyokuwepo!

  Lesser Flamingoes tunawapigia hesabu ya kuwamaliza kwa ajili ya virupia kutoka kiwanda tutakachojenga Lake Natron.

  Serengeti tunajenga mahoteli na kiwanja cha ndege kuhudumia watalii watakaokuja kuangalia wanyama ambao hayo maendeleo ndiyo kiama chao!

  Kweli tunajiuliza hao watoto na wajukuu wetu tutawaachia nini?

  Mungu inusuru nchi yetu.
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Fundi Mchundo,

  Hivi haya majengo si yalikuwa yamependekezwa na UNESCo kuwa yaachwe kama vitu vya kale na kihistoria? Kwa nini tumekimbilia kubomoa kumbukumbu nzuri kama hiyo? Mwandosya yuko wapi ambaye ni waziri wa Mazingira au yule wa Utamaduni?

  Kwa nini tunakimbilia kufanya vitu kiholela tuu?

  Kwa nini wasipeleke hawa wawekezaji kule Uswekeni ili maisha Bora yaanze kuwafikia Watanzania kama huyu Mwekezaji atajenga barabara na kuhakikisha kuna maji kufika hotelini kwake?

  Ama kweli tunagidiwa kama mabwege!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nilishangaa sana niliposikia kuwa hayo majengo yanabomolewa. Mimi nilidhani kuwa kwa kuwa kuna maeneo mengi tu ya kujenga hoteli za kitalii, ingekuwa vema iwapo majengo haya ya kale yangewekwa katika hali nhzuri, ili watalii waje kuyaangalia na haapo hizo hoteli zinazojengwa zingepata wateja. Sasa ukibomoa vivutio vya kihistoria, watalii watakuwa kuanghalia nini?
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tunauongozi ambao ni dhaifu na unaofanya maamuzi kwa niaba ya wengi ili kujinufaisha.
  Once we preserve the oldies we have history can be easily passed from a generation to another.But the government is not aware nor does it care.
  Ningeomba kuuliza,Ina maana kwenye hii nchi hatuna mamlaka husika inayohusiana na vito vya kale?na kama ipo hawa watu ni wa kuhoji maana am sure they also have a hand in all these!
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Itakuwa vigumu sana kupata, na inawezekana kamwe hatutapata, majibu ya maswali haya kama hamna vyombo vya habari kwa kusaidia kufikisha mambo haya kwa wanaotakiwa kuyajibu. Hatuna press!!!

  Habari inasema "Jengo la kale Bagamoyo nusura limmalize Mchina" lakini kumbe ni watu kibao wamejeruhiwa. Mwandishi kaona Mchina tu!! Hii ni mbaya kuliko "Mtu mmoja na Wamakonde wanne wapata ajali," manake angalau katika ile classic epic, Wamakonde - japo wao sio watu - walikuwa recognized katika kichwa cha habari.

  Na hata kama ingekuwa ni huyu Bw. Tai Yang peke yake ndio kaumia, hutakiwi kusema "Mchina" kaumia. Kabila/rangi/Utaifa wa majeruhi unatajwa kama tu unahusiki moja kwa moja na nyeti za habari. Kitu kimoja nimejifunza katika world class press ni kwamba the only time unaweza kuandika kitu kama "aliyesababisha ajali ni African American" ni kama labda dereva mmoja alikuwa ni African American ambae kakimbia eneo la ajali, hivyo anatajwa alivyo kwa sababu anatafutwa. Vinginevyo ukitaja race ya mtu bila sababu noma!!!!

  Na nigekuwa mimi mwandishi ningembana mbavu (ningejitahidi nisimbane koo ) huyu daktari aliyehitimisha kwamba wagonjwa wake wamejeruhiwa kwa sababu hawakuwa waangalifu. Umesikia wapi emergency room doctor anatibu huku anatoa public statements kuhusu uzembe wa wagonjwa kuhusiana na construction site safety ??? Yeye daktari alitembelea construction site kabla ya ajali na kugundua hatari ? Serikali ilikuwa wapi ? Au kama alikuwa anapita tu njiani akaliona hili, kwa nini alienda ku complain kwa "Mchina" tu na sio kuliwakilisha hili kwa wahusika Serikalini ?

  Hayo yote ni sehemu ya uvunjaji wa hili jengo na ajali hii. Lakini ukisoma habari kwenye gazeti letu lolote unaondoka na maswali tu, binafsi huwa najisikia nimeondoka mjinga kuliko nilivyokuja, maana gazeti lina ku treat kama mjinga. Nahakika inaweza kuchukuliwa kama nimeruka nje ya mada ya uvunjaji majengo ya Kihistoria, lakini kuna siku watu wataona kwamba the press is the weakest link katika mnyonyoro wa kuvuta gurudumu la maendeleo maana haitusaidii kujua yanaondelea. Huwezi kuendelea kama hujui kinachoendelea.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kuhani,
  'We need people like you in the editing room. Have you ever thought about going into journalism?
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145


  Mimi niliamini kuwa kwa sababu Rais wetu anatoka Bagamoyo basi huo mji utapata afueni! Kumbe ndiyo imekuwa kinyume. Miradi ya bandari, air-port, prawn fishing yote itaupeleka mji huo kuzimuni! Bora waende wakaupige picha na kutangaza kuwa ruksa kubomoa na kujenga kwenye mji mkongwe.

  Hao mawaziri wapo tuu. Sidhani kama wana uchungu wowote na mazingira. Ingekuwa hivyo tungewasikia wakipinga kubomolewa kwa majengo Darisalama. Lakini wapi!

  Naona hata Mkurugenzi wa Mambo ya Kale amenyanyua mikono!

  Iko kazi.

  Amandla................
   
Loading...