Tutaandamana bila kibali cha Polisi ifikapo Jan 5 - Slaa

Kweli Slaa umeshikwa pabaya, na haya unayotaka kuanzisha hatuafikiani nayo, dola ikiwafanya vibaya sie hatumo, kwani huko ni kuichokoza dola kwa makusudi kabisa.
Hivi we genius brain hivi kweli dola ikifanya upuuzi haistahili kuguswa? Hata kama ina nguvu na inavunja sheria inamaanisha isiguswe, isikosolewe na watu wasiidai haki kwa kuwa ni dola tu?
 
Ukitaka kuingia ndani unapita mlangoni, ikishindikana mlangoni basi dirisha litumike, nalo pia likishindikana basi utaratibu mwingine ikiwa ni pamoja na kutoboa ukuta ili kuingia ndani.


Chadema tumechoka sasa na tunatoboa ukuta (mimi niko tayari), huku kuchekeana sasa hivi kumetuchosha, CCM wanataka tuwaonyeshe kuwa tunamaanisha tunachokisema.

Mungu ibariki Chadema daima itetee haki ya mtanzania maskini na mnyonge ambaye sauti yake ni kelele masikioni mwa Serikali ya CCM, Mungu ibariki Tanzania na wote wazalendo wa nchi hii!
 
Dk. Slaa kuongoza maandamano Arusha leo

na Janet Josiah

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa pamoja na viongozi wengine, leo anatarajia kuongoza maandamano na mkutano wa hadhara mkoani Arusha kupinga unyanyaswaji na ubakwaji wa demokrasia unaofanywa na vyombo vya dola hasa Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema maandamano hayo yatakuwa na ujumbe tofauti tofauti kuieleza serikali namna vyombo hivyo vya dola vinavyokiuka sheria na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa mameya wa halmashauri.

Alisema maandamano na mkutano huo utaelezea mambo yote yanayoendelea katika halmashauri za Hai, Mwanza na Arusha kuhusu umeya; yatazungumzwa ili kuwapa Watanzania na serikali hali inayoendelea.

"Lengo kubwa la maandamano ya amani na mkutano mkubwa wa hadhara ni kutaka kuwaelezea Watanzania na serikali, machafu yahusuyo unyanyaswaji wa demokrasia katika uchaguzi wa mameya unaoendelea.

"Suala la kuandikwa kwa Katiba mpya na kitendo cha kinyama cha kumshambulia na kumuumiza hadi kulazwa hospitali mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, uliofanywa na askari polisi mkoani humo vitawekwa hadharani" alisema.

Dk. Slaa alisema ingawa katika halmashauri ya Kigoma Mjini tayari kitendawili kimeshateguliwa, bado Watanzania wanahitaji kujua kinachoendelea katika halmashauri nyingine ambazo hazijafanya uchaguzi na kwa nini hakuko shwari.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameamua kufanya maandamano ambayo yamepata kibali cha Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kuwapa taarifa ya kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kupatiwa ulinzi.

Hadi sasa halmashauri za mikoa ya Arusha, Mwanza na Hai hazijaweza kufanya uchaguzi wa kuwapata mameya, kutokana na hisia za kuwepo kwa uchakachuaji, kutofautiana juu ya njia za kupiga kura na mbunge wa viti maalum kuteuliwa kupiga kura.

Hata hivyo, uchaguzi kwenye halmashauri ambazo Chama cha Mapinduzi (CCM) kilionekana hakina upinzani, ulifanyika bila ya matatizo ikiwa ni pamoja na manispaa za mkoa wa Dar es Salaam.
 
Ule Ujasiri wa Dkt Slaa na Wapinzani kwa Jumla ulitokana na Ujasiri na Utayari wa Rais Kikwete kupokea Changamoto za Wapinzani, pamoja na zile Heka hela zote bado tulikuwa tunafanyia Semina za Serikal kwny Hotel za Mh. Mbowe, Billicanus iliruhusiwa kuendelea kukwepa Kodi
 
Back
Top Bottom