Ukombozi dhidi ya CCM utapatikana na wanaharakati sio na wanasiasa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,891
Ni jambo la kheri kuwa wanaharakati na wanasiasa hatimaye wametengana na kila mmoja anapambana na hali yake. Kuvunjika kwa koleo sI mwisho wa uhunzi.

Kwani hata nini cha mno kilipatikana tokea miaka 90 hadi leo kwenye muunganiko wa makundi haya? Hadithi zile zile za kuibiwa chaguzi na kutendewa ndivyo sivyo kulikopitiliza.

Japo umoja ni nguvu, bado yawezekana utengano huu ukawa ni mbaraka uliojificha (a blessing in disguise).

Uzi huu wenye kumtambua "kila mdau" kwenye siasa unahusika:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Ikumbukwe vyamani kuliko sheheni wanasiasa waliotamalaki, wanaharakati pia wapo. La msingi ni kuwa, kuwa mwanaharakati hakumsimamishi mtu kuwa mwanasiasa. Hii ikizingatiwa kuwa vyama vyenyewe vya upinzani ni vyama vya harakati.

Tangu lini wasioamini kwenye demokrasia wakawa waumini au washirika kwenye kupambania demokrasia?

Vipi mpigania demokrasia kutomwona Mrusi ni mvamizi Ukraine, akakaa kimya asimwunge mkono Ukraine kwa hali na mali au hadharani?

Au vipi mpigania demokrasia kutomwona Israel kuwa ni mvamizi Palestina, akakaa kimya asimwunge mkono Palestina au HAMAS wenye kupambana na mwizi wao?

Undumila kuwili wa wamaagharibi mgogoro Gaza, Putin Dume!

Mpigania ukombozi au demokrasia hawezi kuwa mandumila kuwili.

"Vipi kuilaumu TCRA na Serikali kuzuia matumizi ya VPN wakati chamani na hata mitandaoni hamko tayari kukosolewa?"

Hatuwachukii CCM Kwa sababu ya jina lao, rangi wanazotumia au mwonekano wao. Tunawachukia kwa sababu ya vitendo vyao vya kutoheshimu demokrasia.

Kwamba hauheshimu demokrasia popote? Wewe pia hatuwezi kukuthamini. Wewe pia ni kama li CCM jingine tu katika rangi zako na mwonekano wako.

"Kwa hakika kupigana vita na wewe upande mmoja ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu."
 
Kuna mambo ukiwa mkubwa utajua ulikua bado unawaza kitoto.

Siasa sio kuongea kila kitu au kufanya kila kitu, dunia haipo hivyo.. Nyerere na ujanja wake wote alithubutu hili likamgharim na nchi kidogo imshinde.

Harakati za panya kuzungunguka bila malengo nazo hazisaidii kitu.

Sasa hao unaona wanaweza kubadili kitu, wana rasilimali gani?

Au unadhani kuropoka na kuhoroja kwenye TV ndio kuleta mabadiliko.

Nikuhakikishie Tanzania siasa za harakati hazifanyi kazi na zaid zaid mnajitafutia maumivu yasiyo na sababu.

Kama unadhani uongo jaribu kufikiri G55 wapo wapi? Kina James Mapala waliishia wapi?

Nyaucho Marando yupo wap?

James Mbatia yupo wap?

Augustine Mrema alienda wap?

Ulimboka alienda wapi?

Mifano ni mingi , muache mihemko, style lazima ibadilike.
 
Kuna mambo ukiwa mkubwa utajua ulikua bado unawaza kitoto.

Siasa sio kuongea kila kitu au kufanya kila kitu, dunia haipo hivyo.. Nyerere na ujanja wake wote alithubutu hili likamgharim na nchi kidogo imshinde.

Harakati za panya kuzungunguka bila malengo nazo hazisaidii kitu.

Sasa hao unaona wanaweza kubadili kitu, wana rasilimali gani?

Au unadhani kuropoka na kuhoroja kwenye TV ndio kuleta mabadiliko....

Nikuhakikishie Tanzania siasa za harakati hazifanyi kazi na zaid zaid mnajitafutia maumivu yasiyo na sababu.

Kama unadhani uongo jaribu kufikiri G55 wapo wapi?
Kina James Mapala waliishia wapi?

Tatizo lako ni kujifanya mjuaji mno kama vile wewe ni supernatural au una mawasilisno na supernaturals.

Wote uliowataja unaodhqni walikwama ndiyo angalau waliotufikisha hapa tunapoendelea kupumua leo, nje ya mashine.

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Kwenye listi ni wanasiasa wanaharakati hakuna mwanasiasa usu hapo wa aina ya akina Samia, Magufuli, au wote unaowafahamu.

Wanasiasa usu ambao ni hawa hapa, hawawezi kutufikisha kokote:

a) Atasimama na suala la katiba au bandari au lolote la wananchi kama ana maslahi nalo binafsi tu. Humo yakiwemo maslahi kiuchumi na ki madaraka.
b) Husimama na wananchi anapoona kuna maslahi yake binafsi yaliyo wazi kwa wakati huo au yaliyo fiche.
c) Huyu gia kubadlika angani ni kawaida.
d) Agenda kipaumbele huwa ni maslahi binafsi. Za wananchi huwa ni kisingizio tu ambazo nazo hutumika kama daraja.
e) Huyu anachosema si lazima kuwa ana maanisha.
f) Hayuko tayari kuwa sehemu ya gharama za ukombozi ikiwamo kufa au kufungwa, yeye au jamaa zake. Huhamasisha wengine kuwa tayari kulipa gharama hizo.
g) Demokrasia kwake mtihani. Yaani alichoona yeye ndiyo masimamo. Haambiliki.
h) Huyu si nadra kuwa na wafuasi wa kulipwa, kumkingia kifua hata bila ya kuwa na hoja.
I) Anampenda mwanaharakati asiyejitambua Ili kumtumia Ili kuyafikia malengo yake.
 
Kuna mambo ukiwa mkubwa utajua ulikua bado unawaza kitoto.

Siasa sio kuongea kila kitu au kufanya kila kitu, dunia haipo hivyo.. Nyerere na ujanja wake wote alithubutu hili likamgharim na nchi kidogo imshinde.

Harakati za panya kuzungunguka bila malengo nazo hazisaidii kitu.

Sasa hao unaona wanaweza kubadili kitu, wana rasilimali gani?

Au unadhani kuropoka na kuhoroja kwenye TV ndio kuleta mabadiliko....

Nikuhakikishie Tanzania siasa za harakati hazifanyi kazi na zaid zaid mnajitafutia maumivu yasiyo na sababu.

Kama unadhani uongo jaribu kufikiri G55 wapo wapi?
Kina James Mapala waliishia wapi?

Nyaucho Marando yupo wap?

James Mbatia yupo wap?

Augustine Mrema alienda wap?

Ulimboka alienda wapi?

Mifano ni mingi , muache mihemko, style lazima ibadilike.
Hata Israel walikariri kama wewe ila kilichowakuta Juzikati hawatakisahau kamwe!
 
Wanaharakati ni zaidi ya hao ila na hao wakiwamo. Zingatia orodha hii pia:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Wa namna hiyo.

Wanasiasa ni kama huyu:

View attachment 2783449

Hakuna ukombozi hapo.

Mkuu mbona mafumbo mengi? Badala muendelee na mipango yenu mnaongea kwa mafumbo tena! Adui amafahamihika, hit the target usisubiri wenye mbinu nyingine. Hapo itaonekana mlikuwa na mipango, lakini backup yenu mlitegemea kuipata mahali pengine. Mna hoja za msingi, zutumieni hizo ziwape ushindi. Lakini mkiendekeza mafumbo mtaonekana Ngoma hamuiwezi bali mnaleta mikwara mbuzi.
 
Hata Israel walikariri kama wewe ila kilichowakuta Juzikati hawatakisahau kamwe!

Israel kwa mustabala huu ni kama CCM tu yaani ni mvamizi mpinga demokrasi.

Alipo anadai ni mawingu. Baba yake kamwambia atulie kitanuka.

Asante Iran.

Udhwalimu utashindwa!
 
Mkuu mbona mafumbo mengi? Badala muendelee na mipango yenu mnaongea kwa mafumbo tena! Adui amafahamihika, hit the target usisubiri wenye mbinu nyingine. Hapo itaonekana mlikuwa na mipango, lakini backup yenu mlitegemea kuipata mahali pengine. Mna hoja za msingi, zutumieni hizo ziwape ushindi. Lakini mkiendekeza mafumbo mtaonekana Ngoma hamuiwezi bali mnaleta mikwara mbuzi.

Fumbo liko wapi ndugu. Hata tusiongee? Haya ya kuzuiana kuongea ndiyo ya CCM na Serikali yake.

"Usipambane na mleta mada (hoja), pambana na mada (hoja) zake. Kulikoni kuumia moyo hivyo ndugu?

Hata tusifikirie kwa sauti? Mnataka tufikirie kimya kimya siyo? Mbona tunaendelea Kufikiri?

Sasa hivi sisi wananchi wadau tunajua, ukombozi wa nchi hii uko na wanasiasa wanaharakati hawa hapa:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.

Hii ikiwa ni matokeo ya kufikiria. Kwa hakika Kwa kufikiria (objectively) tunaweza kuiona kesho yetu njema iliko kwa uwazi zaidi.
 
Israel kwa mustabala huu ni kama CCM tu yaani ni mvamizi mpinga demokrasi.

Alipo anadai ni mawingu. Baba yake kamwambia atulie kitanuka.

Asante Iran.

Udhwalimu utashindwa!
Ufaransa kamwambia Iran asithubutu kujiingiza Gaza kwani atujuta!
 
Fumbo liko wapi ndugu. Hata tusiongee? Haya ya kuzuiana kuongeza ndiyo ya CCM na Serikali yake.

"Usipambane na mleta mada (hoja), pambana na mada (hoja) zake. Kulikoni kuumia moyo hivyo ndugu?

Hata tusifikirie kwa sauti? Mnataka tufikirie kimya kimya siyo? Mbona tunaendelea Kufikiri?

Sasa hivi sisi wananchi wadau tunajua, ukombozi wa nchi hii uko na wanasiasa wanaharakati hawa hapa:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.

Hii ikiwa ni matokeo ya kufikiria. Kwa hakika Kwa kufikiria (objectively) tunaweza kuiona kesho yetu njema iliko kwa uwazi zaidi.

Duu leo kazi ipo.
 
Ufaransa kamwambia Iran asithubutu kujiingiza Gaza kwani atujuta!

Huo ni mkwara tu. Mkwara mdogo tu wa Israel, Israel anabakia mpakani na maji kafungua kwenda Gaza.

Uelekeo wetu kuipata Katiba mpya tumeujua. Wanasiasa wametuchelewesha sana.

Nani atakwenda kwenye maandamano ya wanasiasa wasiotokea wao wenyewe Ila kuwatumia wanarakati.

Picha Iko wazi:

"Kutumiana kama magrader hakukubaliki."
 
Ni jambo la kheri kuwa wanaharakati na wanasiasa hatimaye wamejitenga na kila mmoja anapambana na hali yake. Kuvunjika kwa koleo sI mwisho wa uhunzi.

Kwani hata nini cha mno kilipatikana tokea miaka 90 hadi leo kwenye muunganiko wa makundi haya? Hadithi zile zile za kuibiwa chaguzi na kutendewa ndivyo sivyo kulikopitiliza.

Japo umoja ni nguvu, bado yawezekana utengano huu ukawa ni mbaraka uliojificha (a blessing in disguise).

