Wakunyuti
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 380
- 13
Dk. 37, Simba 2 Prisons 0....Mgosi katwanga la pili.
Aminia Mgosi....
Dk. 37, Simba 2 Prisons 0....Mgosi katwanga la pili.
Roya Roy mi naungana na mawazo yako.... Hivi jamani hawezekani wakajitoa tu kwenye hayo mashindano mwakani, naona aibu tupu... juzi juzi nilisoma kwenye gazeti moja eti wanamuomba kocha mkuu wa Yanga awe mshauri wao kwenye mashindano mwakani mmh yangu macho......
wadau ,pambano la yanga na mtibwa vp?
Mtibwa 1 Yanga 0
Timu zote zina point 3 , zimefunga/fungwa goli 1.
Inabidi kupigwa kura kupata washindi 2 kesho (according to Kaijage)
Mtibwa 1 Yanga 0
Timu zote zina point 3 , zimefunga/fungwa goli 1.
Inabidi kupigwa kura kupata washindi 2 kesho (according to Kaijage)
Wakikusikia wenyewe hao.
Habari toka : NIFAHAMISHE Tanzania news portalBAO pekee la Zahor Pazi wa Mtibwa Sugar jioni hii lilitosha kuitoa Yanga kichwa chini katika michuano ya Kombe la Tusker na sasa timu hiyo haijuwi hatima yake iwapo imefuzu Nusu Fainali au la mpaka itakaposubiri kura hapo kesho asubuhi..
Pazi ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Idd Pazi Father, alifunga bao hilo katika dakika ya nane ya mchezo huo baada ya kuinasa kona iliyochongwa na Rashid Gumbo.
Mtibwa leo jioni iliwakilishwa na Shaaban Kado, Obadia Mwangusa, Idrissa Rajab, Chacha Marwa, Salum Sued, Shaaban Nditi, Zahor Pazi, Rashid Gumbo, Abdallah Juma, Uhuru Suleiman na David Mwantobe.
Yanga: Juma Kaseja, Shedrack Nsajigwa, Abdul Mtiro, Nadir Haroub Cannavaro, George Owino, Geofrey Bonny/Gaudence Mwaikimba, Shamte Ally, Nurdin Bakar, Jerry Tegete, Abdi Kassim na Mrisho Ngassa.
Kwa matokeo hayo, Yanga, Mtibwa na Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kesho asubuhi zitapigiwa kura kujua timu zitakazoingia nusu fainali za michuano hiyo. Timu zote zina pointi tatu na bao moja la kufunga na kufungwa.
...watamchuna ngozi?
Kanda2 mdebwedo!
Yanga kazi wanayo hata wakifata alphabeti
Mtibwa
Ura
Yanga
Duh...! Hii ni noma...Tumeshapigwa chini tayari! Kura za kuhuni za kwenye bahasha, Yanga tumeokata iliyoandikwa OUT! Kila la kheri watani wetu. Ndipo pa kumalizia hasira hapo.