Tutarajie kumuona Professa Kabudi akigombea ubunge 2020 ili kujiimarisha rasmi kama mwanasiasa au akirudi kushika chaki?

thA goD

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
1,941
1,844
Mwanasheria Msomi vs Mwanasheria Msomi na Mwanasiasa.

Sasa ni Tundu Antipas Lissu dhidi ya Profesa Paramaganda Kabudi katika ulingo wa siasa za kimataifa.
Tundu Lissu ni mwanasheria nguli ni wakili msomi ambaye nusu ya maisha yake hadi hii leo ameyatumia kusimama mahakamani akijenga hoja mbele ya majaji na mahakimu, akinukuu vifungu mbalimbali vya sheria na katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katiba mbalimbali. Tundu Lissu akiwa wakili msomi asiyekubali kushindwa kwa hoja mahakamani akiongozwa na dhamira hii imempelekea kuwa si tu mwanasheria au wakili msomi Bali Albert Einstein ama Shaaban Robert wa sheria anayebisha aseme.

Ninapomtizama Tundu Lissu napata picha ya kijana wakili enzi zake akianza kazi hii ya kusimamia haki ashakumsi matusi kazi ya kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo, akikesha na makabrasha ya vitabu, ripoti, katiba na nyaraka mbalimbali za kisheria, rejea za kesi za zamani n.k ili kumshinda opponent wake siku inayofuata, ili kuhakikisha mteja wake anapata haki yake.

Nusu ya pili ya maisha ya Tundu Lissu ilianza katika siasa na ishallah itamalizikia katika siasa. Tundu Lissu aliingia katika ulingo wa siasa akiwa mwanasheria nguli kama Andrew Chege Einstein mwingine wa sheria hapa bongo. Wakati Andrew Chenge (makengeza) akiingia katika siasa kupitia CCM, Tundu Lissu aliingia katika siasa kupitia jukwaa la upinzani, jukwaa la hoja mbadala akiianza kujaribu bahati yake kupitia NCCR Mageuzi mwaka 1995 kura hazikutosha kisha hapo baadae akaingia bungeni kwa tiketi ya Chadema Mwaka 2010.

Utamchukia kwa hoja zake utampenda pia kwa hoja zake. Tokea alipoingia bungeni uwanja wa sheria umekuwa ni wake, sisemi hivi kuwabeza wabunge wengine wanasheria na wanaojenga hoja kwa sheria. Tundu Lissu ameacha alama kama mbunge anayehubiri vyema somo la sheria, anayeihimiza serikali, bunge mahakama na vyombo vingine kuzingatia sheria na katiba ya nchi. Huku wabunge wengine wakizizika taaluma zao wanapojenga hoja mara zote Tundu Lissu amesimama akitetea na kujenga hoja kupitia taaluma yake ya sheria. Tundu Lissu ameonja machungu mengi na matamu machache ya siasa za upinzani hapa Tanzania. Hata kilichomfikisha Ubelgiji baada ya tukio la kupigwa risasi ni machungu siasa za upinzani hapa Tanzania.
Nyuma ya pazia wanasheria, majaji, waandishi wa habari walimtambua Tundu Lissu kama mwanasheria Nguli, mpambanaji, mwanaharakati. Baada ya kuingia katika siasa tumemtambua Tundu Lissu kama Mwanasiasa, mwanasheria, wakili msomi, mwanaharakati, mtu jasiri sana ambaye kadri siku zinavyoenda Tanzania inazidi kuuona umuhimu wake na kumhitaji zaidi.

Kwa upande mwingine Profesa Paramaganda Kabudi ni mwanasheria msomi (PhD holder) ambaye muda wake mwingi ameutumia kama mhadhiri akifundisha na kutahini wanasheria pale Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Bila shaka ni wakili pia kwa maana ya kumiliki vibali vinavyomruhusu kusimama mahakamani kama wakili na kama kamishna wa viapo. Lakini sina hakika sana kama Profesa Kabuni amesimama sana mahakamani bila shaka muda wake mwingi ameutumia kuandaa wanasheria na kutoa ushauri wa kisheria. Kwahiyo hapa tunamuona Wakili Tundu Lissu akitumia muda wake mwingi katika viunga vya mahakama na Professa Paramaganda Kabudi akitumia muda wake mwingi kufanya tafiti (researches), kuandaa lectures, handouts, tutorials na kadhalika kwa ajili ya wanafunzi.

