Tusker project fame 6...usanii mtupu

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,814
Kweli kila kitu usanii. SHINDANO limeisha hivi punde, HOPE kutoka Burundi ndio mshindi, lakini walisema kuwa kura ndio zitaamua mshindi, toka shindano limeanza mpaka leo HISIA from TANZANIA liongoza kwa kura, tena alikuwa anawaacha wenzake mbali sana.

Cha ajabu leo ndio amekuwa wa mwisho, yuel dada wa Uganda kawa wa 3, wakati kwenye kura anakuwa nyuma ya HISIA kila siku, aliyeshinda anakuwa wa mwisho kwa kura kati ya waliokuwa wamebaki.

Je, kuna haja ya kuwaambia mashabiki wapige kura?

Au huko napo ni ubabaishaji kama BSS, japo kwa maandalizi na stage na kila kitu hawa jamaa ni kiboko!
 
Uko sahihi kabisa kuna usanii wa hali ya juu katika haya mashindano. Mshindi anaandaliwa kabisa. Hata nyimbo za mwisho za walizomchagulia hazikuwa nzuri kama wengine.
 
Hili shindano mi nililiona toka mwanzo kuna ubaguzi mkubwa sikidogo hawa watangazaji walikuwa hawawataki kabisa wabongo mi nafikiri next seeson wabongo wajitoe hakuna haja ya kuendelea na mashindano kama haya ambayo mshindi ana amuliwa toka mwanzo
 
Hata mimi kweli wamenikwaza,yaaan i knew Hisia Ndiyo mshinda,!!!I am very disappointed.
Ni wakati sasa Tanzania tuanze kampeni rasmi kupinga washiriki wa tz kushiriki hilo shindano,bali tuthamini vya kwetu i mean "BSS"japokuwa kwa shingo upande
 
Kweli kila kitu usanii. SHINDANO limeisha hivi punde, HOPE kutoka Burundi ndio mshindi, lakini walisema kuwa kura ndio zitaamua mshindi, toka shindano limeanza mpaka leo HISIA from TANZANIA liongoza kwa kura, tena alikuwa anawaacha wenzake mbali sana.

Cha ajabu leo ndio amekuwa wa mwisho, yuel dada wa Uganda kawa wa 3, wakati kwenye kura anakuwa nyuma ya HISIA kila siku, aliyeshinda anakuwa wa mwisho kwa kura kati ya waliokuwa wamebaki.

Je, kuna haja ya kuwaambia mashabiki wapige kura?

Au huko napo ni ubabaishaji kama BSS, japo kwa maandalizi na stage na kila kitu hawa jamaa ni kiboko!

Usilazimishe Umtakaye Wewe ndiyo Ashinde Kwani Hatuwezi Jua Pengine Wenzetu Wana Vigezo Vingi na Kusema Kuwa Tanzania Season Ijayo Tusishiriki Sidhani Kama ni Kauli Ya Hekima na Busara bali Tujiulize Wapi Mwenzetu Amekosea Kisha Tujipange Kuanzia Hapo Kwani Hata Kama Hisia Ameshindwa ila Amesaidia Kuitangaza Tanzania na Hata Kufungua Mlango Kwa Wengine Kuzidi Kufanikiwa na Kuitambulisha Tanzania Hususan ktk Suala Zima la Music industry. Alipofikia Mshiriki Wetu si Haba na Asikate Tamaa Kwani Ana Kipaji na Uwezo na Atafika Mbali Sana. Happy independence Day My Fellow Tanzanians!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom