Tusiwabeze wazungu, tunawahitaji na wanatuhitaji

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Kuitana Beberu sijui majina gani, haisaidii. Mbona tunasubiria takwimu zao kutuambia tumepanda au kushuka. Wakituambia tupo uchumi wakati sasa, nishangwe kila kona.

Ila wakituambia hatuna Demokrasia, tunanuna na kuanza kuwatukana. Tukitaka Ndege, tunawafuata wao, tukitaka uchimbaji twawahitaji wao, tukitaka ma V8 tuwahitaji wao, vifaa vya mahospitalini na zahanati, hakuna hata kimoja tunatengeneza hapa nchini, tunawafuata haohao ma beberu. Wakitusifia ni wazuri, wakitukosoa ni wabaya. Mhh!

Tunakuwa ni kama hatujielewi vile, laiti tungejielewa, tusingejaribu kujenga hoja kama hizi za ubeberu kwa wale tunaowategemea kwa asilimia 80 kwa vitu vingi. Hata kuwauzia nafaka zetu ni wao twawategemea.

Wenzetu wa China kuondokana na mabeberu, wakaamua kununua teknolojia toka kwa wazungu, nakupeleka vijana wengi kusoma huko ili warudi nyumbani na kutengeneza kila kitu uchina. Sisi hata robo hatujawekeza kununua teknolojia na kui implement hapa nyumba.

Watukane mabeberu, wakati huo wajitegemea kwa asilimia mia kwa kila kitu. Tanzania tuwe wapole kwanza kabla yakuanza viburi na kejeli dhidi ya wabia wetu. Tusitukane mamba kabla ya kuvuka mto. Tutumie busara sana viongozi wetu, na sio kuwa na viongozi wenye loose talks (kuropoka tuu) kufurahisha lay umati tuu na wasiojua Dunia inaenda vipi? wakati munaumizwa kama taifa.

Mfano, mlichukua za nini fedha za corona kama Tanzania hatuna huu ugonjwa? Mkiulizwa mrejesho wa hesabu za matumizi yake, tunachukia na kukasirika.

Busara na ungwana ni vizuri, tujitathimini sana kama Taifa, tunataka kupita njia ipi? Sisi sio kisiwa hapa duniani. Tunaihitaji Dunia zaidi kuliko Dunia inavyotuhitaji. Think about that? Ni mtazamo tuu!
 
Unaunyea mkono unaokulisha Tanzania tuna viongozi wa ajabu Sana ng'oeni mabango ya usaid na msaada wa watu wa marekani ndio muanze kuwaita mabeberu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom