Dhana ya Ubeberu na Siasa za Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,224
26,039
Amani iwe nanyi wadau!

Leo napenda nitoe Elimu kwa watanzania juu ya propaganda za wana CCM kuwa yeyote anayempinga Raisi Magufuli ni kibaraka wa Mabeberu. Wanasema haya wakitaka kujenga picha kwa watanzania ( wadanganyika) kuwa ubeberu ni kama dhambi au jambo fulani ambalo halifai. Najua kwa watanzania wenzangu wengi wetu Elimu kwetu imekuwa shida na kwa sababu hiyo wanasiasa wamekuwa wakitumia kutokujua kwetu katulisha mambo ambayo wao wanataka tuyaamini. Wanafanya haya kwa maslahi yao ya kisiasa

Asili ya Ubeberu ni nini hasa?

Kwanza kwa watanzania wasiofahamu, Dunia ya leo inaongozwa na pande mbili zinazopigana kila kukicha kutawala Dunia.

Pande ya kwanza inaongozwa na Marekani na washirika wake hasa nchi za Ulaya Magharibi na Scandnavia yaaani Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Canada, Sweden , Norway, Hispania, Ureno, Ubelgiji na washirika wao wengine. Hizi nchi zote zinaamini katika dhana ya maendeleo ya ubepari Yaani uhuru katika kuamua, kuwekeza na kumiliki.

Dhana hii hairuhusu serikali kukamata njia kuu za uchumi na inawapa nafasi watu binafsi kukamata njia kuu za uchumi. Dhana hii ina hatua yake ya juu ambayo wengi wanaiita kuwa Ubeberu. Kutokana na dhana ya ubepari/ ubeberu kuamini kwenye Uhuru wa watu katika maendeleo na kumiliki vitu nchi nyingi zenuw hii dhana raia wao wana maisha mazuri sana na wanaishi maisha ya kistaarabu sana na kuheshimiana.

Katika nchi hizi mtu unaweza kuwa tajiri wakati wowote kwa sababu kuna mifumo imara ya kuruhusu watu kukua kiuchumi na kimaisha ili mradi ufanye tu kazi na uwe na kipaji halali . Taasisi za hizi nchi ni imara na ndo zinawasimamia viongozi wa serikali. Viongozi hawana uimara kuzizidi taasisi zao. Na wakati wowote viongozi wanaweza kuwajibishwa.

Pande ya pili inaongozwa na Urusi na washirika wake ambao ni Venezuela, Cuba, Korea ya Kusini na nchi chache za ulaya ya mashariki. Hawa wanaamini kwenye ujamaa yani Sera ya serikali kumiliki njia zote kuu za uchumi. Nchi hizi haziamini kwenye Uhuru wa watu wao kwenye biashara, siasa, dini au maisha na hata ukiziangalia nyingi zimepiga Marufuku dini mbalimbali Tanzania Chama cha Mapinduzi nacho kinaamini kwenye Sera za ujamaa ingawa wao wanaamini kwenye uhuru wa dini Ila zile zinazokuwa chini ya uangalizi/ mkono wa serikali Mf. Bakwata.

Katika hizi nchi , nyingi raia wake wana maisha magumu sana kwa sababu wote wanategemea serikali ili kuishi na kukua. Kwenye nchi hizi huwezi kuwa tajiri kama serikali haijaridhia na wakati wowote hata ukiwa tajiri serikali inaweza kukufanya kuwa masikini. Wananchi wanaaminishwa serikali ni kama Mungu na haikosei. Watu wanaaminishwa kuwa kiongozi mkuu wa serikali hawezi kukosea. Vyombo vyote na taasisi za nchi lazima ziwe na utii kwa serikali na kiongozi wa serikali. Kwenye hizi nchi viongozi wa kisiasa ndo wanakuwa matajiri kuliko watu wa kawaida kwa sababu wao ndo wanakuwa na access ya vitu vizuri

Katikati ya hizi nchi kuna nchi kama China. Wao kisiasa wanaamini kwenye dhana ya Ukomunist ambayo haitofautoani sana na upande wa pili niliouelezea hapo juu ila kiuchumi wana mfumo wa kibepari/ ubeberu. China anafanya hivi kwa sababu alipeleka watu wake wengi Urusi na Marekani/ Ulaya ambao walisoma hizi dhana zote mbili na wakarudi kwao kutengeneza dhana yao.

