Tutaponea wapi sisi Watanzania baada ya Serikali kututupa mkono? Airtel nao washusha kiwango cha Data

...mkuu mie natumia halotel, gb 1 kwa sh 1,000/ kwa wiki. Zamani mpaka mwaka jana November-December, speed ilikuwa nzuri sanaaa na hakukuwa na kukatika katika kwa mtandao..Lakini baada ya hapo, inakata sanaaaaa

Halotel kasi ya internet imepungua.
 
zantel wankupa dk 20 sms 100 Gb 1= siku 30 kwa 1000
afu kwa 2000 ni mara mbili ya hapo na 5000 wanatoa gb 5 kwa mwezi.
uko ndo kwa kukimbilia...
Aisee sijui nitafute line ya zantel
Maana Tigo ni utopolo tu, yaani napata 1 GB KWA tsh 10,000 Kwa mwezi
 
zantel wankupa dk 20 sms 100 Gb 1= siku 30 kwa 1000
afu kwa 2000 ni mara mbili ya hapo na 5000 wanatoa gb 5 kwa mwezi.
uko ndo kwa kukimbilia...
Huu mtandao si nilisikia Tigo ndio wanaumiliki siku izi?

Anyways, alianza mmoja wengine wanafuata tulia tu......
 
Nilimsikiliza bashungwa kwenye kipindi cha power breakfast (clouds fm) aliulizwa hili swali akasema mwisho wa mwezi huu kuna chamaana watakifanya kuhusu mambo ya bando ila kwa mwendo huuu inakatisha tamaaaa
 
Nilikuwa nanunua jimixie bando GB tatu kwa buku 3 leo nimekuta buku 3 ni GB moja nimwumia sana
 
Mimi natumia Airtel uwa najiunga vifurushi vya wiki au mwez Jana nashangaa naenda jiunga nakuta kifurushi Cha 20000 unapata gb 11 sikuamini macho yangu.
Nasubiri star link ifike afrika tuhamie huko maana internet ni 100$ mwez mzima speed ya kufa mtu mpaka mb 50/sec ping 52 milliseconds

Zuku fiber naskia wapo fresh au ni uzushi?
 
Bado sijaona mtandao nafuu hapa bongo kuliko Airtel.

Ona kifurushi chao cha buku 1000 hicho.

Una Dak 100 za kupiga simu Airtel,Dak 10 kwenda mitandao yote,SMS 1000 na 1GB hadi 14-02-2021 18:22:15.Kujua salio piga *149*81#
Jaribu leo ulete mrejesho kama bado iko hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom