Madai ya kupata katiba mpya ni mapambano ya haki ambayo hayawezi kukamilika bila ya kupata katiba nyingine tofauti na iliyopo.
Mwenyekiti Mbowe na baadhi ya wapiganaji (Mola awafanyie wepesi) tayari wako mikononi mwa watesi wetu.
Wao wametangulia na hakuna mpambanaji aliye salama.
Pamoja na kuwa mapambano haya ni ya haki na yako kwa mujibu wa sheria, unyeti wake na vizingiti vilivyomo vinalazimu kufahamiana vizuri kwa mustakabala mwema wa zoezi zima.
Yafahamu makundi haya yaliyopo katika jamii yetu:
1. Wadai: Wapambanaji walio dhamiria kuidai haki yao ya kuwa na katiba mpya itakayo wahakikishia wote uhuru, usawa, haki, demokrasia na uwajibikaji.
2. Wadaiwa: Wanufaika wa hali iliyopo sasa. Hawa ni walioko madarakani. Wenye maslahi binafsi yenye uwezekano wa kupotea kwa ujio wa katiba mpya.
3. Washirika: Marafiki zetu wa ndani na nje ambao pamoja na tofauti zetu nao katika mambo mengine, tuna malengo ya mwisho kuhusiana na katiba mpya yanayofanana.
4. Maadui: Hawa ni vibaraka wa wadaiwa. Hapa wamo wale wenye vipigo vya mbwa koko na wote wanaotumika kwa namna yoyote ili kutatiza harakati hizi kwa maslahi yao binafsi na mabwana zao wa #2.
Kwenye kundi hili wamo pia wajumbe kadhaa wa humu JF. Mitizamo yao kupitia nyuzi na comments zao inajieleza wazi.
5. Wasiohusika: Hawa wapo wenye kutokujua kuwa wanahusika na wengine wenye kujitoa ufahamu kwa makusudi (opportunists) ili kupisha kuwa sehemu ya mchakato na kusubiria matunda wale bila karaha.
Wasiohusika kwa kutokujua wanahitaji kuelimishwa. Ndipo umuhimu wa makongamano na mikutano ya vyama vya siasa inayopigwa vita na wadaiwa na maadui zetu ulipo.
Angalizo: tutazamane usoni vizuri kujiridhisha. Mamba wala watu hawawezi kuwa sehemu ya ushauri wa namna ya kuvuka mto salama.