Washirika wa Mabeberu

Hapa duniani Mabeberu/ Mabepari wana washirika wao pia. Washirika wa mabeberu ni nchi kama Korea kusini, Malyasia, Kuwait, Dubai, Saudi Arabia, Israel, Morocco, South Africa, Botswana, Ivory Coast, Ghana, Algeria, Singapore, Japan na wengineo wengi. Nchi hizi zote hizi kiujumla zimepiga hatua kubwa sana kimaendeleo hasa maendeleo ya watu na vitu. Kuna miundombinu ya uhakika, uwekezaji wa uhakika, fursa nyingi za ajira na kiwango kizuri cha elimu na teknolojia.

Washirika wa Wajamaa

Hapa kuna nchi kama Tanzania, Cuba, Venezuela, Korea ya kusini, Burundi, Congo, Sudan ya Al bashir, Sudan Kusini, Korea kaskazini na wengineo. Nchi hizi zote zina umasikini wa kutupwa na kuminywa kukubwa kwa haki za binadamu. Kuna umungu kwa viongozi wa mataifa na kiwango kikubwa cha kuzuia kukua kwa wananchi hasa wenye mawazo huru na mipango huru. Matajiri kwenye hizi nchi ni wale wanaojitoa kula na viongozi wa serikali na mara nyingi hawako stable kwa sababu wote wanategemea serikali na Viongozi wake. Vyombo vya maamuzi havo a Uhuru.

Hapa Tanzania Vyama viwili vikuu CCM na Chadema vimegawanyika kwenye mgawanyo huu. CCM wanaamini kwenye dhana ya ujamaa na Chadema wanaamini kwenye dhana ya Ubepari

Ewe mtanzania embu pata hii Elimu na ujue wanaosema huyu ni Bepari/ Beberu wanamaanisha nini na anayesema huyu mjamaa anamaanisha nini.

Mwisho niseme hakuna shida yeyote mtu kufuata dhana ya ubepari/ ubeberu ila kuna walakini mkubwa mtu anapofuata dhana ya ujamaa


Usisahau Kushare!!

Sambaza Upendo.

No hate No Fear!

Lord Denning
 
Pata madini haya ili tulikomboe taifa na wananchi kutoka kwenye utumwa wa fikra za kulishwa maneno ya uongo
 
Pata madini haya ili tulikomboe taifa na wananchi kutoka kwenye utumwa wa fikra za kulishwa maneno ya uongo
Kwa miaka mingi sana CCM imetawala hii nchi kwa propaganda zisizo na ukweli wowote ule. Ni wakati sasa watanzania wapewe ukweli wote na waamue wenyewe.
 
Madini kuntu haya.. buku 7 watasema umetumwa
Hakuna kutumwa ndugu. Hii ndo kweli itakayotuweka huru watanzania. CCM wamekuwa mabingwa wa kutengeneza propaganda chafu ili tu waendelee kuwatawala watanzania. Sasa inatosha ni lazima watanzania waelimishwe kuijua kweli.
 
I wish JF ingekuwa ni kama TV flani hivi ambayo inapatika a nchi nzima hadi vibibi na vibabu vya Nyang'wale, Matombo na Tandahimba wanayapata haya.
 
I wish JF ingekuwa ni kama TV flani hivi ambayo inapatika a nchi nzima hadi vibibi na vibabu vya Nyang'wale, Matombo na Tandahimba wanayapata haya.
Ni rahisi pia elimu hii kuwafikia kupitia wewe na mimi. Share kwa watu wengi uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi ndugu
 
I wish JF ingekuwa ni kama TV flani hivi ambayo inapatika a nchi nzima hadi vibibi na vibabu vya Nyang'wale, Matombo na Tandahimba wanayapata haya.
Elimu hii haiwezi kuwafikia bila mimi na wewe kuwafikishia. Share na watu wengi zaidi elimu hii na itawafikia tu!!!
 