Profesa Paramagundi si mwanasiasa, hakuwahi kuwa mwanasiasa na mpaka sasa si mwanasiasa ingawa yuko katika ulingo wa siasa akipambana na wanasiasa aina Tundu Lissu ambao wanaitumia sheria kama silaha kuu ya mapambano. Professa Paramaganda Kabudi alijizolea umaarufu kupitia tume ya Jaji Warioba ambayo ilifanya kazi ya kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni juu ya katiba mpya, kuyachakata na kutuletea rasimu bora kabisa ya katiba mpya. Uwepo wake katika tume na umahiri wake katika sheria ulikuwa na mchango Mkubwa uliopelekea kupatikana kwa rasimu hii bora. Hapa Professa Paramaganda Kabudi alikuwa ni msomi mbobezi wa masuala ya sheria akifanya kazi ya taaluma yake na kutuletea rasimu bora kabisa. Baada ya hapo jicho la John Magufuli likamuona na kumteua kama mbunge na kisha kupewa uwaziri wa sheria. Bila shaka lolote naamini ulikuwa ni uteuzi bora ukizinga taaluma, weledi na wasifu wa Professa Kabudi. Akiongozwa na dhamira ya kizalendo Professa Kabudi aliupokea kwa mikono miwili uteuzi huu na kuanza kuufanyia kazi. Hata hivyo naamini hakuacha kuendelea kujichukulia kama msomi anayetekeleza majukumu kiserikali kupitia nafasi ya kisiasa. Hata baada ya uteuzi hakujidhihirisha kuwa ni mwanasiasa kama mwezake Professa Kitila Mkumbo ambaye alikwisha jidhihirisha kuwa ni mwanasiasa kupitia Chadema, ACT Wazalendo na mara baadaye kuuvaa ukada wa CCM baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya maji. Kutokea hapo hoja zake zilizidi kuwa za kisiasa zaidi, kipropaganda zaidi kulikoni kuwa za kisomi zaidi.

Professa Kabudi akiwa mwanasheria katika wizara ya sheria aliendelea kupata nafasi ya kujibu hoja zake kisomi huku akiitetea na kuilinda serikali. Kuna muda alitoa lecture bungeni. Alifanya yote haya akijidhirisha kuwa ni msomi ambaye yupo tu katika siasa kwa sababu ya waliomhitaji kumpa nafasi hii adhimu ili aokoe jahazi. Sasa imefika muda wanataka kumtumia kisiasa afanye kazi ya siasa kwa sababu inaonekana wazi huko ughaibuni Einstein wa sheria anakichafua. Nimeshuhudia wanasiasa na watu mbalimbali wakijaribu kupambana na Tundu Lissu kuanzia enzi za bunge la Anne Makinda hadi hii ilipoibuka (misunderstanding) ikiwa kuikosoa serikali, Rais na viongozi wengine wa serikali ni kukosa uzalendo kwa nchi yako.Wengi niliowashuhudia wakibattle na Einstein wa Sheria Tundu Lissu wameishia kujipaka oil chafu. Mara nyingi ukimkosoa Tundu Lissu atakuaibisha kwa hoja. Professa Paramaganda Kabudi vs Tundu Lissu mchuano ni mkali. Je,Tutarajie kumuona Professa Kabudi akijidhihirisha sasa kama mwanasiasa kamili akiuweka kando usomi na kupangua hoja za Tundu Lissu?

Tutarajie kumuona Professa Kabudi akigombea ubunge 2020 ili kujiimarisha rasmi kama mwanasiasa au akirudi kushika chaki? Kwa sasa namchukulia Professa Paramaganda Kabudi kama Generali mtiifu kwa kamanda wake ambaye amepewa order ya kupeleka askari katika uwanja wa medani kwenda kumshambulia adui. Generali anafuata order lakini mbinu na mikakati ya kivita viko chini yake.Taarifa inayotakiwa kurudi kwa kamanda wake ni taarifa ya ushindi au taarifa ya kushindwa na kisha asubiri adhabu yake. Je atashinda, je atashindwa. Je akishindwa itakuwaje, Je akiadhibiwa plan B yake itakuwaje?Mwanadada nguli wa mziki wa injili Bahati Bukuku aliwahi kuimba....."Maamuzi yako, matokeo ya kesho......amua vema upate mema....wewee...".
Ni hayo tu, tusubiri mtanange.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi ukimkosoa Tundu Lissu atakuaibisha kwa hoja. Professa Paramaganda Kabudi vs Tundu Lissu mchuano ni mkali. Je,Tutarajie kumuona Professa Kabudi akijidhihirisha sasa kama mwanasiasa kamili akiuweka kando usomi na kupangua hoja za Tundu Lissu?
Kabudi ameshapata kichapo cha tofauti ya Nchi na Serikali. Serikali lazima kuichukia, kuikosoa , kuibeza kama inakiuka Katiba, sheria, haki za binadamu etc. The serikali should be denounced as the katiba warrants us to do!
 
Kwani braza, Lissu kaongea tena baada ya upasuaji huu wa hivi karibuni?
 
Kabudi ameshapata kichapo cha tofauti ya Nchi na Serikali. Serikali lazima kuichukia, kuikosoa , kuibeza kama inakiuka Katiba, sheria, haki za binadamu etc. The serikali should be denounced as the katiba warrants us to do!
Asshole comment!
 
Back
Top Bottom