Tutafakari, nchi haiko sawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafakari, nchi haiko sawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Feb 12, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tutafakari, nchi haiko sawa

  John Bwire, Mhariri Raia Mwema Februari 11, 2009


  SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Jamhuri ya umoja ambayo iko chini ya demokrasia ya Bunge la vyama vingi vya siasa.

  Ina nguzo tatu za utawala ambazo ni: Serikali, Mahakama na Bunge. Vyombo hivi vitatu vya utawala vina uwezo na madaraka ya kusimamia shughuli zote za umma.

  Katika mfumo usio rasmi, vyombo vya habari navyo vimetajwa kama mhimili wa nne wa dola, na vimekuwa vikitoa mchango mkubwa katika mfumo mzima wa utawala bora na utoaji elimu na upashaji habari. Kwa muda mrefu vimetimiza wajibu wake.

  Kwa kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ndio uliokubalika na kutumika katika Tanzania, vyama vya siasa navyo vimekuwa na mchango mkubwa katika mustakabali wa taifa hili pamoja na kuwa ndani ya mhimili wa Bunge wamo wanasiasa wa vyama vyote.

  Kwa utangulizi huo hapo juu, tuna kila sababu ya kushituka inapotokea kuwapo kwa kauli za kusigana katika mihimili rasmi na ule usio rasmi na kwa kuongezea katika matatizo hayo inatisha zaidi kuwapo matatizo ndani ya vyama vyote vya siasa na miongoni mwa vyama husika.

  Hali hiyo inavigusa vyama vya upinzani na chama tawala cha CCM.

  Taarifa za hivi karibuni kwamba Spika wa Bunge Samuel Sitta na Jaji Mkuu Augustino Ramadhan wametofautiana hadharani kuhusiana na mipaka ya vyombo vyao, ni mwangwi wa hali ilivyo sasa katika mfumo mzima wa utawala katika taifa letu.

  Kama ilivyo katika utangulizi hapo juu hali hiyo haijaviacha vyombo vingine kama vile Serikali yenyewe ambako tumeshuhudia serikalini vyombo kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi vikilumbana, na kuna wakati vyombo hivyo vimesikikika vikiilaumu Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuhusiana na mwenendo wa kesi vinazochunguza.

  Kadhalika, ndani na nje ya Bunge kumeripotiwa kuwapo taarifa za kuwapo mgawanyiko wa wazi wa vyama vya siasa na hata baadhi ya wanasiasa wa chama kimoja ikiwa ni pamoja na kuparaganyika kwa vyama vya upinzani na hata chama tawala cha CCM.

  Kwa upande wa vyombo vya habari nako hali inaelekea si shwari tena kwa kuibuka malumbano ya wazi ambayo yanapotoeza mwelekeo na sasa kuhamia kuingiliwa kwa mambo binafsi zaidi huku hoja za msingi zinazolenga kuwakomboa Watanzania zikiachwa kwa makusudi kwa nia ya kubeba ajenda za watu wachache wanaotaka kujilinda.

  Kama Taifa, hivi sasa Tanzania inaelekea imekuwa mithili ya mechi ya mpira wa miguu ambayo inachezwa bila ya kuwa na refa kutokana na mambo kwenda ovyo karibu katika kila eneo muhimu kwa mustakabli wa nchi hii.

  Hali hii si njema kwa Taifa na ina hatari ya kuwafanya wananchi wa kawaida wakose mahali pa kukimbilia, jambo ambalo ni la hatari kwa amani na utulivu wa Taifa, tulivyorithi na tulivyovilinda kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

  Sisi tunatoa mwito kwamba sasa ni wakati muafaka wa kutafakari na kuchukua hatua za haraka.


  SOURCE: Tutafakari, nchi haiko sawa
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa maoni yangu, bada ya kusoma ya Mhariri wa Raia Mwema, naona una ombwe (Vacum) kubwa katika uongozi wa nchi. Nadhani hatuna uongozi. Uongozi umeyumba, sawa na familia ambayo wazazi wameshindwa kuiongoza. Tutafakari na vyombo vyetu vya USalama hasa UWT (TISS) waamke na kuacha kutetea mabwana zao wafanye utafiti kuhusiana na hali ya nchi kabla mambo hayajaharibika maana wananchi wakitibuka itakuwa kazi kuwahimili.
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Siku Zote Serikali ya CCM imekuwa ikijivunia AMANI na Utulivu. Sasa hiyo Amani na Utulivu imetusaidia nini katika uchumi. Katika Hiyo Miaka tumeona maisha ya kila siku ya watanzania zaidi ya asilimia 90 yakiwa taabani. Shilingi imeshuka thamani na mfumuko wa bei umeongezeka. Pia ni vigumu kupata hiyo shillingi. Vigogo wamejenga nyumba dubai, USA, South Africa,Mbezi Dar.