Huu mtandao ni kama darasa unajifunza tu hadi raha.
Hii ndo raha ya JF. Hapa ndo utapata jibu kuwa kwa nini yule mtu alisemaga hadharani kuwa anatamani mitandao izimwe. Watu wengi wanaelelimika kupitia mitandao ndo mana watawala wenye hulka za kidikteta hawataki mitandao kama JF
 
Beberu kwa maana ya kisiasa ni imperialist, katika Kiingereza. Impeialist ni dola inayotawala mataifa mengine nje ya mipaka yake, au mtu mwenye fikra kama hiyo. Siku hizi kwa kweli hakuna wa 'imperialists' kwa dhahiri ingawaje msamiati huu pia hutumiwa kwa taifa au mtu anayetaka kuwatamalaki wengine kiuchumi, siasa na utamaduni.

Inabidi nifafanue hivi kwa vile neno hili, beberu, mabeberu, limerudi tena katika matumizi hasa baada ya uongozi wa wa awamu ya tano. Lilikuwa limesahauliwa tangu Ujamaa ulipokufa rasmi.

Katika miaka ya nyuma lilikuwa hasa latumika bega kwa bega na neno 'Mkoloni'. Mkoloni au wakoloni, ni watu walioletwa na nchi nyingine kuunda taifa lao, ikiwemo kuhodhi ardhi, katikati ya watu wa jinsi nyingine, na wakafanya juhudi ya kuwafukuzilia mbali wenyewe.

Imebidi nianze kwa utangulizi huo kwa vile yaelekea hivi sasa neno beberu, mabeberu yanatumiwa katika fahiwa potofu. Hii ni kwa sababu rais wa awamu ya tano alilitumia sana neno hilo, lakini bila ya kuwaeleza watu anamaanisha nini katika muktadha wa hivi sasa.. Hivi kwamba 'beberu' hivi sasa anaweza kuwa mwekezaji tu maadam si mtu mweusi! Watanzania wengi hivi sasa wamejazwa 'dhana ya kuonewa' kiasi kwamba imefikia hawakubali kuwa Mzungu (pengine Mhindi, Mwarabu...) anaweza kuja Tanzania kufanya biashara halali kabisa ili apate faida! Maadam ni wa rangi tofauti...ni beberu!

Humu mwenye JF neno beberu linatumiwa kila siku! Awamu ya tano imewafanya Watanzania wawe wabaguzi, wenye akili finyo, wanaoamini kwamba Tanzania haimhitajii yeyote! Yote haya yamefungashwa katika kapu la Uzalendo na dhidi ya Mabeberu!
Waingereza wamesema: 'Give a dog a bad name and hang it' Unapomchukia mtu kwa vile tu ni mtu fulani ( si kwa matendo yake)...ni rahisi zaidi kumdhuru.

NB. si dhamira ya thread hii kumkosoa rais wa 5 ambaye nampongeza na kumuenzi kwa mazuri mengi.
 
Mikataba yao ifikirie na usikilize watu wanavyooiga kelele ndo utajua Kama kuna ubeberu au ubia wa maendeleo
 
Aliyeleta ubaguzi huo wa neno beberu ni muathirika wa elimu ya ujamaa na alisoma zamani miaka ya 70 enzi za vita baridi hii dhana ya ubeberu, ukoloni mamboleo ziliasisiwa Urusi kwenye chuo cha patrick lumumba na Warusi kama kutengeneza saikolojiko bombs kwenye vichwa vya wafuasi wao Ili wawaunge mkono kwenye vita ya kugombea maslai ya kiitikadi duniani.Either uwe upande wa ubepari au ujamaa.

Mwalimu alichagua ujamaa mashuleni mitaala ikabadilishwa toka ya kibepari na kuwa ya kijamaa,zikapandikizwa chuki dhidi ya wazungu na malawama kedekede Ili tu uonekane ukoloni ulikuwa mbaya.

Mtawala aliyepita ni muathirika wa propaganda za kijamaa akaja na falsafa za kijamaa kwa kizazi cha sasa kinachoamini kwenye globalization baada ya kuisha kwa vita baridi huku upande wa ubepari au mabeberu ukiibuka kidedea.
 
Back
Top Bottom