Tutajie Mbunge ambaye hujawahi kumsikia akichangia chochote Bungeni

Mbunge wa Karatu anaitwa Daniel Awack ... huyu yupo yupo tu hajawahi kuchangia . Jimboni hayupo wala Bungeni haonekani
 
Hadi wakina Msukuma na Mpina wanapata nafasi kila siku ya kuchangia kati ya wabunge 360 ni ukweli kwamba wapo wabunge wengi ambao kwao wao ubunge ni posho.

Vikao vya bunge vinaanza hadi vinamalizika hakuna siku amewahi kuchangia chochote. Wengi wao ni wabunge wa viti maalum. Swali la kujiuliza wanatumia mbinu gani kuwasiliana na waliowatuma?

Nichukue fursa hii kuomba tuwafahamu wale ambao sauti zao kuzisikia ni nadra tuweze kuwakumbusha umuhimu wa kuongea na kutusemea kunako Bunge.
Kigwa wa Kigwa.....
 
Je,hao wanao ongea kama chiriku,wamefanya nini ktk majimbo yao....? matendo yanaongea zaid kuliko maneno...
 
Mbunge wa Moshi Vijijini Prof. Ndakidemi

Tena ni Prof ila sijawahi kumsikia kabisa.. Itakuwa wananchi wake hawana shida za kuziwasilisha... hahahaha
Uchaguzi wa 2020 Kilimanajaro ilipata hasara sana ukiondoa Dk Kimei nadhani hakuna mbunge mwingine wa maana.
 
Back
Top Bottom