Kisali.TechnitianJr.
JF-Expert Member
- Nov 2, 2012
- 592
- 183
Kuna watu wamezaliwa na tabia ambazo kwa ulimwengu wa leo watapata shida sana
Hapa nawazungumzia wale ambao wamezaliwa huku wakiwa hawawezi kabisa ku-cheat lakini wakati huohuo hawawezi kuhimili mwenza wao kuwasaliti
Hili ni suala gumu sana
Binafsi nilishawahi kujaribu kulifikiria hili nikajikuta nashindwa kabisa,siwezi kutofautisha kumdharau mpenzi wangu na kum-cheat
Yaani siwezi kum-cheat halafu niendelee kujidai eti nampenda
Ni ngumu
Nahisi kujidhalilisha na zaidi sana namdhalilisha mwenza wangu
Nahisi maisha yatakuwa magumu sana kwenye dunia hii ya "cheating is inevitable"
Nawaona wake za watu mitaani wanavypishana kwenye nyumba za wenyeji[sio wageni]
Najaribu kuvivaa viatu vya waume zao nahisi uchungu sana
Na hata wale wenzangu wenye mtazamo huu nawaambieni tutaipata tu kwenye maisha haya
Au tuamue kuachana kabisa na hii kitu?
Tutaoa kweli?
Mimi nimeamua tu kubaki naangalia kwanza!
Maisha ya kuigiza ni magumu sana!
We apa kutogusa jiko la mtu ili atakayegusa lako na kukamatwa umfanye jambo ambalo litawaweka wengine mbali na jiko lako
Au na sisi tuzoee tu?
hapana mkuu wala hata tusijaribu kwani hayo si maisha ndugu yangu,you dont get a thing,after all kama si tabia yako huwezi na siku ukilazimisha tu utaitesa dhamiri yako mpaka basi.
ndo hapo sasa mkuu utaitesa dhamiri yako sana mkuu,kwa hiyo ni bora kujiweka pembeni kabisa,kuwaacha ambao kwao kucheat ni kama maji.Ilishanishinda hiyo
Ki ukweli siwezi kabisa ku-cheat!
Unadhani inaweza kuondoka kwa kukemewa tu?
Kuna dini inawaadhibu watu wa aina hii kwa kuwapiga kwa mawe hadi kufa lakini hawaachi
Unadhani kukemewa tu inatosha?
Looh! Mimi kwa kuiba vya wenzangu mmm, Kucheat naona powa tu. Ila wakwangu never kuibiwa na nikihisi nimeibiwa aloo!! naumia halafu nakuwa na hasira mbaya.
Meaning what?
Kukaa pembeni kwa maana kuachana ma mahusiano au?
Looh! Mimi kwa kuiba vya wenzangu mmm, Kucheat naona powa tu. Ila wakwangu never kuibiwa na nikihisi nimeibiwa aloo!! naumia halafu nakuwa na hasira mbaya.
hapna maana yangu ni kuwa kuakaa pembeni na hiyo cheating,wanaoona kucheat kuwa ni jambo la kawaida waendelee na sisi tunaojionea shida tukae pembeni tunawaangalia tuone mwisho wake ni nini.
Mkuu
Hii siamini kama ni kweli
Sidhani kama kuna mahali hiyo iliwahi kuwezekana!