Tutaishikisha adabu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaishikisha adabu CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by minda, Jul 6, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini zimeahidi kukinyima kura Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyia mwezi Oktoba mwaka huu kwa lengo la kukishikisha adabu kwa madai kwamba kimewadharau baada ya kushindwa kutekeleza mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

  Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam na kiongozi wa Jumuiya hizo, Ally Basaleh alipozungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtoro.

  Alisema CCM kimewadharau Waislamu kwa kushindwa kutekeleza Ilani yake ya mwaka 2005 ambapo kiliahidi kuanzisha mahakama ya Kadhi kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali ya Kiislamu.
  Aidha alisema Waislamu hawapo tayari kuona serikali inaanzisha Mahakama hiyo kupitia mgongo wa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (Bakwata).

  Alipinga kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwamba jukumu la kuunda Mahakama hiyo waachiwe Waislamu wenyewe kwa kuwa serikali inataka kujitoa katika suala hilo.
  Aliongeza kuwa Waislamu wanataka suala hilo liingizwe katika Katiba ya nchi pamoja serikali kutoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wake ikiwemo kulipa mishara ya watumishi wake.
  "Tunataka serikali iunde mahakama hiyo pamoja na kuigharamia kwa kuwa CCM mwaka 2005 katika ilani yake ya uchagzui iliahidi kutekeleza mpango huo," alisema

  Aliongeza kuwa matatizo ya Waislamu yakiwemo ya kudai mirathi na talaka yanatakiwa kushughulikiwa na wao wenyewe kwani wao wanayajua kwa undani kuliko watu wengine.
  Waislamu jijini Dar es Salaam wameandaa maandamano kwa ajili kudai mahakama hiyo huku Jeshi la Polisi likiwataka kuachana na mpango huo.
  Wamedai kwamba hata kama polisi watawazuia kuandamana wao hawatajali lakini lazima watimize azma hiyo.
  Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Charles Kenyela alisema waislamu wanaotaka kuandamana bila kibali wanakurupuka na kwamba mazungumzo kati ya jeshi hilo na viongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania, yanaendelea vizuri.
  Kamanda Kenyela alisema viongozi hao waliwasilisha barua ya kuomba maandamano kufanyika Julai 9, mwaka huu, ambapo bado haijajibiwa na ipo kwenye hatua ya majadiliano.
  "Nashangaa nimesoma kwenye vyombo vya habari viongozi hao wakitamka kwamba wataandamana kwa nguvu hata kama jeshi limekataa... Naona wanakurupuka tu bila kuzingatia sheria," alisema Kamanda huyo.


  CHANZO: NIPASHE; Na Waandishi wetu -3rd July 2010.

  HIVYO: wana jf, tatizo langu ni hapo kwenye rubrics. je, ni haki kisheria/kishariya, kutumia fedha za walipa kodi ambao baadhi yao ni makafiri, kugharamikia mahakama tajwa? without prejudice to the ongoing tallks between the GoT and BAKWATA/muslims, naombeni michango yenu.
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nina baa yangu na bucha la kiti moto sitaki kodi yangu iichangie hiyo mahakama.mpaka bakwata iniandikie barua ya maombi. mpo hapo wadau?
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Njia ya mongo ni fupi. Kama kawaida yake ccm wakitumia aina ile ile ya usanii kutafuta kuungwa mkono wamejitumbukiza katika kisa cha kuvunja katiba ya nchi ndani ya ilani yao ili wawapendezeshe baazi ya watu. Sasa yamewafika shingoni. Waislamu nchini waliwapa ccm kura zao wakijua kwamba watatimiziwa ahadi ya mahakama ya kadhi. Sasa ni wajibu wa serikali ya ccm kuwapa hiyo mahakama kama walivyoahidi. Huku nje nasi tusio waislamu tunasubiri hayo yatimizwe ili tuanze rasmi mchakato wa kumpa mkuu wa nchi red card kwa kukiuka kiapo cha kuilinda katiba ya nchi. Nina wasi wasi kama kweli waisilamu wana ubavu wa kuinyima ccm kura. Ilani ya kumrudisha kikwete madarakani itakuja bila kipengele cha kadhi na kitakachofanyika ni kuwasanii waislamu bila kujifunga kisheria. Kitu ambacho ccm inaamini kwamba kuwahadaa waislamu ni kazi rahisi tu. Unawagawanya na kisha unawatawala
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Waislamu wana point kubwa sana katika madai yao. Wanachodai wao ni ahadi iliyotolewa na CCM kupitia ilani ya Uchuguzi wa 2005 na si zaidi. Watanzania wote tungejifunza kudai kama waislamu wanavyofanya nchi hii inekuwa mbali. Mimi ni mkristo lakini nawaunga mkono 100% kama ahadi hiyo ilitolewa ni kwanini haitekelzwi kama tatizo ni fedha mbona mafisadi wanajichotea wanavyotaka bila ya sisi kuchukua hatua yoyote, mahakama hizi zipo karibu nchi zote Kenye, South Africa na hata Ulaya.

  Tuache ushabiki wa kidini it is their right kwa kuwa walipatiwa ahaidi hiyo
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  njia pekee ya kukishighulikia chama mbacho hakijatimiza ahadi ni kukiondoa madarakani, sasa kwa kua wao kuna ahadi fualni hawajatimiziwa basi october si mbali, wasiwachague tu! simple as that badala ya kuleta bugudha kwa wakazi wengine wa jiji!
   
 6. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  mlidanganywa mkakubali! poleni sana. kama ulikubaliana na CCM kuwa wanaubavu wa kuanzisha mahakama ya kdhi then check your level of literacy
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Basi mtawashawishi hata wale wa ufaransa wamnyime rais wao kura maana wametangaza kupiga marufuku hijab kuvaliwa nchini mwao?:heh:
   
Loading...