Tutaandamana bila kibali cha Polisi ifikapo Jan 5 - Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaandamana bila kibali cha Polisi ifikapo Jan 5 - Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Dec 24, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa juzi Desemba 22 kamwandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa ikieleza kwamba, iwapo madai yao hayatatekelezwa hadi Januari 4, 2011 chama hicho kitaitisha maandamano siku inayofuata bila kujali yana kibali cha polisi au la.

  "CHADEMA sasa tumefikia mahali tumechoka na unyanyasaji, serikali ijue hivyo. Ni imani yetu kama serikali inataka haki itendeke, hatua stahiki ziwe zimechukuliwa kwa wahusika kabla ya terehe 4 januari, 2011," ilieleza barua hiyo.

  Masharti ya barua:

  Katika barua hiyo kimetoa masharti ya kumaliza migogoro ya uchaguzi wa mameya katika maeneo yote yenye utata.

  Barua imetaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na Halmashauri za majiji ya Mwanza na Arusha, Hai, Kigoma Ujiji, ambako chama hicho kimedai chaguzi zimevurugwa katika mazingira yanayoashiria kuwapo maelekezo kutoka ngazi za juu.

  Masharti ya chama hicho ni pamoja na kutaka usifanyike uchaguzi wowote wa mameya au wenyeviti wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Manispaa ya Arusha na Hai.

  Masharti mengine Chadema imemtaka Mkurugenzi wa Manispaa Arusha ajiuzulu kwa kukiuka kanuni za halmashauri na kusimamia uchaguzi kinyume na taratibu, vile vile uongozi wa TAMISEMI uliingilia uchaguzi hasa Kigoma/Ujiji, hivyo wahusika wote wachukuliwe hatua.

  Chama hicho pia kimeitaka serikali kumchukulia hatua OCD wa Arusha kwa kuingia na kumkamata mbunge ndani ya kikao halali kinyume na kanuni za uendeshaji wa halmashauri. Kwa mujibu wa barua hiyo, chama hicho kinamtaka OCD huyo ajiuzulu au aondolewe.

  Chama hicho kimesema polisi ni watuhumiwa katika matukio ya Arusha, hivyo kama hakutakuwa na maridhiano serikali itakuwa imewalazimisha kuchukua hatua ya kuandamana.

  Yaliyokubaliwa:

  Katika barua yake Dkt. Slaa alieleza kuwa chama chake kinaheshimu mazungumzo yake na Bw. Tendwa na yale ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Bw. Said Mwema.

  "Kama tulivyokubaliana kati ya Dkt. Slaa na Bw. Tendwa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaratibu mkutano huo na kuwajulisha wahusika juu ya malalamiko ya CHADEMA," ilieleza barua hiyo.

  Mapendekezo ya CDM:

  Kimependekeza uitishwe mkutano wa majadiliano baina yake na viongozi wa juu wa serikali, ikiwezekana ahusike Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, viongozi wa TAMISEMI na kusitishwa kwa chaguzi za wenyeviti na mameya katika maeneo yenye utata.

  Kabla ya kuandamana:

  Kitaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuomba wananchi wa Arusha watulie hadi watakapojulishwa hatua zaidi, iwapo serikali haitakuwa imechukua hatua.

  "CHADEMA tumejitaidi kutuliza wapenzi wetu hata baada ya wananchi kupigwa mabomu na polisi bila sababu sasa tumechoka kunyanyaswa," alisema Dkt. Slaa.

  My take: Enough is enough.
   
 2. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Imekaa vizuri sanaa! Aluta!!! mapambano ya uhuru wa mtanzania ndiyo kwanza yanaanza!Together we can do it!
   
 3. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwaa tz yetu hii, atachemsha tu muda si mrefu
   
 4. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  good start to bring irresponsible responsible!!, nataka kujua kama maandamano ni yan nchi nzima au ni kwenye maeneo yenye utata?
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Good Move
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Who will be the first to sacrifice?
   
 7. d

  dicaprio Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  "a deaf can't be compelled to hear because that is his/her basic disorder "
  Muda unavyoendelea na giza linaanza kuondoka, watanzania tumieni fursa zinazojitokeza za
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,661
  Likes Received: 21,879
  Trophy Points: 280
  Uungwana unaoonyeshwa na Chadema hauna mfano. Ila serikali hii kwa vile hii ina viongozi wenye fikra tata hawalioni hilo.
  Pengine wananchi watakapo amua kufanya maandamano kupitia maeneo wanakoishi viongozi na familia zao ili kama fujo na uharibifu ukitokea uwaguse kwa karibu ndio wataingia woga. Ukitaka mtu mbishi akuelewe vizuri maumivu yaiguse familia yake.
   
 9. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  inabidi tuandamane nji nzima, siyo maeneo yenye utata tu.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,037
  Trophy Points: 280
  Usifikiri wanajeshi wote huwa jasiri wengine huwa wanajiharishia vitani, you just sleep and wait others to bring fruits for you.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  kazi ipo mwaka huu
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,037
  Trophy Points: 280
  Wametonesha kidonda cha uchaguzi kichoanza kupona tulitegemea tamko kama hili litolewe muda mrefu, Slaa usitusahau sisi wa Shinyanga tuko tayari hata leo bado tunakumbuka tulivyoibiwa kwa kura moja iliuma sana.
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli Slaa umeshikwa pabaya, na haya unayotaka kuanzisha hatuafikiani nayo, dola ikiwafanya vibaya sie hatumo, kwani huko ni kuichokoza dola kwa makusudi kabisa.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Kama wananchi wengi wakiwa na mawazo kama yako!!!
   
 15. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe unazungumzia TZ ipi? Acha kujidanganya.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Chadema ni wahuni tu! Imekula kwao!
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  That's right!!! Nchi nzima!!!!
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyu Slaa kashindwa uchaguzi sasa anataka watu wauwane.
   
 19. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sorry I know you don't wanna hear this... but that is a question frequently asked by cowards!!!
   
 20. a

  arasululu Senior Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu anayedai haki huitwa muhuni?
   
Loading...