Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,884
35,901
Hii ni orodha fupi ya wenye ujasili wa kumkabili CCM. Kama hauko humo kuwa tayari kujiunga na CCM. Hao ni wenzako hujijui tu:

1. Wanaompinga Israel na udhwalimu wake Gaza.
2. Wanaowaunga mkono wapalestina dhidi ya uvamizi wa Israel.
3. Wanaotambua kuwa vita vya wapalestina ni vya ukombozi.
4. Wanaotambua kuwa vita vya Israel ni vya uvamizi.
5. Wanaotambua vita vya Urusi huko Ukraine ni uvamizi.
6. Wanaotambua vita vya Ukraine dhidi ya Urusi huko Ukraine ni vya ukombozi.

Pia kama uko humo na uko CCM ondoka tu huko, hakukufai.

Suala la haki za watu haliwezi kuwa la kishabiki kama wa Simba na Yanga. Suala la haki za watu haliwezi kuwa la kufanyia mzaha, kupigia kamali au ku bet.

Kuuachia undumila kuwili wenye kutufananisha na popo kuwa karibu nasi, ndilo kosa letu kuu kwenye harakati za ukombozi. Kuwa tunawaendekeza watu wasiojua wanachopigania au hata wanachotaka. Hatari zaidi wanapokuwa kwenye usukani.

"Vipi wasiojua wanachopigania watakuwa na wito kamili kwenye shughuli?"

Wasiofuzu kuwemo kwenye listi ya mapambano wajitathmini na kupisha wenyewe kabla ya kuwafurusha bila kujali nafasi zao.

Shughuli ya kupambana na CCM Inahitaji zaidi mno.ya idadi ya watu. Ni Heri kuwa na watu wachache kuliko kuwa na watu mizigo.

Post #2 imejielekeza wakati nyuzi 2 hizi zinahusika:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Undumila kuwili wa wamaagharibi mgogoro Gaza, Putin Dume!
 
IMG_20231015_072729.jpg

IMG_20220927_190940_421.jpg
 
Hamas wanabaraka za Palestine, katika uovu wao, Hamas wameua watu waliokuwa kwenye festival Israel, wakaona poa, ajabu wao wakibondwa wanapiga kelele wanaonewa ajabu sana hii, Jana wenzao(Islamic jihad) wamerusha kombora kimakosa likaangukia hospital, that's mean they bomb themselves, mistakenly, they claim Israel does!, dunia inapata wakati mgumu mno kwa sababu chanzo cha uchokozi ni Hamas, son of Palestine.
 
HAMAS wanapambana na mvamizi. Vita vyao ni vya ukombozi kama Mau Mau, ANC, MPLA, FRELIMO au ZANU PF.

Dunia inapita wakati mgumu sana chanzo uvamizi wa Israel.
 
HAMAS wanapambana na mvamizi. Vita vyao ni vya ukombozi kama Mau Mau, ANC, MPLA, FRELIMO au ZANU PF.

Dunia inapata wakati mgumu sana chanzo uvamizi wa Israel.
Hapa duniani mtu akishakaa mahala kwa zaidi ya miaka 50,hapo ni nyumbani kwake, na ndio maana wachaga ni waethiopia, wangoni ni Jamii za kusini mwa Afrika, Palestine must accept this, na wabakie na kipande Chao in peace.
 
Yaani kukubali kuibiwa siyo?

Kwa hiyo CCM keshakaa miaka 62 hamna haja ya kurumbana naye siyo?

Hakika uko kwenye mada mkuu. Bakia huko huko. Wewe ni mwenzao.
 
HAMAS wanapambana na mvamizi. Vita vyao ni vya ukombozi kama Mau Mau, ANC, MPLA, FRELIMO au ZANU PF.

Dunia inapata wakati mgumu sana chanzo uvamizi wa Israel.
Hao Hamas ni chama gani cha siasa uko pelestine?.Ni ukombozi gani unaofanywa na kikundi cha watu wanaojiendesha kama magaidi.Wangekua na akili na nia yakujikomboa walitakiwa wajiimarishe wawe sehemu ya serikali ya palestine ili wawe na nguvu yakupeleka agenda yao kwa umoja kupitia serikali inayotambulika.Kwa mtindo wanaotumia hakuna namna utakayomwambia mtu anayejielewa kua wanafanya kwa ajili ya ukombozi.Kwasababu kama ni ukombozi walitakiwa wawe wameshajikomboa kwasababu huu mgogoro wa hawa ndugu niwa miaka mingi sana.Isitoshe palikua pametulia kwa upuuzi wao wameanzisha tena mgogoro kwakijinga utakaowamaliza na kuharibu kila kitu walichokijenga kwa miaka mingi.Kwa kifupi ni kwamba hao watu hawataki kuona wanaishi kwa amani.
 
Una maana waliokufa vita vya SWAPO, ANC, FRELIMO, MPLA nk? Au wanaouwawa na Israel? Kwa hakika hawana hatia. Mwenye hatia ni mvamizi.
Kama Hamas wangeshambulia wanajeshi, vituo vya kijeshi dunia nzima ingetambua wanapambana dhidi ya uovu lakini kushambulia na kuteka watu wasio na hatia pia wameua raia wa nchi nyingine huo ni ugaidi.
 
Hao Hamas ni chama gani cha siasa uko pelestine?.Ni ukombozi gani unaofanywa na kikundi cha watu wanaojiendesha kama magaidi.Wangekua na akili na nia yakujikomboa walitakiwa wajiimarishe wawe sehemu ya serikali ya palestine ili wawe na nguvu yakupeleka agenda yao kwa umoja kupitia serikali inayotambulika.Kwa mtindo wanaotumia hakuna namna utakayomwambia mtu anayejielewa kua wanafanya kwa ajili ya ukombozi.Kwasababu kama ni ukombozi walitakiwa wawe wameshajikomboa kwasababu huu mgogoro wa hawa ndugu niwa miaka mingi sana.Isitoshe palikua pametulia kwa upuuzi wao wameanzisha tena mgogoro kwakijinga utakaowamaliza na kuharibu kila kitu walichokijenga kwa miaka mingi.Kwa kifupi ni kwamba hao watu hawataki kuona wanaishi kwa amani.

Hujui kuwa HAMAS ndiyo serikali yenye mamlaka Gaza? Hujui kuwa HAMAS ni sehemu ya utawala wa Palestina? Kama hayo hujui huoni unasema usiyoyajua?

Unajua kuwa ANC, SWAPO, FRELIMO, MPLA, na hata kina Mandela waliitwa magaidi?

Tofautisha wapigania uhuru na magaidi. HAMAS ni wapigania uhuru.
 
Kama Hamas wangeshambulia wanajeshi, vituo vya kijeshi dunia nzima ingetambua wanapambana dhidi ya uovu lakini kushambulia na kuteka watu wasio na hatia pia wameua raia wa nchi nyingine huo ni ugaidi.

Israel amekuwa anashambulia raia siku zote na hata hIvi sasa Gaza.

Muhimu kutambua wavamizi ni wavamizi tu iwe ni jeshi au wakazi kwenye maeneo yaliyovamiwa (settlers).

Settlers si raia. Settlers ni shabaha sahihi. Hao ni adui.
 
Historia inathibitisha kuwa kabila 12 za wana wa Israeli waliondolewa katika ardhi ya babu zao mwaka 70 AD na dola la Warumi. Na katika kipindi hicho wala hakukuwa na sheria za kimataifa zenye kutafsiri kuhusu haki ya mipaka na makazi ya watu.

Mwaka 1948 AD ndipo taifa la sasa la Israeli likaibuka tena, chini ya uwepo wa sheria hizi za sasa za kimataifa. Tunatambua sheria hizi kwa mtazamo wa kibinadamu haziwezi kuwa "retrospective". Pale zilipotungwa ndipo zikaanza rasmi kuwa "binding" ili kulinda maslahi ya wakoloni katika makoloni waliyokuwa wakiyamiliki.

Kwa muktadha huo, ardhi ya Palestina kwa vigezo vya kihistoria ni ya Wayahudi wa kale, yaani zile kabila 12 za wana wa Israeli. Lakini kwa vigezo vya sheria za sasa za kimataifa wote Wapalestina na Waisraeli wana mipaka yao, ila Waisraeli wamevuka mipaka na kujitwalia maeneo yasiyokuwa yao.

Jambo muhimu la kuangaliwa katika jicho la kiroho, kupitia katika historia katika ardhi hii Israeli alikuwa na alama tatu muhimu sana za Kiyahudi, walikuwa chini ya ufalme wao wa Yuda, walikuwa na umiliki wa 100% wa mji wao mtakatifu wa Yerusalemu, na ndani yake walikuwa na hekalu lao takatifu.

Taifa jipya la Israeli lilipoanzishwa tena mwaka 1948 lilikuwa ni likiwa, masalio ya Wayahudi hawakuwa tena na kabila zao 12 za asili wala chini ya ufalme wa Yuda, hawakuwa tena na umiliki wa 100% wa mji wao mtakatifu wa Yerusalemu, wala pia hawana hekalu lao pale katika mlima wa Moria.

Sheria za sasa haziwaruhusu tena kupata haki hizo za asili kuendana na historia. Ndiyo maana Waisraeli wa sasa wanaamini Masihi wao atakuja hivi karibuni na kukalia kiti cha Daudi kama mfalme, ataimiliki Yerusalemu na kuitawala dunia tokea hapo, na atawarudishia hekalu lao pale ulipo msikiti wa Al Aqsa.
 
Kimawaida mgogoro huo wa palestina na Israel ni vigumu kuisha.
Waparestina wana chuki kubwa sana na wayahudi,tena wanawaona kama wanyama na watu wasio kuwa na akiri wala imani yoyote.Yani mparestina kumuua myahudu ni kitendo cha heri zaidi na chenye thawabu kwa allah wao.