  Inakuwaje uchumi wa Marekani uyumbe halafu dola yao iwe imara kuliko Shillingi ya Tanzania.

  UWT/TISS wanasaidia nini?? Mbona hawakuweza kuzuia Kashfa ya EPA, CIS, Majengo Pacha, Richmond, IPTL?? Mbona TISS wasizuie mauaji ya albino.

  TISS/UWT ni kwa ajili ya usalama wa nini,??

  Angola na Rwanda wamekuwa kwenye vita zaidi ya miaka 16, wametulia kwa miaka michache iliyopita, lakini angalia uchumi wao unavyokuwa kwa kasi, Thamani ya pesa zao inaongezeka, Sisi amani na utulivu imetusaidia nini??

  Pia hali mbaya ya uchumi ikiendelea kuwa mbaya, halafu Mambo ya UFISADI yakiendelea ujue kuwa Wananchi watakosa uvumilivu. Dalili zimeanza kuonekana, Zomea zomea viongozi, Kupiga mawe misafara ya Raisi, Maandamano....Bado huku mitaani wananchi wanalaani sana, Wanasema Hii NChi itakuwa ya Michakato mpaka lini au uchunguzi unaendelea mpaka lini. Wanataka mafisadi waadhibiwe, ufisadi ukomeshwe na uchumi uimarike.

  Nawaomba hao usalama wa Taifa, wafanye utafiti. Wapande dala dala, waingie madukani kusubiri watu wanaokuja kununua bidhaa, foleni za wagonjwa hospitalini na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko ya watu wa kawaida, maisha ya kawaida . wasikilize mazungumzo na mijadala. Hali ni mbaya, taifa linaelekea pabaya.
  UWT/TISS acheni mzaha, fanyeni utafiti na mumshauri RAiS.

  PIa ccm yenyewe si moja, si chama kimoja tena. Kuna makundi au umoja fulani fulani au mtandao wenye masilahi tofauti. Hivyo kuna Chama ndani ya Chama. ENzi za MZee Mwinyi haikuwa hivi. Chama ndani ya chama imeanza kujijenga wakati wa mkapa. Na sasa wakati wa Kikwete kuna vyama ndani ya Chama.

  Wakulima na wafugaji ni ugomvi. Pia ugomvi kati ya wafanyabiashara upo, mfano mafuta ya diesel.

  Natamani kuanzisha mjadala wa kitaifa ili Vyama vyote vya kisiasa vijadili mustakabadhi wa taifa. Angalia Marekani, kuna demokrasia ya kweli na Wamarekani wanapendana mno. Sisi watanzania vipi??

  Wamarekani wakimaliza uchaguzi wanarudi mezani wanaanza kujenga nchi.

  Pia angalia WAarabu, Warusi (USSR) na Waisraeli. Wanauzalendo na nchi zao. Popote pale walipo wanatetea nchi zao, hata wakenya wapo mbele yetu. Angalia wanavyovutia kamba upande wao masuala ya EAC.

  Sisi inabidi tutume wasome nchi za nje wakatuletee Teknologia nchini kwetu.

  Pia watu walioko kwenye sekta nyeti na za maamuzi mazito wapewe mishahara mizuri na wawekewe Life insurance. Sasa hapo atakuwa mzalendo. Na kama ataamua kuwa fisadi, ni kuwa ameisaliti nchi na anastahili kunyongwa.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Halisi,

  ..........yaani inasikitisha sana.........watu wamekosa nidhamu..........wanapayuka payuka tu kama wako kwenye jukwaa la Simba au Yanga.........utafikiri hawakupata elimu ya uongozi.......kwenye serious issue......unakuta mtu anapayuka atakavyo......halafu wasema potelea mbali........damn!
   
 5. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Kama wewe siyo albino,nchi hii haina matatizo yoyote.
  Kwa hiyo,Mr. Bwire,we ask you not to panic.
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hii hali tumekuwa nayo muda mrefu na wala si jambo lililojitokeza kipindi hiki peke yake, tofauti inonekana kutokana na uwazi ulioongezeka kipindi hiki cha JK hadi tunashuhudia live mijadala ya bunge na uhuru wa media umeongezeka kidogo.

  La muhimu ni viongozi wetu kulitambua hilo na kujizuia kulumbana hadharani vinginevyo watatutia wasiwasi sisi raia wa kawaida.
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na hakuna tafakuri, kwa kuwa siku zinakwenda, hatujui, na hatujui kwamba hatujui hadi siku tutakapojua, wajuzi watakuwa wamesahau kwamba walitutenda na watakuwa hawapo tena. Watakua Asia Amerika na Ulaya. TUMEKWISHA.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Umesema vyema, tunachokiona ni dalili tu za ugonjwa uliopo. Tunachokishuhudia ni kutetema kwa mgonjwa wa malaria. Hatujawa tayari kuangalia tatizo hasa ni nini.

