Tusker Challenge Cup Updates

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Leo ilikuwa ni kati ya Mtibwa vs URA na matokeo ni kuwa Mtibwa wamelala kwa mabao 1 - 0.
 
Mtibwa yaanza vibaya kombe Tusker leo
MTIBWA Sugar ya Morogoro leo jioni imeanza vibayao michuano ya kombe la Tusker baada ya kuchapwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika pambano lililofanyika uwanja wa zamani wa taifa.

Kazi nzuri iliyofanywa dakika ya 55 na Tonny Mawejje, iliweza kuipa ushindi mtamu timu hiyo iliyotawala pambano hilo.
Katika michuano hiyo, kesho Tusker ya Kenya itaumana na Prisons kwenye mechi ya Kundi B, kabla ya bingwa mtetezi, Yanga kushuka uwanjani keshokutwa dhidi ya URA.

habari toka NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Leo Prisons ya Mbeya,Tanzania imefungwa 2-0 na Tusker ya Kenya...Timu za Tanzania mhh mbona zinaanza vibaya jamani,jana Mtibwa leo Prisons...Noma kweli
 
TIMU ya soka ya Prisons ya Mbeya jioni hii imeanza vibaya michuano ya kombe la Tusker baada ya kufungwa mabao 2-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mabao ya Tusker yalifungwa na Francis Oduor katika dakika ya 43 na la pili lilifungwa na Oscar Kadenge katika dakika ya 70.

Mchezaji Yona Ndabila wa Prisons alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 51 baada ya kuonyeshwa kwa mara ya pili kadi ya njano.

Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati ya Yanga na timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).

Habari na NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.


Tatizo la timu zetu liko wapi?
 
Simba 1 Prisons 0, dk. 28.
Mfungaji Ramadhani 'Redondo'.
 
Back
Top Bottom