Kamwe mparestina hawezi kukaa meza moja na myahudi wakaelewana.Mpalestina anamtambua mu Israel kama mnyama asie staili kuishi nae,kitabu chake mpalestina kina mwambia kuwa myahudi ni adui wake hadi kiama .

Myahudi anamuona mpalestina ni mtu duni,hawezi hata kushirikiana nae kwenye mambo ya msingi,anamuona kama mtumwa anae lazimisha kufanana na boss wake

Chuki iliyopo kwa mparestina zidi ya mu Israel ni kubwa mno.Mambo yatakuwa yanapoa tu na baada ya mda yanaibuka tena.

Hawa watu kwa kutafuta suruhu labda kama mmoja wao angeondoka eneo hilo,yaani mparestina aondoke hapo au muisrael kitu ambacho ni ndoto za alinacha
 
Historia inathibitisha kuwa kabila 12 za wana wa Israeli waliondolewa katika ardhi ya babu zao mwaka 70 AD na dola la Warumi. Na katika kipindi hicho wala hakukuwa na sheria za kimataifa zenye kutafsiri kuhusu haki ya mipaka na makazi ya watu.

Mwaka 1948 AD ndipo taifa la sasa la Israeli likaibuka tena, chini ya uwepo wa sheria hizi za sasa za kimataifa. Tunatambua sheria hizi kwa mtazamo wa kibinadamu haziwezi kuwa "retrospective". Pale zilipotungwa ndipo zikaanza rasmi kuwa "binding" ili kulinda maslahi ya wakoloni katika makoloni waliyokuwa wakiyamiliki.

Kwa muktadha huo, ardhi ya Palestina kwa vigezo vya kihistoria ni ya Wayahudi wa kale, yaani zile kabila 12 za wana wa Israeli. Lakini kwa vigezo vya sheria za sasa za kimataifa wote Wapalestina na Waisraeli wana mipaka yao, ila Waisraeli wamevuka mipaka na kujitwalia maeneo yasiyokuwa yao.

Jambo muhimu la kuangaliwa katika jicho la kiroho, kupitia katika historia katika ardhi hii Israeli alikuwa na alama tatu muhimu sana za Kiyahudi, walikuwa chini ya ufalme wao wa Yuda, walikuwa na umiliki wa 100% wa mji wao mtakatifu wa Yerusalemu, na ndani yake walikuwa na hekalu lao takatifu.

Taifa jipya la Israeli lilipoanzishwa tena mwaka 1948 lilikuwa ni likiwa, masalio ya Wayahudi hawakuwa tena na kabila zao 12 za asili wala chini ya ufalme wa Yuda, hawakuwa tena na umiliki wa 100% wa mji wao mtakatifu wa Yerusalemu, wala pia hawana hekalu lao pale katika mlima wa Moria.

Sheria za sasa haziwaruhusu tena kupata haki hizo za asili kuendana na historia. Ndiyo maana Waisraeli wa sasa wanaamini Masihi wao atakuja hivi karibuni na kukalia kiti cha Daudi kama mfalme, ataimiliki Yerusalemu na kuitawala dunia tokea hapo, na atawarudishia hekalu lao pale ulipo msikiti wa Al Aqsa.

Unasemaje badala kuanzia 70AD uanzie mwanzo kuwa ilikuwa Adam, Eden huko.

Halafu kutokea hapo useme Dunia ilianza na Adam na hivyo Israel na mataifa yote hayakuwapo.

Halafu Sasa useme watu wote ni waisrael na dunia yote ni Israel. Hivyo wote ni ndugu tuishi popote Kwa amani?

Tuacheni ndoto za kufirika. Kama ni amani Kila MTU ana yake.

Kwani Baniani au ma Buddha huko wana imani kama yako?

Sheria ni utangamano. Tuheshimu sheria:

IMG_20231015_072729.jpg
 
5. Wanaotambua vita vya Urusi huko Ukraine ni uvamizi.
6. Wanaotambua vita vya Ukraine dhidi ya Urusi huko Ukraine ni vya ukombozi.
Nakuunga mkono kwa haya mawili pekee, yaani #4 na 5.

Kwa #1 hadi 4, ni ama umefuata mihemko ya udini au bangi.

Ni kosa kubwa kudhani maoni yako tu ndiyo sahihi
 
Mimi nitawaunga mkono ndugu zetu Wapalestina mpaka mwisho. Ipo siku Israel itafutwa kwenye Ramani ya Dunia. By Mahmoud Ahmedneijad, aliyewahi kuwa Rais wa Iran.
 
Nakuunga mkono kwa haya mawili pekee, yaani #4 na 5.

Kwa #1 hadi 4, ni ama umefuata mihemko ya udini au bangi.

Ni kosa kubwa kudhani maoni yako tu ndiyo sahihi

IMG_1567.jpg

Screenshot_20231015-072654.png

Kwenye list hiyo hawawezi kuwa wavuta bangi Wala wadini hao.

List hiyo imefanyiwa kaxi ya kutosha kiasi kuwa vigezo kuzingatiwa mtu anawwza kujitathmini solo.
 
Back
Top Bottom