Uzi huu wenye kumtambua "kila mdau" kwenye siasa unahusika:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Ikumbukwe vyamani kuliko sheheni wanasiasa waliotamalaki, wanaharakati pia wapo. La msingi ni kuwa, kuwa mwanaharakati hakumsimamishi mtu kuwa mwanasiasa. Hii ikizingatiwa kuwa vyama vyenyewe vya upinzani ni vyama vya harakati.

Tangu lini wasioamini kwenye demokrasia wakawa waumini au washirika kwenye kupambania demokrasia?

Vipi mpigania demokrasia kutomwona Mrusi ni mvamizi Ukraine, akakaa kimya asimwunge mkono Ukraine kwa hali na mali au hadharani?

Au vipi mpigania demokrasia kutomwona Israel kuwa ni mvamizi Palestina, akakaa kimya asimwunge mkono Palestina au HAMAS wenye kupambana na mwizi wao?

Undumila kuwili wa wamaagharibi mgogoro Gaza, Putin Dume!

Mpigania ukombozi au demokrasia hawezi kuwa mandumila kuwili.

"Vipi kuilaumu TCRA na Serikali kuzuia matumizi ya VPN wakati chamani na hata mitandaoni hamko tayari kukosolewa?"

Hatuwachukii CCM Kwa sababu ya jina lao, rangi wanazotumia au mwonekano wao. Tunawachukia kwa sababu ya vitendo vyao vya kutoheshimu demokrasia.

Kwamba hauheshimu demokrasia popote? Wewe pia hatuwezi kukuthamini. Wewe pia ni kama li CCM jingine tu katika rangi zako na mwonekano wako.

"Kwa hakika kupigana vita na wewe upande mmoja ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu."
CCM imeroka kwenye misingi ya uanzishwaji wake.

Ni vyema kikapumzishwa
 
Mkuu mbona mafumbo mengi? Badala muendelee na mipango yenu mnaongea kwa mafumbo tena! Adui amafahamihika, hit the target usisubiri wenye mbinu nyingine. Hapo itaonekana mlikuwa na mipango, lakini backup yenu mlitegemea kuipata mahali pengine. Mna hoja za msingi, hizo ziwape ushindi. Lakini mkiendekeza mafumbo mtaonekana Ngoma hamuiwezi bali mnaleta mikwara mbuzi.
Nyie mpo upande gani ktkt hili?
Je hili ni la kikundi fulani?
Je ni maslahi ya taifa au watu binafsi?
Kwani mnawachukuliaje wananchi, Hawana vichwa na hawawezi kufikiri ninyi (Mbowe & company)ndio mnafikiri badala yao?
 
CCM imeroka kwenye misingi ya uanzishwaji wake.

Ni vyema kikapumzishwa

Mkuu hilo kila mtu analijua hata CCM wenyewe wanalijua. Ndiyo maana bila ya haya tunawaita kuwa ni "maadui."

Huo ndiyo ulio msingi wa mada wenye kutambua tusipoamka tutaendelea kucheza makida makida iliyochezeka tokea miaka ya 90.

Kujua kwanini imekuwa hivyo na kuchukua hatua zingine ndilo hili naloliona wanaharakati watatuvusha.
 
Nyie mpo upande gani ktkt hili?
Je hili ni la kikundi fulani?
Je ni maslahi ya taifa au watu binafsi?
Kwani mnawachukuliaje wananchi, Hawana vichwa na hawawezi kufikiri ninyi (Mbowe & company)ndio mnafikiri badala yao?

Kwenye orodha ile kuna hii:

h) Huyu si nadra kuwa na wafuasi wa kulipwa, kumkingia kifua hata bila ya kuwa na hoja.

Kwenye ukombozi ni lazima tutambuane kwa mujibu wa huyu mwuungwana (Zawadini) kutoka zenjibar huko. Hasa hasa ikizingatiwa ukombozi wenyewe hauhitaji wala watu wengi:

IMG_20220927_190940_421.jpg
 
Back
Top Bottom