  Taifa letu liko matatani si kwa sababu halina wasomi, si kwa sababu halina mali, si kwa sababu halina sera, au sheria zake hazipo; bali kwa sababu moja kubwa. Taifa letu limekosa viongozi wenye uwezo wa kuongoza.

  Tatizo letu liko matatani kwa sababu wale waliopo wengi wao wapo wapo tu. Wana uwezo wa kupiga kelele, wana uwezo wa kutoa vitisho, wana uwezo wa kuzungumza (baadhi yao) lakini ni wachache wenye uwezo wa kuongoza.

  Nimejuaje? nimeangalia matokeo! Uongozi haupimwi kwa kuangalia majigambo, sera, magari n.k Uongozi unapimwa kwa matokeo. Matokeo ni mabaya.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Sasa nani anaweza kuongoza?
   
 10. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Maybe I was the only person who took him seriously mwenzetu mmoja hapa aliposema 'Somalia is better than Tanzania' japokuwa hakutoa sababu, you can all see what he meant!
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tumpe nchi Fundi Mchundo, I mean it!!!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Feb 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Naah...mimi nasema Kitila Mkumbo....
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Seconded, I mean it !!!
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu M.M., nchi hii ina wataalam wa kila aina. Ina viongozi wenye uwezo mkubwa, wenye mapenzi mema na nchi na watu wake. Ina rasilimali zote na zaidi ya zinazotakiwa kuleta maendeleo, usalama na amani kwa watu wote. Nchi hii imebarikiwa kwa kila kitu.

  Ila tu, kila mwenye uwezo wa kufanya mabadiliko ni adui mkubwa wa utawala uliopo. Ni adui kwasababu anakuwa tishio kwa uwepo wa wengi wao na anakuwa tishio kwa ustawi wao.

  Wakuu, nchi hii ni nchi pekee ambayo haijui watu wake ni akina nani (hakuna national Id) hadi leo na haijui wana uwezo gani. Kwa ufahamu wangu mdogo, najua hilo ni tatizo kubwa sana katika juhudi zozote za maendeleo na usalama wa nchi. Fikiria, kuna waTanzania Kongo, Rwanda, Burudni n.k ambao wanafanya mambo mazuri na ambayo hayapo hapa kwetu (tunayatamani) bila nchi kujua wapo huko. Wangekuwepo hapa, wangesaidia sana. Ila hawajulikani na hata wakirudi, hawatapewa nafasi nzuri ya kufanya mambo kama wanayofanya huko walipo. Mambo mazuri sana.

  Wataalamu wetu kwa kutokujaliwa na utawala wetu, wameamua kuishi na kuendeleza nchi za wengine, kwakuwa huko walau wanapata wanachoona wanastahili. Nchi hii ni moja ya nchi ambazo wananchi wake hawashirikishwi kwa namna yoyote katika maendeleo ya kila siku ya Taifa (zaidi ya uwakilishi kwa njia ya Bunge, ambao wote mnajua jinsi ulivyo). Wananchi wana nia thabiti ya kushiriki maendeleo yao. Ila hakuna mpango wa kuwashirikisha. Serikali ndio inayojua kila kitu na ndio inayotaka kufanya kila kitu. Kama ikiamua watu wafanye baadhi, basi watakuwa wale wale wakuu wanaowapenda sana.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa nchi umeyumba na haustahili tena kurudi madarakani 2010. Wengi wetu tulikuwa na imani kubwa na Kikwete kutokana na ahadi zake chungu nzima alizoahidi wakati wa kampeni ikiwemo kuipitia upya mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwetu Watanzania, kupambana na mafisadi, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Sasa hivi hakuna hata moja katika ahadi zake ambalo ametimiza, matumaini ya maisha bora kwa kila Mtanzania yamepotea, sasa imekuwa ni maisha bora kwa kila fisadi. Na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya sasa imegeuka na kuwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya kuminya uhuru wa Wabunge kila kukicha katika maswala mbali mbali ambayo yana maslahi makubwa kwa nchi yetu. Wengine walimwita ni chaguo la Mungu, kumbe ni chaguo la mafisadi. Hakukosea pale alipowapa kipaumbele ili wambebe na kungia Ikulu sasa anafanya kila njia kuwalinda mafisadi hao kwa hali na mali.

  Kesi ya EPA ni danganya toto tu itavutwa hadi uchaguzi wa 2010 baada ya hapo itadaiwa hakuna ushadi wa kutosha dhidi ya watuhumiwa na hivyo wote kuachiwa huru.

  Nchi yetu inaelekea pabaya sana na wa kulaumiwa ni Viongozi wa juu wa CCM na Serikali ambao wameweka mbele maslahi ya chama chao badala ya yale ya nchi.
   
Loading...